Utajiri ni bahati ila kuwa na maisha Mazur sio

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
13,691
29,011
Mzuka wanajamvi!

Wabongo wengi tunatofautisha kuwaTajiri na kuwa na maisha Mazuri ama bora.

Wataalamu wa uchumi wanasema Tajiri ni yule ambaye ana utajiri ama hela kwa anzia dollars za kimarekani million moja au kulingana na kiasi hicho. Huyo ni tajiri kwasababu ana 'financial freedom'. Na utakuta wenye kiasi hicho ni wachache wanahesabika ndio maana kuwa Tajiri ni bahati.

Kuwa na maisha bora siyo bahati hapa ni juhudi tu weledi, kuweka akiba na kufanya kazi kwa bidii na nidhamu. Maisha bora ni kukidhi 'basic needs' makazi bora, mavazi malazi na msosi mzuri usiokupiga chenga. Kwa mbongo hapo eti wewe tajiri.

Ndo maana unakuta wengi wanaroga wanatoa kafara wanafanya mambo ya ajabu basi akiwa na kamilion kake hamsini yeye ni tajiri iyo ni dollars elfu ishirini tu.

Kwa iyo kina Diamond waheshimiwa hata akisingiziwa ni ngada wangapi wanafanya ngada hawamfikii. Kuna Alex Massawe ni jambazi wangapi ni majambazi siyo matajiri. Wengine flan malaya ndio maana tajiri wangapi malaya siyo matajiri.

Utajiri ni bahati lakini maisha mazuri I na bora siyo. Kila mtu anaweza kuwa na maisha mazuri na bora lakini siyo kila mtu anaweza kuwa tajiri. Kwa iyo tajiri yeyote aheshimiwe Haijalishi alipataje huo utajiri kwasababu ni bahati na siyo kitu rahisi.
 
Mzuqa sana!! Ni kweli maisha mazuri na utajiri ni viztu viwili tofauti...wapo matajiri lakini hawana maisha mazuri...wanaishi kama digidigi kwa kujificha na hawana amani.
 
True lakini bahati utengezwa pia.
Huwezi kuwa na bahati bila kijiconect au kuzivuta nguvu za bahati zije kwako. Wale positive minded ni mashuhuda
 
Back
Top Bottom