Utajuaje kuwa unachoangalia ni filamu ya Bongo

Utajuaje kuwa unachoangalia ni filamu ya Bongo

1 ~ actor anatumia nusu saa kutembea kuelekea kwenye gari na inatumia nusu saa mpaka gari lipotee mtaani.
2 ~ main actor wote ni wafanyabiashara na lazima wataongelea mizigo kutoka bandarini.
3 ~ main actor lazima akae nyumba ya. Gorofa.
4 ~ lazima waende supar market au kununua nguo.
5 ~ actress huwa hawwapiki chakula. Hata chai
 
Scene ya kulia inachukua dakika 30 ili kupata nafasi ya kutengeneza part 2 ya movie.
 
1. Mtu hata akipigwa mguuni damu hutoka mdomoni.
2. Hata mapigano yawe makubwa kiasi gani hawavunji TV wala redio.
3. Alie jinyonga humuoni mwili wote kwa mara moja, akioneshwa sehemu yakichwa haonyeshwi miguu na akioneshwa miguu aoneshwi kichwani.
 
*waigizaji ni walewale wa kila siku,
*mchana jua kali mwanga mwingi eti wanasema ni usiku
 
Ikiwa hakuna yeyote katika sisi tunaolalamika atachukua hatua basi hakuna kitakachobadilika na hivyo malalamiko yetu yataishia kuwa "Ugonjwa mpya wa Watanzania wa kulalamika bila kuchukua hatua." Sisi tunaokosoa tushike camera, mouse za kompyuta, taa, microphone, stand, cranes, make ups na tufanye kitu.

Ni kweli kuwa wakosoaji wanatakiwa lakini pia watenda kazi mahiri wanatakiwa pia. Marekani kuna James Cameron, Steven Spielberg, Digital Dmain, ILM etc, hao wakilalamika basi James Cameron anafanyia kazi malalmiko yao, huku nani anafanyia kazi ukosoaji wenu (wetu). Ninyi mliosoma Kompyuta tutengenezeeni effects nzuri tutatoa pesa, ninyi mnaosifu script ya Jack Bauer ama Jason Bourne tuandikieni nzuri basi. Sisi uwezo wetu umeishia hapo.

Tanzania ni masikini..... sawa.
Waigizaji ni vilaza........ sawa.
Yanga haina chochote.. sawa.
Hemed anaringa sana.... sawa.
Titanic ni noma............ sawa.
Waafrika ni masikini....... sawa.
Weusi unatokana melanin nyingi katika ngozi..... sawa.
China ni noma hata Marekani wanawaogopa..... sawa.
Iran ni noma, Israel watakoma.... sawa.
Malawi wanatuchezea hawa..... sawa.
Yule jamaa ni gamba tu.... sawa.

KISHA NINI?
 
Ni kweli mkuu, nilijizuia nisichangie chochote kwenye mada hii
lakini kutokana na mchango wako ninalazimika kusema machache.
Kiukweli katika wachangiaji wengi, na asilimia kubwa ya wanaojiita
wakosoaji wa filamu wa kiTanzania ni vilaza wa kutupwa kwa
kuwa wanakosoa jambo ambalo wao wenyewe hawalijui na wanaongozwa
na chuki badala ya taaluma. Sidhani kama ni sahihi kujiita wakosoaji,
badala yake wangeitwa wapondaji kwa kuwa mkosoaji siku zote
huonesha njia (namna ya kufanya) badala ya kuishia kuponda
tu bila kuonesha solution. Kwa mtu yeyote makini na anayeijua
tasnia ya filamu hawezi kukosoa sinema ya Kanumba (kwa mfano)
kwa kuilinganisha na sinema ya Denzel Washington, kwa vyovyote
atakuwa na matatizo ya akili. Kuendelea kulalamika au kuponda
bila kuchukua hatua hakutusaidii, sana sana ninachokiona hapa ni
kujaribu kuyahamishia matatizo yetu kwenye mitandao ya jamii
tukidhani kuwa tunatafuta solution...
 
