Utajiri wa Kamanda Barlow Unatisha! Soma hapa...

Hizi mali za mashaka ni ushahidi kuwa watendaji wetu wengi ni majambazi wasioweza kutoa maelezo ya jinsi walivyochuma. Barlow maisha yake, kifo chake hata kipato chake ni picha ya majambazi wanaoifanya Tanzania iwe omba omba. Bahati mbaya ni kwamba jinai hii inaanzia ikulu hadi kwa mfagiaji.

Heri Mungu awapunguze wanangu wezi walionishinda ili wale wasafi hasa wakulima na wafanyakazi wa kipato cha chini wapunguziwe mzigo na madhara. Je hao nao wakipata nafasi watafanya nini? Zingatia sana hili Mtanzania. Vinginevyo unaweza kukuta unamchukia Barlow kumbe unajichukia mwenyewe.

respect..............
 
Suala la msingi hapa ni kufuatilia kujua kwa nini gari alilokuwa nalo namba zake ni batili, kwa maana kuwa namba hiyo hiyo inatumiwa na gari la mtu mwingine. Hali hii imeshamiri sana hasa katika mkoa wa Mbeya.

Sioni tatizo kwa yeye kuwa na nyumba za gorofa. Hivi ni kweli kuwa na gari tatu, nne tano au kumi ni utajiri? Hii ndiyo tafsiri ya utajiri kwa Tanzania? hizo nyumba hata tathmini hazifanyiwa kuweza kuestablish value zake lakini tunarukia tu huyu ni tajiri. Gari kuu kuu zinauzwa kwa fedha kidogo sana.

Umeeleza vizuri kuwa ana malozi ya mizigo yanayofanya biashara na bado unauliza hizo fedha amepata wapi? Tusitishe watu kuwa waoga wa kujiletea maendeleao kwa kigezo kuwa mishahara yao haiendani na mali walizo nazo. Si wote wameanza kazi wakiwa hawana kitu. Usimjaji mtu kwa kujiangalia wewe unapoanzia, kila moja ameanzia katika ngazi tofauti. Wapo walioanza kazi zao wakiwa na biashara tayari.
 
huyu mtu alikua mlafi w kilakitu,wake za watu,mali,madaraka etc,yawezekana waliomuua pia aliwazulumu

Inawezekana kabisa mkuu,yani hii nchi watu tuliowapa madaraka,wanayatumia kwa faida yao na ndugu zao,very sad!
 
Biblia inasema MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI. Si vizuri kuhukumu watu lakini inabidi maana hawa wezi wa mali zetu wanatuumiza sana.
 
Haya mambo ni ya kawaida sana kwa polisi. Kuna mjomba wangu mmoja aliwahi kuuziwa gari na watu fulani kule Moshi na alipouliza wapi kadi ya gari aliambiwa tunakutuma Dar ukamuone IGP fulani enzi hizo(jina nalihifadhi)atakupatia hiyo kadi basi huyo mjoma akaja akafikia kwangu.

Asubuhi akaniomba nimpeleke kwa huyo IGP, baada ya kuingia ofisini kwake alijitambulisha na akapokelewa kwa furaha sana na chai juu,akaandikiwa kiji-note aende kwa mkuu wa trafiki na vehicle inspector ambapo alipewa kibali cha usajili.

Tukaondoka hapo ofisini na baada ya siku chache mjomba wangu akapata kadi akasafiri zake kwenda Moshi. Hadi hivi leo ile gari ambayo ilikuwa mpya anayo na huwa anakuja nayo hapa Dar bila tatizo.

Hiyo ndiyo Tanzania jamani, mjenga nchi ndio mbomoa nchi.
 
Tukianza kufuatilia uwiano wa mali za wanasiasa na vipato vyao halisi sina uhakika kama kuna atakayesalimika, kikubwa sisi wananchi tujipange kuitwaa nchi yetu tena amabayo kwa sasa imetekwa na kikundi cha wezi wachache, tuichukue tuikabidhi kwa viongozi miongoni mwetu ambao tutawapa masharti namna ya kuiendesha, sisi sasa hivi kiongozi anafanya kosa la wizi au ufisadi akiambiwa ajiuzulu anawaambia waajiri wake(wananchi) sijiuzulu ngo!!
 
bahati mbaya, mtu tunayemzungumzia hayupo, laiti angekuwepo angeweza kutoa maelezo na kila mtu akaridhika. niliwahi kuzungmza na mtu mmoja ambaye anafanya kazi kwenye taasisi mojawapo ya fedha, alisema kamanda alikuwa mtafutaji, na kamwe hakuogopa kukopa. karibia kila taasisi inayokopesha pesa, yeye amekopa na alikuwa na marejesho mazuri. Hadi FINCA wanamjua mtu huyu.
 
Hata kifo chake kitakuwa kimesababishwa na mambo mengi ikiwemo dhuluma na wake za watu.
 
acha akiliza kitoto, je wanao uziwa dhamana zao hawakukopa? biashara ni zaidi ya kukopa au kuwa na mtaji
 
Huwa inaniudhi sana mambo haya yanapotajwa ama wakati mhusika hayupo madarakani au kafariki....Hii inaonesha bado kuna kulindana au kuna matabaka na ubabe wa hali ya juu unaooneshwa na tabaka la walionacho...
 
imekula kwake mali hazina majina yake,bora hata angekuwa anaandika ya watoto au mke wake,imekula kwake
hAKUNA KAMANDA WA POLISI ALIYETAWALA MWANZA NA ALIYEONDOKA MWANZA BILA YA KUJENGEWA NYUMBA NA WAFANYA MAGENDO na majambazi. Kapri point na nyakahoja , maeneo hayo yana nyumba nyingi sana za kifahari za makamnda wa polisi ambao baada ya kuripoti kituoni tuu, hualikwa kisiri na wafanya magendo na kukabidhiwa nyumba !

Hii ya kamanda Narlow, inafichua siri iliyokuwa imejificha kwa zaidi ya miaka 40 ! Ni adhabu ya kifo tuu kwa wezi na wala rushwa itakayo ijenga nchi hii.
 
Nchi hii inatakiwa tufike mahali kila mtu mwenye mali achunguzwe na hasa wafanyakazi wa serikali. wengi ni wapokea rushwa na ndio maana nchi haiendi mbele.
Hapa suala ni mfumo mzima umeoza. Tumeshaelezwa mara nyingi ya kuwa watu kama trafiki ni lazima kila jioni wawakilishe kwa mkubwa wao kiasi fulani cha mapato. TAKUKURU wakiamua kufanya kazi vituo vya Polisi vitafungwa,zahanati na hata mahospitali,IKULU,kote ni uozo tu.
 
Ukifuatilia wale wote wanaoisupport ccm wanautajiri/mali za kimagumashi za aina ya Barlow. Kiongozi mmoja aliwahi kusema "njoo ccm mambo yako yaende vizuri"
 
Mie kitu ninachoipendea nchi hii ni kimoja ......kila mmoja analalamika....wote...wananchi na viongozi wao wa kisiasa.......ccm na upinzani.....Hivi nani anayetakiwa kuchukua hatua za kuondoa hayo malalamiko???
 
Kuna tetesi kifo chake kimetengenezwa kwa sababu alikuwa anatajwa sana kuja kumrithi Said Mwema!Je ni kweli??
 
Back
Top Bottom