Utajuaje kua asali imeathiriwa na nikotini?

Markomx

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2016
Posts
792
Reaction score
933
wakuu

napenda kufanya ulanguzi wa asali mikoa ya tabora pamoja na singida

ila changamoto ya hii mikoa hua inaathiriwa sana na maua yanayotokana na tumbaku ambayo hua na sumu ya nikotin ambayo huathiri sana soko la asali,

hivyo basi ningependa kupata ufafanuzi wa kuitambua asali yenye nikotini

msaada wenu
 
Huhitaji Kuingiwa na hofu.Study ya Kisayansi iliyosample asali toka Urambo na Same imethibitisha kwamba kiwango cha Nicotine ni insignificant (Kiasi kidogo Sana)
 
ila asali yenye nicotin biashara yake sokoni hua inasumbua kwa wateja,
kama unaelewa dadavua mkuu
 
wakuu

napenda kufanya ulanguzi wa asali mikoa ya tabora pamoja na singida

ila changamoto ya hii mikoa hua inaathiriwa sana na maua yanayotokana na tumbaku ambayo hua na sumu ya nikotin ambayo huathiri sana soko la asali,

hivyo basi ningependa kupata ufafanuzi wa kuitambua asali yenye nikotini

msaada wenu
Inakuwa nyeusi
 
Asali nzuri ina rangi ya kahawia,
Daah mkuu sa ntaijuaje kwamfano make wasambazaji hawana vifungashio maalum. Wengine wanahifadhi kwenye chupa za BALIMI EXTRA LAGER, asali ina display as if ni alcohol cha ndani hakijulikani!! sa mteja ntahakiki vipi? ukisema uimwage ili ujue brown ama nyeusi basi hiyo yako tayari!!
 
Asali ya mahali kama tabora panapolimwa tumbaku daima huwa na weusi fulani
 
Mkuu hii itakuwa ni ana anado!
chukulia tu kwa mfano nakutana na hawa wauza asali mjini kati kama city garden kwa pamoja wananivamia na bidhaa zao na zote zipo nyeusi nyeusi wanadai ni asali ya Kibaigwa! sa ntabagua vipi?
 
Kisima tena wale ndio wana asali feki kuliko feki yenyewe! Asali halisi bila kujali rangi yake ukimimina kidogo ukapiga kibiriti inawaka
Hebu ukionana nao tena jaribu hili
 
Kila asali ina Nicotine ya kiwango cha 0.005 ambacho hakina madhara kwenye mwili wa Binaadamu.
Sehemu wanazolima tumbaku kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa asali upungua, hii kutokana na dawa wanazozitumia kwenye zao hili nyuki ufa kwa kiwango kikubwa
 
Duh...hili swali ingefaa sana lijibiwe na Nyuki wenyewe, Binadamu watakulaghai tu.
 
Inakuwa nyeusi
Mkuu Mshana hapa umefyatua.
Rangi ya asali inategemea na msimu na mime iliyopo karibu
Kuna eneo huku Zanzibar linaitwa uzi,asali yake ni nyeusii,yaani inakuwa na weusi mwingi,wakati hata hayo mambo ya ukila wa mani cotin hatuna.

Ukanda wa pwani wenye Mikoko,asali yake nyingi huwa na asali yenye weusi mwingi na ni salama zaidi.Na ghali sana
 
Back
Top Bottom