Mimi sikubaliani na wewe. Mimi sio kilaza na wakiitwa vilaza sitakwenda mbele. Kama wewe ni msomaji mweye kumbu kumbu nzuri, utakumbuka siku za nyumba niliwahi kuuliza Lucy Kihwele anafanya nini kuwasaidia wasanii wa Bongo, kwa nini anaeleka cinema za Bongo MTV zikiwa na poor quality. Tumeshasema sana hapa, kwa nini wasanii wa Bongo wasiwape watu cinema zao wafanye editing, kuona obvious engilish mistakes? Tunaishia kupata aibu kubwa kwenye cinema za Bongo!

Tumeshasema sana, wakina Ray, kwa nini wasiajili watu watakaokuwa wanapitia scripts zao ili kuona kama zina mantiki?

Mkuu, hii thread haijaanzia hapa, soma threads za nyuma uone tumesema nini.
Hatuna jabza wala wivu na Ray, wengine hatutegemei hata siku moja kuingia kwenye hiyo tasinia.
Ila, tunasema kwa sababu tunaona, na hata wewe mwenyewe unaona!
This is true empty (ukweli mtupu)
 
Hawavunji hata glass bana!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kaka, nisichokubaliana nacho ni hiki: siku hizi kuna wimbi la wanaojiita wakosoaji wa filamu
ambalo limeibuka kwa kasi ya ajabu, wengi wamecharuka kuandika maoni na ujumbe mbalimbali
kupitia mitandao ya kijamii wakiponda sinema za Kitanzania kila kukicha pasipo hata kutoa
ufumbuzi wa nini kifanyike ili kuboresha kazi hizi. Ieleweke kuwa ukosoaji wa filamu duniani ni
uchambuzi na utathmini wa filamu, iwe kwa mtu mmoja mmoja au kwa pamoja. Kwa ujumla,
kazi hii ya ukosoaji wa filamu inaweza kugawanywa katika makundi mbalimbali kama vile mapitio
ya filamu yanayofanywa na waandishi wa habari ambayo huonekana mara kwa mara katika magazeti,
na njia nyingine maarufu, kupitia maduka ya usambazaji, au ukosoaji wa kitaaluma ambapo wasomi
na wanataaluma katika filamu hutoa taarifa na nadharia ya filamu na kuchapishwa katika majarida.

Wapitiaji wa filamu hufanya kazi kwenye magazeti, majarida, vyombo vingine vya habari, na
machapisho mengine kwenye mitandao, hasa hupitia kazi mpya zilizotoka karibuni au zilizo mbioni
kutoka ili kuuhabarisha umma. Na kwa kuichambua filamu kitaaluma na kuweka wazi mapungufu na hata
mazuri yake hasa kwa filamu ambazo zipo karibuni kutoka inaweza kuwa na impact kubwa katika kile
ambacho kama mapitio hayo yatakuwa yenye tija watu wataamua kuitafuta filamu.

Kwa vyovyote vile upitiaji mbovu (poor review) wa filamu au kutafuta makosa tu (kuponda) bila
kuangalia mazuri siku zote haujengi, na ndiyo chuki binafsi zinapoanzia. Katika siku za hivi karibuni,
mapitio na ukosoaji wa filamu nchini yamekuwa yakizua mjadala mkubwa, hasa pale wapitiaji na
wakosoaji hawa walio wengi wanapoonekana kulenga zaidi katika kuponda tu na kushindwa hata
kuyaona mazuri machache yaliyopo kwenye kazi husika jambo linalowachukiza waandaaji wa kazi hizo.

Kwa kawaida, kama ni mpitiaji au mkosoaji wa filamu, kabla hujaanza kutoa makosa ni lazima kwanza
ueleze yale mazuri (hata kama ni moja) uliyoyaona, kisha ndipo ueleze makosa uliyoyaona na kuelekeza
namna nzuri ya kuyarekebisha ili mtayarishaji, msanii au muongozaji husika asije akayarudia tena.
Hii ni aina nyingine nzuri ya kupeana darasa na inaweza kuwasaidia wasanii ambao hawakubahatika
kukaa darasani.

