Jebel
JF-Expert Member
- Jul 10, 2021
- 376
- 2,513
Wasalaam,
Je, umeshawahijiuliza njia rahisi ya kutoka kimaisha kutokana na kilimo? Basi leo nataka nikuletee jibu la swali lako.
Kama wewe ni kijana mwenye ndoto za kutoka kimaisha basi pata mtaji mtamu sana kutoka kwenye kilimo hiki cha mbegu za mchicha. Hiki ni kilimo chenye gharama nafuu sana, kwani hakihitaji dawa ya aina yoyote, palizi moja tu na soko la mazao yake ni la uhakika sana.
Kama ilikuwa hujui mbegu za ule mchicha wa kung’oa baada ya siku 18 tu zinatoka wapi, basi leo ni siri nakuletea.
A. NAMNA YA KULIMA ZAO HILI.
-Andaa shamba lako vema, udongo wa kichanga cheusi yaani wenye rutuba au tifutifu unafaa zaidi.
-Hakikisha shamba lako lina rutuba ya kutosha kama rutuba haitoshi basi ongeza mbolea ya samadi kisha baada ya week 4 au 5 ongeza mbolea ya UREA.
-Kwa ekari moja ya 70/70 mbegu 1Kg inatosha sana. Bei ya kilo moja ya mbegu ni Tsh 6000tu.
-Jitahidi sana upande kwa wakati mwafaka kulingana na msimu wa mvua wa eneo lako mfano mkoa wa Kagera wilaya za Muleba, Bukoba mjini na vijijini, Misenyi na Karagwe yote panda kuanzia tarehe 15/8 wilaya ya Biharamlo na Ngara pande September, Kigoma wilaya zote panda katikati ya September na October mwanzoni. Kwa kifupi msimu wa kupanda mahindi katika eneo lako nawe panda kipindi hicho hicho.
-Zingatia palizi kwa mda mwafaka sana
-MUHIMU zaidi jitahidi sana spacing kati ya mche na mche iwe ya kutosha, hivyo wakati wa palizi jitahidi sana iwepo pruning ya kutosha yaani haya majamaa haitakiwi yasogeleane sana kwa matokeo mazuri zaidi.
-Zao hili ni la mda mfupi sana miezi 3 tu unavuna, hivyo andaa tundubai kwa ajili ya kuvuna. Haya majamaa ni mepesi sana kuvuna kuliko ZAO lolote yaani ni ya kukata kwa kisu unaweka kwenye tundubai, unayapiga na kupata tule tu mbegu, peleka sokoni urudi na pesa.
B. SOKO LAKE.
Kuna uhakika wa soko kwani wakulima wa mchicha ni wengi sana, na wanahitaji mbegu hii lakini pia mbegu hii ina matumizi mengine zaidi ya kupanda.
C. CHANGAMOTO ZAKE
Kilimo chochote usidanganyike kina changamoto tu lakini kwa ZAO hili ukilinganisha na mazao mengine ni chache sana
-Spacing yake, yaani haya majamaa yakibanana sana utavuna kidogo sana ili yaweke matunda mazuri ni vema iwepo nafasi ya kutosha walau 3-6cm kati ya mche na mche. Kuya prune huwa ni changamoto sana
-Kama ardhi haina rutuba utavuna kidogo sana
D. GHARAMA ZA JUMLA KWA EKARI MOJA
- Kodi kwa ekari 50,000Tsh
-Kulima ekari 50,000Tsh
-Kupanda ekari 20,000Tsh
-Palizi na pruning 50,000Tsh
-Kuvuna na kupack 50,000Tsh
-Mbegu 4,000Tsh
-Extra costs 20,000Tsh
JUMLA 250,000Tsh.
E. MAVUNO KWA EKARI MOJA
-Kama shamba lina rutuba nzuri, mvua imeenda vema, umepanda vizuri kuna uhakika wa kuvuna kuanzia 500-800Kg kwa ekari moja
F. SOKO LAKE NA BEI
Kwa maeneo mengi 1Kg utaweza kuuza kwa Tsh 3500-4000. Soko lake ni uhakika sana kwani nchi nzima mchicha unalimwa na kuliwa.
NB. Mwaka huu nimelima ekari 10 tu nimeweka zaidi 13M NMB na gharama niliyotumia ni chini ya 3M. Na hii ni ndani ya miezi 3 tu.
Mwisho achana na kilimo cha mahindi na mpunga utakufa kwa presha.