Utajiri wa Mohammed Dewji (MO) na Kampuni ya MeTL umechangiwa na maamuzi ya Serikali ya awamu ya tatu

Ufunguo

JF-Expert Member
Aug 18, 2012
330
231
Mnamo mwezi wa 06 mwaka 2018, Mohammed Dewji alifanya Mahojiano na mwandishi mashuhuri wa maswala ya biashara ndugu MFONOBONG NSEHE (http://www.campdenfb.com/author/mfonobong-nsehe). Mahojiano hayo yalichapishwa tarehe 19/06/2018 katika tovuti ya CampdenFB.com (http://www.campdenfb.com/article/tanzania-s-titan-mohammed-mo-dewji). Lengo kuu la mahojiano hayo ni kuonesha mafanikio na changamoto za kibiashara za Kampuni ya MeTL.

Hizi ni baadhi ya dondoo za mahojiano hayo:

Mohammed Dewji (MO); Nilianza kujifunza biashara nikiwa na umri wa miaka 11. Nilikuwa nikiuza duka pamoja na Baba yangu pale SINGIDA. Wakati wa likizo Baba alikuwa akiniambia, "Mohammedi, hii ni biashara ya familia hivyo unatakiwa kujua mbinu".

MO; Nilisoma maswala ya biashara nchini Marekani na baadae nilipata kazi ambayo nilikuwa nalipwa kama dola 60,000 kwa mwaka. Ilikuwa pesa nyingi kwa Maisha ya Tanzania, lakini haikuwa kitu kwa Maisha ya Marekani hususani gharama za Maisha pale New York nilipokuwa naishi. Mambo yangu hayakuwa vizuri. Hivyo, nilimwomba Mzee awe akinitumia pesa kidogo ya kujikumu wakati naendelea kupambana na Maisha lakini Mzee alikataa kata kata. Alisema, kwanini nahangaika kutafuta vijisenti na kukuza uchumi wa Marekani badala ya kurudi Tanzania na kuendeleza biashara za familia na kukuza uchumi wa Tanzania. Baada ya Maneno hayo, mwaka 1998 niliamua kupaki mizigo na kurudi Tanzania. Nilifanya kazi kwenye Kampuni ya MeTL kama Chief Financial Controller.

MO; Nilikuja na wazo la kuanzisha biashara ya viwanda ili kuzalisha baadhi ya bidhaa muhimu. Nilishangaa kwanini nchi yangu ilikuwa ikinunua hadi sabuni na mafuta ya kula kutoka nje ya nchi wakati kulikuwa na fursa ya kuzalisha bidhaa hizo nchini. Hivyo, nilimshauri Mzee tuanzishe viwanda lakini alikataa. Mojwapo ya sababu ilikuwa ni swala zima la mtaji pamoja na uzoefu katika biashara hiyo.

MO; Ndoto yangu ya viwanda ilitimia Mwaka 2003. Wakati huo, Serikali ya awamu ya tatu ilichukua uamuzi wa kuuza viwanda vyote vilivyokuwa vikipata hasara na kuelekea kufilisika kutokana na uongozi mbovu, rushwa n.k. Mali hizi ziliuzwa kwa bei poa. Tulinunua viwanda, mashamba, magodown n.k. Kadri biashara ilivyozidi kupanuka ndivyo tuliendelea kununua mali zingine kutoka kwa makampuni na watu binafsi. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa sura mpya ya Kampuni ya MeTL.

MO; Makampuni makubwa ya Kilimo ya Kimataifa yamekuwa yakinijia kutaka kuwekeza katika kilimo lakini bado sijafikia uamuzi huo

MO; China haiwezi kushindana na mimi katika uzalishaji wa nguo. Kwa mwaka tunazalisha vitambaa vya nguo vyenye urefu unaoweza kuizunguka dunia zaidi ya mara 2,500.

Soma zaidi makala hiyo ili ujifunze mbinu za ujasiriamali pamoja na mchango wa Kampuni ya MeTL katika uchumi wa nchi ya Tanzania.

MO PIC 1.png
MO PIC 2.png


Sharing is Caring
 
Ni kanji aliyechangamkia fursa. Hamlaumu waliouza viwanda? Kama serikali imeshindwa kuviendesha ingeingia ubia lakini wachache wenye tamaa waliviuza kwa kufikiria 10%
Na tusiwateke watu kwa misingi ya wivu. Makosa ni ya Serikali ya Tanzania. Yeye alichangamkia fursa. Saizi ndo tunapata akili baada ya mali nyingi kumilikiwa na familia moja. Kazi sana nchi hii
 
Na tusiwateke watu kwa misingi ya wivu. Makosa ni ya Serikali ya Tanzania. Yeye alichangamkia fursa. Saizi ndo tunapata akili baada ya mali nyingi kumilikiwa na familia moja. Kazi sana nchi hii
Waliouza walifikiria maisha yao na familia zao. Si maisha ya Watanzania wote. Ninakumbuka kauli ya Mwalimu Nyerere kuwa “uongozi ni dhamana “.
 
Na warudishe mali zote walizojitwalia kutokana na utawala wao. Saizi watu wananyang'anywa ardhi na mali zingine kutokana na uzembe na matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi wetu. Hii siyo sawa. Wahusika wote wawajibishwe badala ya kuhangaika tu na matajiri
Si ndio maana huyu mmoja tulimteka na kum black mail ili aachie, utaona siku c nyingi mali zetu zinavyorudi, akikaidi tu zile video tulizomrekodi kule mafichoni tunaziachia. Dadeki
 
Waliouza walifikiria maisha yao na familia zao. Si maisha ya Watanzania wote. Ninakumbuka kauli ya Mwalimu Nyerere kuwa “uongozi ni dhamana “.
Watafutwe walipo warudishe mali za watanzania. Watanzania wengi hawana hata ardhi ya kulima, wengine wanaitumia tu kukopea mikopo na kuwakodishia wananchi. Haya yote ni mapungufu yanayotakiwa kufanyiwa kazi. Lakini mfumo wa kutatua changamoto hiz usiwe wa uonevu. Sheria na taratibu zizingatiwe.
 
Watafutwe walipo warudishe mali za watanzania. Watanzania wengi hawana hata ardhi ya kulima, wengine wanaitumia tu kukopea mikopo na kuwakodishia wananchi. Haya yote ni mapungufu yanayotakiwa kufanyiwa kazi. Lakini mfumo wa kutatua changamoto hiz usiwe wa uonevu. Sheria na taratibu zizingatiwe.
Hii ardhi Nyerere aliilinda sana mpaka aliwafukuza Lornrho Brothers walikuwa wakilima chai kwenye milima ya Usambara na Mafinga. Lonrrho walifungua kesi London. Tumekuja kuitoa kwa bei ya maandazi
 
Back
Top Bottom