Badala yake tumekuwa tukishuhudia kuongezeka watu wanaojiita wakosoaji ambao kiukweli hawakosoi
bali wanaponda, inawezekana kwa chuki au kwa kutokujua pia. Ndiyo maana hushauriwa kuwa mkosoaji
wa filamu lazima awe na elimu ya filamu (narudia tena, LAZIMA awe na elimu ya filamu) ili iwe rahisi kwake
kuitazama filamu kitaaluma zaidi badala ya kuvutwa na shabiki.

Ni kweli kuwa watunzi wa filamu nchini hawana mafunzo maalum ya uandishi wa script, nddiyo maana
tatizo kubwa lililopo kwenye filamu (nyingi) za Kitanzania ni uwezo mdogo wa uandishi wa miongozo,
kitu ambacho kinasababisha filamu na michezo mingi ya kuigiza kuonekana kuwa haina muelekeo.

Pia waigizaji wa Kitanzania wengi ni wazuri katika uigizaji lakini si katika kuandaa miongozo ya filamu,
na kwa kuwa lengo ni kuzifanya filamu za Kitanzania kuwa na ubora, mnaojiita wakosoaji kwa pamoja
mngehimiza katika kuwataka waandaaji kupata mafunzo ya sanaa na uandishi wa script kwanza.

Sisiti kusema kuwa nina mashaka sana na uwezo ama mbinu mnazozitumia mnaojiita wakosoaji katika
kufikisha ujumbe wao, nina shaka kama kweli mnafanya tafiti za kutosha kuhusu sekta hii, na kama
mnafanya basi zitakuwa ni za juujuu tu. Huwezi kukosoa sinema za Kitanzania kwa kuzilinganisha na
za Hollywood, vinginevyo utakuwa na matatizo ya uelewa.

Kama kweli hawa wanaoponda wana nia ya dhati ya kutaka kazi za Kitazania ziboreke basi wanapaswa
kwanza kufanya tafiti za kina kabla hawajakimbilia kuziponda filamu za Kitanzania kwenye mitandao,
wao pia wanapaswa kusoma ili kuondokana na pazia la uzuzu linalowafunika usoni wakashindwa kuyaelewa
mazingira halisi ya tasnia ya filamu. Baada ya kuelimika na pia kujiridhisha na tafiti zao ndipo waanze
kutafuta njia sahihi za kuwasaidia watengeneza sinema na si kuishia kuponda tu.

Ni kweli kuna makosa katika filamu za Kitanzania, kati ya hayo yapo ambayo hayahitaji uwe na
bajeti kubwa bali ni ufahamu na ujuzi, na kuna makosa yanayosababishwa na ufinyu wa bajeti na
mfumo mbovu uliopo nchini.

Tuelewe kuwa kila fani ina elimu yake, sio mtu unakurupuka tu kwa kuwa umezoea kuangalia sinema
za Hollywood na Ulaya basi unajiona wewe ni mkosoaji wa filamu. Elimu ya filamu umeipata wapi?
Au na wewe uko kwenye ule mkumbo ule ule wa hao unaowaponda wa "usanii upo kwenye damu!"
Sijui ukosoaji nao ni kipaji? Au kwa lugha nyingine "ukosoaji upo kwenye damu!"

Katika elimu ya filamu hufundishwa nidhamu (academic discipline) inayohusu mambo mbalimbali ya
kinadharia, historia, na njia bora za uhakiki makini wa sinema (critical approaches to the cinema)...
 
1-walinzi wengi huwa ni comedians
2-tajiri anakuja kumpenda masikini
3-jambazi lazima awe anavaa miwani nyeusi na mvuta sigara na koti refu jeusi
4-wote wanaouwawa kwa bunduki hupigwa kifuani au tumboni sio kichwani
5-mtu yupo village,life gumu ana wave kichwani
6-wimbo wa malavidavi unaimba mpaka unaisha
7-nusu saa mtu anatembea, anakimbizwa, ananunua vitu
8-wakifika hotelini imezoeleka ni juice au wine isiyofunguliwa
9-madem wanaamka wana makeups usoni na hereni kabisa
10-part 2 ya movie ukiiona mwanzo unajua part 1 ilikuwaje
11-jini akifika barabarani anaangalia pande zote ndo avuke..!
 
Back
Top Bottom