Utajiri wa Babu Loliondo kufilisiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajiri wa Babu Loliondo kufilisiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Wa kusoma, Dec 2, 2011.

 1. Wa kusoma

  Wa kusoma JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,321
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280

  MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi’ (pichani), anaendelea kusakamwa na wagonjwa wanaodai hawakuponyeshwa na dawa yake, wapo walioweka nia ya kumburuza mahakamani lakini mpya ni pendekezo la kumfilisi.


  Madai hayo yanakuja wakati ambao Babu Ambi ameukata, ameshakamilisha ujenzi wa nyumba yake ya kisasa kijijini Samunge, pia anamiliki magari mawili ya bei mbaya, Toyota Land Cruiser (pick-up) na Isuzu (pick-up).

  Babu Ambi, ameshahama nyumba chakavu aliyokuwa anaishi zamani na sasa anaendesha maisha yake kwenye mpya ya kisasa ambayo kwa Samunge, inaonekana ni kama Ikulu kwa jinsi inavyomeremeta.

  Wakati Babu alizoea kukanyaga vumbi kwenye nyumba yake ya awali ya udongo, yenye chumba kimoja cha kulala, hivi sasa anatembea juu ya sakafu iliyotandikwa vigae (tiles) kila eneo.

  Nyumba ya Babu, pia ina kila kitu ambacho hustahili kuwemo kwenye nyumba ya kisasa yenye hadhi ya mtu mwenye fedha, vile vile ina umeme wa mionzi ya jua na maji ya uhakika.
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  jioteshe dawa na wewe
   
 3. i

  ibange JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mwacheni babu wa watu kwani alilazimisha watu waende? Kwanza alisema ni matibabu ya kiimani
   
 4. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanamwonea wivu babu wa watu bure, kama mumeshindwa kuwaburuza mahakamani na kuwafilisi mafisadi waliokula mabilioni ya wapiga kura kwanini mmufilisi babu ambaye yeye kachukuwa 500/= tu?
   
 5. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  kwani mlilazimishwa kwenda kwa babu?wajinga ndio waliwao'mbona wengine hatukwenda kwake?majungu hayo
   
 6. babad

  babad Member

  #6
  Dec 2, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama watamfilisi waanze kwanza na wachungaji wanaotembelea magari ya kifahari kwa hela za wenye imani wao kama Rwakatare,Kakobe,Lusekelo,Mwingira.Hakuna aliyelazimishwa kwenda na inawezekana ambao hawakupona imani yao ilikuwa haba
   
 7. brightrich

  brightrich Senior Member

  #7
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwacheni babu wa watu, kwanza alisema hiyo tiba ni IMANI, halafu mlitumwa kwenda huku kunywa dawa? Babu aliwaita? Mkome viherehere vyenu. Wafilisini waliochukua majasho ya wananchi (EPA) sio babu wa watu.
   
 8. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wawafilisi madereva waliotoza nauli kubwa
   
 9. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Walalamikaji wanadai nini? TShs 500 au gharaza za nauli?
   
 10. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata na mimi nashindwa kujua madai yako ya msingi ni nini? lakini pia ni hospitali ngapi walishakwenda wakatibiowa bila kupona na je walienda kuwadai madaktari gharama za matibabau?
   
 11. HT

  HT JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yep, wakiambiwa hawakusikia...walijipeleka wao wenyewe. Wakaifilisi serikali yao tukufu waliyoisikiliza!
   
 12. F

  FUSO JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  go babu go..........kiendacho kwa mganga...
   
 13. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Mganga wa kienyeji kama Babu wa Loliondo harudishi kitu.Sisi waona mbali tulisema humu jamvini.Tukapuuzwa sana na kusemwa sana.Babu ni mganga wa kienyeji tu.Hana lolote.Imekula kwao hao wadai.
   
 14. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  tULIWAAMBIA TOKA MWANZO KUWA HUYO NDAGA FIJO NI TAPELI WATU WALIBISHA TENA KWA DHIHAKA KUBWA HUMU HUMU JF ,BABU ALIKUWA MJANJA ALITUMIA NJIA YA DINI KUWAINGIZA WATU MKENGE.

  HUMU NDANI JF WATU WANA KASUMBA YA DINI HATA KAMA WAKIONYWA VIPI HAWASIKII KWA KUWA KWA NJIA MOJA AU NYINGINE DINI ZAO ZINAGUSWA.

  PIA HAITOSHI KUMBURUZA BABU PEKE YAKE BALI HATA KANISA LA KILUTHERI NA ASKOFU LAIZER NAO WABURUZWE MAHAKAMANI KWANI NAO WALINUFAIKA NA MGAWO NA MWISHO SERIKALI KUPITIA KWA WAZIRI LUKUVI NAYO IBURUZWE VILEVILE.

  KIKO WAPI BANDUGU NATARAJIA NIONE TENA HUMU JF WATU WALE WALIOKUWA WANASHUPALIA KUWA DAWA YA HUYO BABU NI MUUJIZA NA INAFANYA KAZI, WAJITOKEZEE
   
 15. Wa kusoma

  Wa kusoma JF-Expert Member

  #15
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,321
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280