SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,836
- 1,845
Miaka kadhaa iliyopita tulipewa taarifa ya ugunduzi wa ma million cubic ya ujazo ya gesi asilia, na moja kwa moja viongozi wa nchi wakatuambia sasa umasikini ndo bye bye. Wimbo maarufu ulikua uchumi wa gesi, huku mahubiri ya kisiasa yakichagizwa na matumaini kwa watanzania kuwa wakati wetu wa kuuaga umasikini umewadia.
Nani asiyemkumbuka Prof. Muhongo alivyosimamia mahubiri haya, lakini pia serikali ya CCM ilivyofikia hadi hatua ya kupeleka Polisi na Jeshi kudhibiti watu kule Kusini ili uchimbaji wa gesi ufanikiwe. Ziara zikafanyika nchini Algeria na Urusi ili kupata uzoefu wa kuendesha uchumi wa gesi.
Cha kushangaza, hakuna tena anayeongelea kuhusu uchumi wa gesi wala kuuaga umasikini kupitia uchumi wa gesi.
Huu utajiri wa gesi umepotelea wapi hivi?