Utajiri wa jamii unaletwa na wafanyakazi, wakulima na wataalam wafanyao kazi

Jo Africa Tz

Member
Jul 23, 2019
10
10
Kwa maana jinsi hii...

Utajiri wa jamii unaletwa na wafanyakazi, wakulima na wataalamu wafanyao kazi. Ikiwa watachukua maisha yao katika mikono yao wenyewe, na kuchukua bidii katika kuyatanzua matatizo badala ya kuyakwepa, hapatokuwa na shida yo yote katika dunia ambayo hawatoweza kuishinda.

Lazima tuzitambue shida, tuzichambue na tupambane nazo. Hakuna njia zilizonyooka katika dunia; lazima tujitayarishe kufuata njia ambayo ina mizunguko na mipindo na tusijaribu kupata vitu kwa urahisi.

Isiwazwe kwamba mnamo ahsubuhi moja nzuri wapinga maendeleo wote watapiga magoti kwa hiari yao. Viongozi lazima waungane na umma mzima katika juhudi ya pamoja ya kuleta maendeleo. Shida ziko nyingi na zisipuuzwe. Mtu ye yoye anayeona upande mzuri tu lakini haoni upande wa shida basi mtu huyo hawezi kupigana vyema katika kazi ya kuijenga jamii yake.

Historia ya binadamu ni ile ya maendeleo yasiosita kutoka milki ya lazima kwenda milki ya uhuru. Mwenendo huu hauna mwisho. Katika jamii yo yote ambamo matabaka bado yapo, mapigano ya kitabaka daima hayatokwisha. Katika jamii isiyo na matabaka, mapigano baina ya vipya na vikongwe na baina ya ukweli na uwongo daima hayatokuwa na mwisho.

Katika mapigano ya kuendeleza uchumi na majaribio ya kisayansi, binadamu anafanya maendeleo ya milele na maumbile yanapata mabadiliko yasiyosita; daima hayabakii katika daraja hiyo kwa hiyo. Kwa hivyo, binadamu anataka milele awe akikusanya maarifa na aendelee kugundua, kuvumbua, kuunda na kusonga mbele. Fikra za kutoendelea, kutazamia misiba, kulegea legea na za kujiona na kujiridhisha zote ni za makosa.

Yeyote anayetaka kukijua kitu hana njia ya kufanya hivyo isipokuwa kufanya maingiliano na kitu hicho yaani kwa kuishi (kutenda) katika mastakimu yake. Kama unataka ujuzi, lazima ushiriki katika vitendo vya kuugeuza ukweli wa mambo. Kama unataka kujua ladha ya tunda, lazima uligeuze tunda kwa kulila wewe mwenyewe. Kama unataka kujua nadharia na njia za mapinduzi, lazima ushiriki katika mapinduzi. Ujuzi wowote wa kweli unatokana moja kwa moja na maarifa ya mtu. Ujuzi unaanza kwenye vitendo, na ujuzi wa nadharia unaopatikana kwa njia ya vitendo lazima tena urejee kwenye vitendo.

Ni wazi kwamba unapofanya kitu cho chote, kama hujaifahamu hali yake hasa, tabia yake na hahusiano yake na vitu vyenginevyo, basi hutozijua kanuni zinazoziendesha kitu hicho, au kujua vipi kukifanya, au kuweza kukifanya vyema.

Ikiwa mtu anataka kufanikiwa katika kazi yake, yaani kuyapata matokeo yanayotizamiwa, lazima azifanye fikra zake ziambatane na kanuni za ulimwengu uliotuzunguka; kama haziambatani, atafeli katika vutendo vyake. Baada ya kufeli, anapata masomo, anazitengeneza fikra zake kuzifanya ziambatane na kanuni za ulimwengu uliotuzunguka, na kwa njia hii anaweza kugeuza kushindwa kuwa kufaulu. Hii ndiyo maana ya "kushindwa ni mzazi wa kufaulu."

Udhanifu na Metaphysics ndio vitu rahisi kabisa katika dunia, kwa sababu watu wanaweza kuropokwa upumbavu kama wanavyopenda bila ya kuwa na msingi wa ukweli wa mambo au kuufanya ujaribiwe na ukweli wa mambo. Uyakinifu na upembuzi, kwa upande mwingine, ni vitu vinavyotaka jitihada. Lazima viwe na msingi wa ukweli wa mambo na vijaribiwe nao. Kama mtu hajachukua jitihada, basi yumo katika hatari ya kutelezea kwenye udhanifu na Metaphysics.

Siku zote lazima tutumie akili zetu na tufikirie kila kitu kwa makini. Wahenga walisema "Kunja uso na utagundua rai ya kufanya." Kwa maneno mengine, kufikiri sana kunaleta busara.

Kiongozi usingoje mpaka matatizo yamejirundika na kusababisha matata chungu nzima kabla ya kujaribu kuyatanzua. Viongozi lazima waende mbele ya vugu vugu, wasibaki nyuma yake. Tunachohitaji ni akili ya jitihada lakini iliyotulia na kazi ya bidii lakini yenye mpango.

