Utajuaje kuwa unachoangalia ni filamu ya Bongo

Utajuaje kuwa unachoangalia ni filamu ya Bongo

Mimi ndo hua sina mda kabisa na hayo maigizo ya kibongo yaani yanachefua mpaka unahisi kutapika.
 
Lazima waigizaji wa kike wavae vinguo vya disco hata wakiwa ndani kwao
 
Tatizo movie softwares wanazotumia ni za buku jero.Hawana uwezo wa kununua.Kuedit movie uwe seriously umesomea.
 
Unachoongea kinaukweli lakini sio filamu zote. Binafsi najitahidi kuboresha.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums

Ni kweli mmefanya kitu ndiyo maana mnafanya makosa kwa kuwa ni wale tu wasiofanya kitu ndio hawafanyi makosa.
Kuna tatizo la waandishi wa hadithi ya sinema yaani scriptwriter kumbuka huyu ni mtu mwenye kipaji cha kuandika hadithi au kugeuza kitabu cha hadithi kuwa hadithi ya sinema
Na kuna waandika dialogue hawa ni muhimu kwa kuwa wanamlisha mane no muigizaji kuna maneno ya kuvutia mfano "matope yapo kisogoni yakifika usoni tutashindwa kutazamana" au
"Maisha yangu kama ya mbuzi kamba mbele fimbo nyuma" pengine "mwanamke ni kama mchanga wa bahari unavumilia kila mawimbi"
Haya maneno yanatengenezwa na Mwandishi wa dialogue
Kifupi mmefanya kazi nzuri katika mazingira magumu
 
Mke amelala na Mume wake, lakini Mmwamke mwilini amejikaza na taulo hadi kifuani then akitaka kuamka kitandani anajikusanya pamoja na shuka la kujifunika anakimbilia washroom kujisitiri..
 
Hahahahah kweli mkuu yaani ndio maana mimi si mpenzi kabisa wa hizo Bongo movie
 
Majambazi wote lazima wavae spy coats miwani nyeusi kama Yale ya kuchomea welding na ni lazima avute fegi
 
Mwenyenyumba utajua nyumba si yake bali wameazima kwani huwa harekebishi,AC,hagusi music system wala hafungui friji!
 
1.kuigizia kwenye majumba mazuri sana ..2.kuwa na title za kiingereza wakati ndani kiswahili..3.kuongea kama wanaimba ngonjera4.mtu mmoja kuwa na majukumu kibao..mfno.mtayarishaji yeye,mwandika story yeye,muongozaji yeye,dereva yeye ,muigizaji yeye nk.5 wakiigiza wanakula lazima chakula kiwe chips kuku6.kama muvi ni ya ngumi'pale mtu anaporusha ngumi au teke kuna mlio fulani hutokea utadhani wanagonga meza.7.maleba/mavazi hayaendani na husika anayocheza mwigizaji..8kila baada ya maneno mawili ya kiswahili linalofuata la kiingereza.....
 

1-walinzi wengi huwa ni comedians
2-tajiri anakuja kumpenda masikini
3-jambazi lazima awe anavaa miwani nyeusi na mvuta sigara na koti refu jeusi
4-wote wanaouwawa kwa bunduki hupigwa kifuani au tumboni sio kichwani
5-mtu yupo village,life gumu ana wave kichwani
6-wimbo wa malavidavi unaimba mpaka unaisha
7-nusu saa mtu anatembea, anakimbizwa, ananunua vitu
8-wakifika hotelini imezoeleka ni juice au wine isiyofunguliwa
9-madem wanaamka wana makeups usoni na hereni kabisa
10-part 2 ya movie ukiiona mwanzo unajua part 1 ilikuwaje
11-jini akifika barabarani anaangalia pande zote ndo avuke..!

Hahahaaaaaaa
 
[h=1][/h]

1- Walinzi wengi huwa ni comedians.

2- Tajiri anakuja kumpenda masikini.


3- Jambazi lazima awe anavaa miwani nyeusi na mvuta sigara na koti refu jeusi.


4- Wote wanaouwawa kwa bunduki hupigwa kifuani au tumboni sio kichwani.


5- Mtu yupo village,life gumu ana wave kichwani.


6- Wimbo wa malavidavi unaimba mpaka unaisha.


7- Nusu saa mtu anatembea, anakimbizwa, ananunua vitu.


8- Wakifika hotelini imezoeleka ni juice au wine isiyofunguliwa.


9- Madem wanaamka wana makeups usoni na hereni kabisa.


10- Part 2 ya movie ukiiona mwanzo unajua part 1 ilikuwaje.


11- Jini akifika barabarani anaangalia pande zote ndo avuke..!
 
-Kiingereza kibovu ajabu kwenye subtitles (Who are they trying to impress? I am sure they are not trying to translate the dialogues)
-Watu wote hufanikiwa kwa au (a) kupata msaada wa mtu tajiri/mwenye uwezo, au (b) kudondokewa na bahati fulani tu.
-Akishafanikiwa, anamsaliti mfadhili wake na hapo hukumbwa na mikasa.
 
Waigizaji kama mnahitaji angalau kupiga hatua moja mbele pitieni hapa manake walaji wamesema.
 
Mii nimeipenda hii: Hemed kapigana, kajeruhiwa, kufika hosp, kafungwa bandeji kibao, lkn mwl mzima bado yupo smart tena na mavazi yale yale ya kwenye tukio!
Bandages zimelowa damu, lkn damu yenyewe ni ya njano!
Kuna nyingine, Hemed kaiba file ndani ya gari supermarket, alivoona hamna hela, ni docs tu, kaamua kurudisha nyumbani kwa aliowaibia! Alipajuaje?
 
Back
Top Bottom