Mkenya aandika kitabu akikiponda "kikombe" cha babu wa Loliondo adai kiliua watu wengi badala ya kuwaponya

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
26,300
Points
2,000

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
26,300 2,000
Raia mmoja wa Kenya ambaye ni muathirika wa HIV aids ameandika kitabu akielezea safari yake ya Samunge Loliondo alikoenda kunywa kikombe cha babu mchungaji Mwaisapile.

Mkenya huyo adai kikombe cha babu hakikuwa na uponyaji wowote kwani yeye hakupona na wengi alioenda nao kutokea Kenya walikufa baada ya kurejea nyumbani.

Katika makala iliyorushwa na Citizen tv wamehojiwa watu wengi wakiwemo waliokwenda kutibiwa na wale waliopeleka wagonjwa wao huko Samunge.
Wengi wameonyesha kumlalamikia Mwaisapile aka babu wa Loliondo kuwa aliwatapeli.
Source Citizen tv

My take; Walioenda kwa babu waliponywa kwa imani zao!

NB: Mahojiano yataendelea leo Jumatatu ambapo mchungaji Mwaisapile aka babu wa Loliondo ataelezea maono yake. Saa 3 usiku Citizen tv!

Up dates: Ghosts of Loliondo part 2

Babu wa Loliondo anasema wakati ule alipokea wageni kutoka pembe zote za Dunia waliokuja kunywa dawa
Babu anasema Mungu alimtokea katika ndoto akamwonyesha dawa ya kutibu ukimwi.

Mchungaji Mwaisapile anadai wale wanaosema watu wamekufa wanamwonea wivu na miongoni mwao ni viongozi wa Kanisa na waganga wa kienyeji.
 
stinger_bug

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2019
Messages
859
Points
1,000

stinger_bug

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2019
859 1,000
Watu walikuwa hawafi kabla ya kuja hicho kikombe?

Umeacha dawa hospitalini na kwenda kunywa mataputapu huko porini, ukifa utasema umerogwa au umejiua kwa upumbavu wako.
Huu ni utapeli. Huyu babu Mwasapile makazi yake yanayomfaa ni katika gereza mojawapo huko Arusha au lile la karanga pale Moshi.
 
Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Messages
22,648
Points
2,000

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined May 11, 2015
22,648 2,000
Tatizo matatizo yenu huwafanya muache kutumia akili na kutumia akili za wengine.

Babu alikutapeli nini afya au pesa?
Huu ni utapeli. Huyu babu Mwasapile makazi yake yanayomfaa ni katika gereza mojawapo huko Arusha au lile la karanga pale Moshi.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
33,295
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
33,295 2,000
My take; Walioenda kwa babu waliponywa kwa imani zao!
Mkuu Yohana Mbatizaji, aka John the Baptist, asante for this, this is the bottom line, "Walioenda waliponywa kwa imani zao". Hata Bwana wetu Yesu Kristo, alipofanya miujiza ya uponyaji, aliwaambia walioponywa, "imani yako ndio imekuponya", wenye imani ya uponyaji, walipona, walipona, akiwemo fulani ambaye naomba nisimtaje, ili watu wasijiulize, "kumbe hata huyu alikuwa ni mgonjwa!". And I am very sorry, kwa wasio imani, walikufa.

Kinachoponya sio kikombe cha Babu, ni imani yako.
P
 
Mokaze

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2018
Messages
4,518
Points
2,000

Mokaze

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2018
4,518 2,000
Hata Bwana wetu Yesu Kristo, alipofanya miujiza ya uponyaji, aliwaambia walioponywa, "imani yako ndio imekuponya"

Huyo aliyesema hivyo ni Yesu nabii wa Mungu, je Mwasapile alikuwa nabii wa Mungu hadi aweze kuponya watu kwa kumuamini??!!------ the Mwasapile calibre= the Jesus calibre??!🤔
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
33,295
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
33,295 2,000
Huyo aliyesema hivyo ni Yesu nabii wa Mungu, je Mwasapile alikuwa nabii wa Mungu hadi aweze kuponya watu kwa kumuamini??!!------ the Mwasapile calibre= the Jesus calibre??!🤔
Yes ni nabii, hata humu jf tuna manabii kibao, tatizo ni nabii huwa hakubaliki nyumbani kwao.