Uchunguzi unaweza kufananishwa na miezi mingi ya uja uzito, na kutanzua tatizo huwa kama siku ya uzazi. Kulichunguza tatizo, hakika ni kulitanzua. Njia pekee ya kujua hali ya mambo ni kufanya uchunguzi wa jamii, kufanya uchunguzi wa hali ya kila tabaka la jamii katika maisha hasa.

Bila ya jeshi la umma, hapana cho chote cha umma. Jeshi lazima lihusishwe katika mpango wa maendeleo, sayansi na teknolojia. Jeshi lisiwe kimbilio la waliofeli elimu, bali liwe ni chombo cha uvumbuzi na ugunduzi wa mambo ya kisayansi zaidi. Iwe ni desturi ya kwamba wabunifu na wataalamu mbalimbali au watu wenye vipaji maalumu na uwezo mkubwa kiakili wapewe vipaumbele jeshini na si watu wenye manguvu ya kimwili wenye uwezo mdogo wa kiakili. Vitu vitengenezwe hapa hapa nchini, jeshi lihusike barabara. Jeshi na polisi wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano. Lakini katika suala la ulinzi wa taifa, inatakiwa kila raia apitie mafunzo ya kijeshi kwa lazima walau kwa miezi sita au mwaka mmoja. Kama kila raia atapitia mafunzo ya kijeshi, basi itakuwa ni rahisi kufanya mapinduzi ya haraka endapo kiongozi yeyote atakiuka katiba na kufanya kinyume na madaraka ya ofisi yake. Ulege lege wa wananchi hupelekea viongozi mashetani kufanya mzaha na maisha ya watu na hata watu hao kushindwa kujitetea. Kila kaya iwe ni kambi ya jeshi.
 
Acha dharau wewe. Usikariri ulofundishwa na walimu wako elimu yenyewe hii. Aliyemfundisha Mtume Paulo kuandika waraka alikuwa mwalimu wako? Format aliitoa wapi?
 
Tatizo si andiko, tatizo ni uelewa wa watu humu na chuki binafsi tu. JF wamelimit uwezo wa users kuedit headings za nyuzi zao. Wameruhusu tu users kuedit body na siyo title wala index. Sasa panapotokea posting errors, wanatoa loopholes kwa baadhi ya watu kukurupuka na matusi yao. Kwa bahati mbaya, wengine si wavumilivu, hujibu baya kwa baya, tit for tat is a fair game. Hivyo uongozi wq JF ufanye technical rehabilitation kwenye posting interface ya jamvi lao.

Users wawe huru kumoderate post zao wenyewe. Ila wana JF kama mtazidi kuonesha dharau kwa post za wenzenu ati kisa mnajiona magwiji sana, tutaelewana tu mwisho wa siku. I don't give a damn shit about anybody. Huwezi ukaanza kutoa lugha ya matusi halafu ukitukanwa unaona umeonewa,huo ni utoto na uchanga. Unapomtukana mtu uwe na kifua cha kustahimili majibu yake. So habari ndo hiyo. JF kama hamwezi kutoa option ya kudelete ama kuedit heading na index, basi nanyi kwenye jamvi lenu mna shida. Ponder on this.
 
Kwa maana jinsi hii....

Utajiri wa jamii unaletwa na wafanyakazi, wakulima na wataalamu wafanyao kazi. Ikiwa watachukua maisha yao katika mikono yao wenyewe, na kuchukua bidii katika kuyatanzua matatizo badala ya kuyakwepa, hapatokuwa na shida yo yote katika dunia ambayo hawatoweza kuishinda.

Lazima tuzitambue shida, tuzichambue na tupambane nazo. Hakuna njia zilizonyooka katika dunia; lazima tujitayarishe kufuata njia ambayo ina mizunguko na mipindo na tusijaribu kupata vitu kwa urahisi.

Isiwazwe kwamba mnamo ahsubuhi moja nzuri wapinga maendeleo wote watapiga magoti kwa hiari yao. Viongozi lazima waungane na umma mzima katika juhudi ya pamoja ya kuleta maendeleo. Shida ziko nyingi na zisipuuzwe. Mtu ye yoye anayeona upande mzuri tu lakini haoni upande wa shida basi mtu huyo hawezi kupigana vyema katika kazi ya kuijenga jamii yake.

Historia ya binadamu ni ile ya maendeleo yasiosita kutoka milki ya lazima kwenda milki ya uhuru. Mwenendo huu hauna mwisho. Katika jamii yo yote ambamo matabaka bado yapo, mapigano ya kitabaka daima hayatokwisha. Katika jamii isiyo na matabaka, mapigano baina ya vipya na vikongwe na baina ya ukweli na uwongo daima hayatokuwa na mwisho.

