Utaliii

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Wakuu habarini!
Hapa nchini kwetu kuna vivutio vingi vya utalii na ni sehemu mbali mbali, kwa hili tumebarikiwa sana. Wazungu hutoka mbeli kuja huku na familia, marafiki , wachumba, wanandoa kuja kutalii tena kwa gharama nyingi! Je hapa tanzania ni asilimia ngapi ya familia (baba, mama na watoto), Wapenzi ((mke na mume)(GF & BF)) na marafiki hufanya utalii hata mara moja katika mwaka kufurahia pamoja katika mahusiano yao na kama ni asilimia ndogo vikwazo vikuu nini??? ni utamaduni, kipato ama ni nini? na tufanyaje ili tuweze kufanya hivi kama haifanyiki? :coffee::typing:
 
Mkuu tatizo ni kipato.
Nini kifanyike?
Maisha ya Mtanzania yakiboreshwa hilo swala litawezekana na tena sio kutembelea kwenye vivutio vyetu tu bali tutakuwa na nafasi ya kutembelea hata vivutio vilivyopo nje ya Tanzania na hata nje ya Afrika.
 
Bahati nzuri niko katika eneo ambalo naona kwa mapana sana flow ya watalii kuja na kuondoka. Mada uliyoanzisha ni sensitive , na inasikitisha sana kwa tulio wengi!...Utalii kwetu waswahili ni ndoto!...Hata watu wanaoishi jirani kabisa na Mbuga bado kabisa hawajawahi kupata msukumo wa kutembelea huko...Labda tuseme kiasili hatuna hobby hiyo, maana ingekuwa ni uchumi, mbona kuna rates za kibongo za kuingilia mbugani ambazo ni as low as 1.5K!..Lakini pia TANAPA HUWA WANATOA OFFER, AMBAPO mwitikio pia huwa chini sana!...Ni masikitiko!
 
Hili ni kweli kabisa! Maana mimi nionavyo zile pesa wapenzi au wanafamilia wanazozitumi katika starehe, kwenye mabaa, Mahoteli zinazidi hata gharama ya kwenda kutalii hasa waliokaribu na maeneo ya utalii, naona hii ipate kampeni kubwa ya kubadilisha mawazo na fikra za kwetu! Maana baa au kwenye hoteli utakuta ni starehe na hamna kubwa la kujifunza huko ila kwenye utalii kuna mengi ya kujifunza hasa katika familia kuna watoto ambao watajifunza mengi kuliko kwenda kwenye mahoteli na kuogelea tu:becky:
 
Bahati nzuri niko katika eneo ambalo naona kwa mapana sana flow ya watalii kuja na kuondoka. Mada uliyoanzisha ni sensitive , na inasikitisha sana kwa tulio wengi!...Utalii kwetu waswahili ni ndoto!...Hata watu wanaoishi jirani kabisa na Mbuga bado kabisa hawajawahi kupata msukumo wa kutembelea huko...Labda tuseme kiasili hatuna hobby hiyo, maana ingekuwa ni uchumi, mbona kuna rates za kibongo za kuingilia mbugani ambazo ni as low as 1.5K!..Lakini pia TANAPA HUWA WANATOA OFFER, AMBAPO mwitikio pia huwa chini sana!...Ni masikitiko!

PENYE MITI HAPANA WAJENZI.. WENGI WETU HATUNAUTAMADUNI WA KUJITUNZIA HELA KWA UTALII(MBGA SI ZIPO TU?!)!! ILA NI WATZ WANGAPI WANATUNZA HELA WAPATE NAULI ZA KUTIMKIA UGHAIBUNI?! :confused2:
 
PENYE MITI HAPANA WAJENZI.. WENGI WETU HATUNAUTAMADUNI WA KUJITUNZIA HELA KWA UTALII(MBGA SI ZIPO TU?!)!! ILA NI WATZ WANGAPI WANATUNZA HELA WAPATE NAULI ZA KUTIMKIA UGHAIBUNI?! :confused2:

Kwenda kufanya nini? kama kupata elimu ni jambo jema
 
JF members walishawahi kwenda trip ya southern circuit...

bado tunaweza zaidi kwa kuhamasisha utalii wa ndani

labda tunahitaji kampuni ambayo itakua focused mojakwamoja na utalii wa ndani badala ya kuchanganya na wazungu kwenye kampuni hiyohiyo maana miafrika kama kawa tukiona mzungu hata kama ni mwizi huwa tunampa priority
 
nadhani tatizo ni mwamko wa watu kuhusu utalii mimi binafsi nimefikiria sana hicho kitu (mimi napenda sana utalii wa ndani) baada ya kwenda Ngorongoro Crater peke yangu mwaka juzi baada ya hapo mwaka 2009 baada ya x-mas tulienda Rufiji River Camp na wife na watoto walifurahi sana kuona viboko, mwaka huu tumepanga kwenda Mikumi halafu nimefanya survey bei wala si kubwa kihivyo maana kutoka pale Mikumi Mjini hotelini mpaka Mbugani kutalii kwa masaa manne ni shilingi 120,000/- ukikodi Land Cruiser hotel room double ni Tsh 30,000 (Genesis Motel) na kuweka camp ni Tsh 20,000 ila tents ni zako. Na chakula chao buffet ni 10,000/- kwa sahani kwa hiyo kama ukijipanga na kudunduliza kwa mwaka mzima wala sio issue kabisa inachotakiwa ni kufanya savings na kupanga matumizi kwa nidhamu sio unasubiri kutafuta hela pindi jambo linaptokea

Pesa tunazotoa kwenye michango ya harusi kwa mwaka ni mara kumi au zaidi ya gharama ya kwenda mbugani mara moja kwa mwaka na asikwambie mtu mie nimefanya mara moja tu ila familia imefurahi mara milioni moja haswa watoto
 
Back
Top Bottom