Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi


mkuu umenigusa
 

Asante sana Lizzy kwa uchambuzi mzuri ni kweli kabisa hakuna cha bure na mali ya kishirikina huja kwa haraka na kwa wingi hivyo kuwavuta wengi
Mwanzoni unapokuwa tight na maisha huku ukizongwa na madeni kila kona na akatokea mtu akakupa mchongo wa namna hii usipokuwa na imani thabiti kwa Mungu wako huchomoi lakini sasa madhara huja huko mbeleni ambako sasa mambo yameshakuwa super na una heshima katika jamii unapotakiwa ukaactivate/ukaboost utajiri
 
Last edited by a moderator:

Kuna mzee mmoja kitaani kwetu ana kihoteli chake,maduka ya jumla,ila hanunui hata baiskeli au pikipiki kapewa masharti awe anatembea kwa mguu,au apande magari ya wengine,sometimes akienda vijijini ataembea zaidi ya kilomita hata 15 kwa miguu na kibrikface chake,

mwingine ana kihoteli wateja kibao ila kapewa mashari asioge wala kufua,nywele mpaka zimegeuka nyekundu njano hivi nguo hazina rangi Kama zimemganda,siku moja bwana afya akamkuta hotelini akaambiwa mwenye hoteli nani akajitambulisha,akafungiwa hoteli chake
 
Wapemba nao ni hatari ushuhuda wao niliupata kwa rafiki yangu mpemba lakini wao wanatumia zaidi majini na mapepo
​Mi naogopa sana hizi mambo,niwe tajiri jina,while sina furaha ya mali husika?inakuaje nna utajiri halafu moja ya sharti nisinunue gari?au nisipendeze?
 
Hili tumelisikia sana between utajiri na kutoa ndugu, kwa imani mimi siamini uchawi ingawa upo,
Najaribu kuuliza watu lakini sipati jibu kama wewe labda mshana jn atafanya utafiti huo

Mkuu nishafanya research mpaka nimeamua kupoteza tu cz design nimeona nikifatilia sana such stuff naweza nikawa tempted to try it. Lol

You know i dont wanna do that shit. Tehe... Patience and working smart is the talent. Hela za ndago sio issue Joh. Muamini Mungu.

Issue inakuja unajilinda vp na mafirauni kama hawa ??? Inabdi uwe fit kiimani pia. Imagine Mangi kakuficha ki mazingara kwenye store ya hardware. Noma sanaa Joh. Hahahaha
 
Haya mambo mwanzo huwa mzuri lakini ngoja mwisho wake mwenyewe utasanda! ukienda uchangani na kwa wakinga haya mambo yapo sana
 
wanasiasa muda huu wapo karibu kinoma na waganga na wagaguzi
 
Wachaga wanafanya sana kafara za damu

Wachagga ni kweli wanafanya hzo issue but zile ni mila (Mungu wa Asili) akina Musa, Ibrahim enzi hzo pia walikua wakitoa sadaka za wanyama. Ni mila na desturi kwa wachagga (Mara nyingi haitafuni watu).

Kama ni Mkristo (Lutheran) na uliwahi soma kipaimara miaka ya nyuma. Kuna topic inaelezea " Mungu wa Asili " as in beliefs za watu wa zamani kabla ya dini kuenea Africa (Dini ulio letewa na mzungu).

Tunachoongelea hapa ni Uchawi alias Ndumba. Issue za kishirikina (devil worshipping) mtu anafanya satanic things for unspeakable rewards.
 
Wapemba nao ni hatari ushuhuda wao niliupata kwa rafiki yangu mpemba lakini wao wanatumia zaidi majini na mapepo

Hivi kuna kitu kinaitwa mapepo au majini? Mi mzito kuamini.
 

Mungu yupo ila watu wanakosea kulazimisha wengine wamuabudu Mungu kwa njia wanazotaka wao.

Kama mtu akawa anaabudu Mungu kwa njia za kimila au kienyeji ni sawa. Sipendi mtu aniaminishe kuwa ukienda lugherani au ukatoliki au kwa mchungaji fulani ndo kuna Mungu.

Au zile dini za kutambiana ipi bora kuliko nyingine. Wengi wanakosea hapo.

Kama mababu zetu kabla ya kuja wakoloni waliweza kwenda milimani kusali na kuomba hadi ukame ukapotea au magonjwa ya ajabu yakaisha au wakafanikiwa katika kitu fulani basi wasiseme kuwa wanakosea sana.
 
Bulldog mapepo na majini Vipo na ni roho zinazotangatanga unaweza usiamini lakini kumbuka hata kwenye misahafu haya mambo yameongelewa kwa mapana yake
Kuna ile habari ya Bwana Yesu kuwaamuru mapepo wamtoke yule mtu nayo yakamuuluza tukitoka twende wapi? Akayaelekeza kwenda kwenye kundi la nguruwe ambao walitimka na kuingia baharini
 
Last edited by a moderator:

Duh
Hii ni noma!!!
 

Thank you. Sijawahi ona wachagga tukifanya mila kwa nia mbaya kama ni hvyo watu wangepiga kelele sanaa.

Kuna watu nawajua wamekua wakiugua kwa muda mrefu sanaa, hangaika kote, maombi kwa sana na hospitali, toa hela kibao, wapii hamna nafuu. Wamerudi Moshi wamefanyiwa mila wamepona wanadunda mpaka kesho.

Ivi vitu watu wana dharau ila vipo. Usione mwanao anafanya vitu vya ajabu ajabu ukasema zezeta au ana kasoro flan. See beyond what u see or understand under normal circumstances.
 
Wachaga wanafanya sana kafara za damu

Sanaaaa
Lkn watakubishia hapa!!!

Though si wao peke yao sikuhizi wengi tu wanafanya hivyo!!
Plus wakinga,wao hutoa mzaliwa WA 1 Mara nyingi,au wazazi
 
Acha tu watu wanatafuta hela kwa kila njia

Mamantilie ndio wanatulisha uchafu mwingi sana anadanganywa na mganga wake kuwa ukitaka uvute wateja wengi pikia chakula maji uliyoogea bila sabuni, basi utakuta mama na mdishi mkubwa wa maji hadi bafuni akifika huko atajitumbukiza mzimamzima na kujisugua na kujifyokonyoa mpaka kwenye naniliu halafu akitoka hapo maji yale machafu na uchafu wote ule ndio atayatumia kupikia vyakula na utakuta watu wamepanga msururu kwenye chakula chake wakikisifia kuwa ni kitamu sana HERI WANGEJUA
 
kujiuliza tu huyo mganga yeye mbona maskini? ila mwisho wa utajiri wa hivyo ni mbaya mpaka tena unaona huruma
 

Mengi yanayofanyika ukisikia hutakula kwa mamantilie,nilikaa manyara nikahadithiwa kwamba watu wanalogana kuna kitu kinaitwa kifafi waganga wanazidiana,ukipigwa kifafi biashara zako zinashuka mwingine anatake over huo mtaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…