Katika mapigano ya kuendeleza uchumi na majaribio ya kisayansi, binadamu anafanya maendeleo ya milele na maumbile yanapata mabadiliko yasiyosita; daima hayabakii katika daraja hiyo kwa hiyo. Kwa hivyo, binadamu anataka milele awe akikusanya maarifa na aendelee kugundua, kuvumbua, kuunda na kusonga mbele. Fikra za kutoendelea, kutazamia misiba, kulegea legea na za kujiona na kujiridhisha zote ni za makosa.

Yeyote anayetaka kukijua kitu hana njia ya kufanya hivyo isipokuwa kufanya maingiliano na kitu hicho yaani kwa kuishi (kutenda) katika mastakimu yake. Kama unataka ujuzi, lazima ushiriki katika vitendo vya kuugeuza ukweli wa mambo. Kama unataka kujua ladha ya tunda, lazima uligeuze tunda kwa kulila wewe mwenyewe. Kama unataka kujua nadharia na njia za mapinduzi, lazima ushiriki katika mapinduzi. Ujuzi wowote wa kweli unatokana moja kwa moja na maarifa ya mtu. Ujuzi unaanza kwenye vitendo, na ujuzi wa nadharia unaopatikana kwa njia ya vitendo lazima tena urejee kwenye vitendo.

Ni wazi kwamba unapofanya kitu cho chote, kama hujaifahamu hali yake hasa, tabia yake na hahusiano yake na vitu vyenginevyo, basi hutozijua kanuni zinazoziendesha kitu hicho, au kujua vipi kukifanya, au kuweza kukifanya vyema.

Ikiwa mtu anataka kufanikiwa katika kazi yake, yaani kuyapata matokeo yanayotizamiwa, lazima azifanye fikra zake ziambatane na kanuni za ulimwengu uliotuzunguka; kama haziambatani, atafeli katika vutendo vyake. Baada ya kufeli, anapata masomo, anazitengeneza fikra zake kuzifanya ziambatane na kanuni za ulimwengu uliotuzunguka, na kwa njia hii anaweza kugeuza kushindwa kuwa kufaulu. Hii ndiyo maana ya "kushindwa ni mzazi wa kufaulu."

Udhanifu na Metaphysics ndio vitu rahisi kabisa katika dunia, kwa sababu watu wanaweza kuropokwa upumbavu kama wanavyopenda bila ya kuwa na msingi wa ukweli wa mambo au kuufanya ujaribiwe na ukweli wa mambo. Uyakinifu na upembuzi, kwa upande mwingine, ni vitu vinavyotaka jitihada. Lazima viwe na msingi wa ukweli wa mambo na vijaribiwe nao. Kama mtu hajachukua jitihada, basi yumo katika hatari ya kutelezea kwenye udhanifu na Metaphysics.

Siku zote lazima tutumie akili zetu na tufikirie kila kitu kwa makini. Wahenga walisema "Kunja uso na utagundua rai ya kufanya." Kwa maneno mengine, kufikiri sana kunaleta busara.

Kiongozi usingoje mpaka matatizo yamejirundika na kusababisha matata chungu nzima kabla ya kujaribu kuyatanzua. Viongozi lazima waende mbele ya vugu vugu, wasibaki nyuma yake. Tunachohitaji ni akili ya jitihada lakini iliyotulia na kazi ya bidii lakini yenye mpango.

Uchunguzi unaweza kufananishwa na miezi mingi ya uja uzito, na kutanzua tatizo huwa kama siku ya uzazi. Kulichunguza tatizo, hakika ni kulitanzua. Njia pekee ya kujua hali ya mambo ni kufanya uchunguzi wa jamii, kufanya uchunguzi wa hali ya kila tabaka la jamii katika maisha hasa.

Bila ya jeshi la umma, hapana cho chote cha umma. Jeshi lazima lihusishwe katika mpango wa maendeleo, sayansi na teknolojia. Jeshi lisiwe kimbilio la waliofeli elimu, bali liwe ni chombo cha uvumbuzi na ugunduzi wa mambo ya kisayansi zaidi. Iwe ni desturi ya kwamba wabunifu na wataalamu mbalimbali au watu wenye vipaji maalumu na uwezo mkubwa kiakili wapewe vipaumbele jeshini na si watu wenye manguvu ya kimwili wenye uwezo mdogo wa kiakili. Vitu vitengenezwe hapa hapa nchini, jeshi lihusike barabara. Jeshi na polisi wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano. Lakini katika suala la ulinzi wa taifa, inatakiwa kila raia apitie mafunzo ya kijeshi kwa lazima walau kwa miezi sita au mwaka mmoja. Kama kila raia atapitia mafunzo ya kijeshi, basi itakuwa ni rahisi kufanya mapinduzi ya haraka endapo kiongozi yeyote atakiuka katiba na kufanya kinyume na madaraka ya ofisi yake. Ulege lege wa wananchi hupelekea viongozi mashetani kufanya mzaha na maisha ya watu na hata watu hao kushindwa kujitetea. Kila kaya iwe ni kambi ya jeshi.
Nimeipenda sana mada hii. Imejaa fikra yakinufu. Hongera sana.
 
Back
Top Bottom