Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,277
- 105,477
Ndo inabidi waanze sasa kuandika taifa bila kujua history ya kiongozi wako ni kazi bure
Haiwabidi waanze kuandika. Ukisema inawabidi unaweka shuruti ambayo haipo.
Swala unaloongelea ni pana.
Kabla ya kuanza kutaka viongozi na wanasiasa waandike vitabu, inabidi jamii nzima ithamini kusoma. Andy Chande kaandika kitabu cha maisha yake, tena kakiweka mtandaoni kila mtu mwenye PDF akisome buree, sijui wanachama wetu wangapi wa hapa JF wamekisoma, au hata wanamjua Andy Chande ni nani katika historia nzima ya Tanzania.
Kitabu kipo hapa
http://andychande.com/A_KNIGHT_IN_AFRICA_by_SIR_JKC.pdf
Mtu mwenye njaa ambaye siyo tu hana muda wa kusoma, bali hana hela ya ziada kununua kitabu, hawezi kuthamini kusoma. Hivyo tuna kwenda kwenye suala la uchumi.
Kama huna sheria kama "Freedom of Information Act" inayoshurutisha watawala kutoa habari kwa waandishi wa habari kwa mfano, watakaoanika maovu ya wanasiasa, huwezi kuwapa sababu wanasiasa kuandika vitabu vitakavyoelezea matukio kutoka upande wao.
Na hata kama una hizi sheria, kama unaandika maovu kila siku na watu hawafuatilii (apathy) ndio unaona watu kama rais Kikwete wanasema "Ni upepo tu huu, utapita" hata hawajitetei kwa kutoa tamko la kuachiwa Salva, seuze kitabu.
Utamaduni wa kurekodi mambo kwa maandishi hatuna tangu zamani. Tungekuwa nao tungekuwa na maandishi yetu.
Hatuwezi kuwa na utamaduni huu kwa kuwataka wakuu watufanyie hisani ya kutueleza siri zao. Frederick Douglas alisema "Power concedes nothing without a demand. It never did and it never will".
Sasa, huwezi kuwaomba wakubwa waandike siri zao vitabuni. Unatakiwa kuwataka, kivitendo.
Na umma usio elimu utafanyaje hivyo? Kwa kuanza na kujielimisha.