P
 
Mokaze

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2018
Messages
4,518
Points
2,000

Mokaze

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2018
4,518 2,000
Tupo tunaopeta hadi Leo akiwemo mzalendo no.1

Hakuna cha kupeta hapa, ukishakunywa kile kikombe na kwa wengine akili zao haziwi sawa, siyo wote ni baadhi.

Wizara ya afya ilitakiwa ifanye utafiti kuhusu jambo hilo. (the body effect after using the medicine). Hadi leo kimya kabisa wakati baadhi ya watu wamedhurika hasa kiakili.

Kisheria alitakiwa Mchungaji akajibu mashitaka ya utapeli,--- hadi sasa kulingana na idadi ya vifo he seems not being apologetic. Sadly in the course he got lots of money.🤣🤣
 
Blac kid

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Messages
4,436
Points
2,000

Blac kid

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2012
4,436 2,000
Hakuna cha kupeta hapa, ukishakunywa kile kikombe na kwa wengine akili zao haziwi sawa, siyo wote ni baadhi.

Wizara ya afya ilitakiwa ifanye utafiti kuhusu jambo hilo. (the body effect after using the medicine). Hadi leo kimya kabisa wakati baadhi ya watu wamedhurika hasa kiakili.

Kisheria alitakiwa Mchungaji akajibu mashitaka ya utapeli,--- hadi sasa kulingana na idadi ya vifo he seems not being apologetic. Sadly in the course he got lots of money.🤣🤣
Nakubaliana na wewe mkuu make mzalendo no.1 nami namtilia mashaka kuhusu side effects.
 
msindikizaji

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2010
Messages
1,410
Points
2,000

msindikizaji

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2010
1,410 2,000
Mkuu Yohana Mbatizaji, aka John the Baptist, asante for this, this is the bottom line, "Walioenda waliponywa kwa imani zao". Hata Bwana wetu Yesu Kristo, alipofanya miujiza ya uponyaji, aliwaambia walioponywa, "imani yako ndio imekuponya", wenye imani ya uponyaji, walipona, walipona, akiwemo fulani ambaye naomba nisimtaje, ili watu wasijiulize, "kumbe hata huyu alikuwa ni mgonjwa!". And I am very sorry, kwa wasio imani, walikufa.

Kinachoponya sio kikombe cha Babu, ni imani yako.
P
Unataka kuniambia kuna waliojifungasha na kutoroka hospitali kwenda kunywa kikombe cha babu bila kuwa na imani??? Waliacha dawa za hosp wakiamini zaidi kiombe cha babu. Ilikuwaje wasipone na huku walienda kiimani zaidi.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
33,295
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
33,295 2,000
Unataka kuniambia kuna waliojifungasha na kutoroka hospitali kwenda kunywa kikombe cha babu bila kuwa na imani??? Waliacha dawa za hosp wakiamini zaidi kiombe cha babu. Ilikuwaje wasipone na huku walienda kiimani zaidi.
Hao walikuwa desperate kupona tuu, kuwa desperate sio lazima kuamini, wao shida yao ilikuwa ni kupona tuu, na sio kuamini, imani yao ilikuwa ya mashaka.

P
 
Mokaze

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2018
Messages
4,518
Points
2,000

Mokaze

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2018
4,518 2,000
Hao walikuwa desperate kupona tuu, kuwa desperate sio lazima kuamini, wao shida yao ilikuwa ni kupona tuu, na sio kuamini, imani yao ilikuwa ya mashaka.

P

Unataka kusema watu wa kuwatia imani wagonjwa leo hawapo??--- yaani imani imepotea kabisa duniani?!!
 
WAKO WAPI WATU WAKO

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2017
Messages
1,433
Points
2,000

WAKO WAPI WATU WAKO

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2017
1,433 2,000
Yes ni nabii, hata humu jf tuna manabii kibao, tatizo ni nabii huwa hakubaliki nyumbani kwao.

P
Watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa...hivi Jiwe alikunywa kikombe cha Babu? ..... Siamini kama jiwe linaweza kuugua... Jiwe halina uhai... Babu wa Samunge ni Nabii wa nyakati hizi....awe wa uongo au vyoyote ni Nabii wa Nyakati hizi..... Tule Konyagi Kama Ndg, Lusekelo
 
iamokay

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2019
Messages
344
Points
1,000

iamokay

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2019
344 1,000
Ile kitu ilikuwa ya kiimani zaidi. Mzee anakwambia lazima wote waje kunywea dawa hapahapa kijijini kwangu.
Nimeoteshwa watu kutoka mataifa ya mbali watafika mahali hapa kuja kunywa dawa.
Mliamini katika ndoto za mzee, tulieni.
Hivi mnajua hata dereva wa lori pia alikunywaga kikombe? Eeeh alikunywa ndio, unasema, kiongozi wa malaika? Eheh huyo huyo.Mbona yupo bado, tena nasikia alipona kabisa.
 
Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2017
Messages
1,171
Points
2,000

Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2017
1,171 2,000
Mkuu Yohana Mbatizaji, aka John the Baptist, asante for this, this is the bottom line, "Walioenda waliponywa kwa imani zao". Hata Bwana wetu Yesu Kristo, alipofanya miujiza ya uponyaji, aliwaambia walioponywa, "imani yako ndio imekuponya", wenye imani ya uponyaji, walipona, walipona, akiwemo fulani ambaye naomba nisimtaje, ili watu wasijiulize, "kumbe hata huyu alikuwa ni mgonjwa!". And I am very sorry, kwa wasio imani, walikufa.

Kinachoponya sio kikombe cha Babu, ni imani yako.
P

Huyooo fulani sasa hapo ndipo nilipo paona naomba nitoe angalizo kuhusu hili ...

Guuku!!! Nicheke kwanza Ha ha haaa ... kwa maana hiyo unataka kutuaminisha kuwa kweli huyo fulani kapona ...!!! na kwamba tuamini kuwa anayo Imani ya kweli kupitia kikombe cha Babu kilicho hitaji Imani ya kweli ili upone ...

Mh! Umenihamasisha sana hapo kwenye dokezo la Yesu na swala kupona kwa Imani japo Yesu hakutumia kikombe nafikiri, labda kama sifaham maandiko yanasemaje ...

Pia nimezidi kuhamasika ninapo jaribu kukumbuka kuwa Babu alikua ni mchungaji lakini pia dawa hiyo alioteshwa na roho mtakatifu ...

Sasa najiuliza Imani iliyohitajika katika uponyaji kupitia kikombe cha Babu ilikua ni kwa mlengo upi???

a) Je, ilihitajika Imani ya dawa kwa kuamini dawa husika inaniponya yaani dawa Kama dawa ambayo ni mti shamba tu waporini ?

b) au ilikua ilihitajika Imani ya roho mtakatifu kwa kuamuamini Yesu kupitia ndoto aliyooteshwa Babu na roho mtakatifu huku ukiichangia Imani yako kwa Tsh. 500 tu kwa kikombe ?

Sasa basi naomba nijumushe haya kwa hoja zifuatazo

1) Ikiwa huyo fulani ana Imani katika mazingira ya (a) hapo juu yani Imani ya dawa kama dawa akiamini mtishamba utamponya ...

Hivyo basi tufaham ya kwamba Imani ya aina hii haina mahusiano ya moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku kwa mfano labda naweza kusema imani hiyo haina mahusiano ya moja kwa moja na maadhimisho ya miaka 2 dhidi ya udhalimu wa wasiojulikana dhidi ya Lissu na wengine katika mtindo kama huo ...

2) Ikiwa huyo fulani ana imani katika mazingira ya (b) hapo juu yaani kuamini uponywaji wa moja kwa moja kutoka kwa roho mtakatifu kupitia Kikombe cha Babu tena huko Semunge Loliondo swekeni Kabisa huko haijalishi utafikaje huko as far as una jero lako mkononi Yesu anakuponya

Kwa maana hiyo basi hapo Imani ya huyo Fulani itakua na mahusiano ya moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku kama jinsi roho mtakatifu alivyo tufunulia kupitia maandiko (kwa maana ya kanisa) na sio kupitia Imani ya kikombe kwamba tuishi kwa amani na upendo na tutende haki kwa wote wala tusidhulimiane haki zetu na wala tusiwe na tamaa wala ubinafsi baya zaidi tusigeuze sheria kupitia mamlaka tulizo nazo kwa maslahi yetu binafsi badala ya maslahi ya wote ...

Bhebhe nkoi!! Usinielewe vibaya hapo juu nimejaribu tu kujiuliza mahusiano ya Imani ya huyo Fulani, je? ana Imani ya dawa kupitia kikombe cha Babu au ana Imani ya roho mtakatifu kupitia kikombe cha huyohuyo Babu na sio kupitia maandiko (kwa maana ya kanisa)? Kumbuka hata huyo Fulani mi simjui anfananaje ...

Anyways Mambo ya muhimu niliyo kua nataka kuya angazia ni haya yafuatayo

1) Ikiwa ilihitajika Imani ya dawa Kama dawa basi ilitakiwa kiutaratibu Kama zilivyo taratibu kwa dawa zingine ingetolewa elimu ya utendaji kazi wa dawa husika katika mwili wa binadamu kwa maelezo rahisi ya kikemia na kibailojia na kusajili dawa hiyo kwenye mamlaka husika kabla hao kinafulani hawajakwenda kunywa hicho kikombe

Tena hilo lilitakiwa kufanywa katika mtindo uleule ambao jopo la hao kinafulani haliwezi kuruhusu dawa nyingine zisambazwe kwa matumizi ya binadamu mpaka hapo watumishi wa jopo hilo (Mamlaka husika) la kinafulani watakapo jiridhisha kuwa dawa hizo ni salama kwa matumizi ya binadamu na zina maelezo ya kutosha ya kikemia na kibaiolojia na hata faida na madhara na tahadhari yake na pia ni mahsusi kwa ajili ya kutibu ugonjwa gani ...

Kwa staili hii tungeweza kuokoa maisha ya wengi ...

2) Lakini pia ikiwa ilihitajika Imani ya roho matakatifu hilo nalo lilihitaji wito wa kiimani kupitia kanisa au taasisi ya kiimani iliyosajiliwa katika mamlaka husika na wito huo ambao siku zote unakwenda sambamba na sadaka bila kujali kiwango cha sadaka nasio Imani ya sadaka ya kiwango maalum cha Tsh 500 tu kwa kikombe kama vile ni biashara

Kwa staili hii tungeweza kuwapata watu halisi waliostaili kunywa dawa ile na sio kwenda kuwanywesha watu dawa ambayo ukiwa huna Imani ya roho mtakatifu basi unakufilia mbali huo ni uuaji ...

Nadhani tunakumbuka tuluvyoshuhudia makundi mbalimbali ya watu kutoka kwenye jamii yenye Imani tofauti tofauti tuliwaona wahindu, waislamu na labda walikuwemo wapagani na waabudu mizimu pia kama ile dini ya kina Yericko Nyerere

Sasa hapa unategemea nini kama sio kuwaua makusudi watu wasio amini katika roho mtakatifu wa Kikombe cha Babu, au hata wale wasio amini katika roho mtakatifu wa maandio ya biblia ambapo Yesu mwenyewe nadhani hakutumia kikombe ili watu walio na Imani ya kweli waamini katika uponyaji.

Mwisho kabisa niseme Kikombe Cha Babu ni makusudi yenye kutiliwa shaka, na ambayo haipaswi kupewa nafasi kujirudia tena katika jamii yetu na iwe fundisho kwa kina Fulani wengine watakao kuja na Imani zao mbalimbali whether ni Imani kupitia vikombe au kupitia maandiko ya biblia lazima taratibu zifuatwe aidha ziwe taratibu za kiimani au za kikatiba ...

Kila Jambo linataratibu zake basi tujenge utamaduni wa kufuata taratibu pale majambo mengine yatakapo jitokeza ili kuepusha vifo visivyo vya lazima ...

2020 hiyo inakuja naona wengine tunaanza kulishwa matango pori ya choka mbaya ili kinafulani wengine waje wafaidi matikiti ya ukuu wa wilaya !!!
 
Forum statistics

Threads 1,390,264
Members 528,139
Posts 34,047,825
Top