Umeshawahi kupata bahati ya kufanikiwa kwenye maisha ukaichezea?

Expensive life

JF-Expert Member
May 2, 2020
1,703
5,477
Ndugu zangu ama kweli bahati haiji mara mbili.

Huu ni ushuhuda nilionao dhidi ya rafiki yangu kipenzi, rafiki yangu huyu baada tu ya kumaliza masomo yake. Mungu si Athumani ni bahati iliyoje alipata kazi haraka sana huko bandarini kwenye moja ya kampuni kubwa sana ya mafuta.

Kaka yake ni moja ya viongozi wakubwa tu huko jeshini, hivyo ilikuwa ni rahisi yeye kupata kazi kutokana na convection aliyonayo kaka yake.

Rafiki yangu maisha yalimnyookea sana huko bandarini, baada ya muda mfupi tu nuru ilionekana alitakata vibaya mno na kitambi kikamtoka kutokana na mafedha.

Marafiki wakaongezeka kwa wingi sana, kazini alikuwa aendi tena kwa daladala, anapiga tu simu tex inakuja kumchukua jioni pia.

Mtaani wakampachika jina la tajiri kibonge, kwa maelezo yake kipindi kile alikuwa anaweza kuingiza si chini ya 300k mpaka 700k kwa siku kama mambo yakiwa mazuri hiyo ni kando ya mshahara.

mambo yakibadilika mwaka 2016 baada ya mwamba John Joseph pombe magufuli kuingia madarakani ( R.I.p)

Mirija yote ya upigaji ilipoea ghafla, akawa anakosa hata 10k kwa siku akawa anategemea mshahara pekee.

Mimi kama rafiki yake kwa kuwa alikuwa akinishirikisha mambo yake mara kwa mara nikuwa nikikumuasa, ndugu yangu nunua hata kiwanja ujenge unachezea sana pesa.

Kama mnavyojua cha mtu ni chake, kutokana na status aliyokuwa nayo mtaani, ilimuwia vigumu sana kuyaishi maisha ya mshahara tu.

Mambo yalizidi kuwa mabaya zaidi 2020 baada ya janga la corona, yeye ni mmoja ya wafanyakazi waliosimashwa kazi kipindi kile kutokana na janga lile.

Bahati alikuwa na akiba nzuri tu bank, hivyo akafungua duka la kuuza nafaka maisha yakaendelea, duka lilitembea lakini halikudumu sana likafa.

Family anayo amepanga kinondoni kodi ya nyumba mzigo, dahhh kutokana na msongo wa mawazo akajiingiza kwenye uvutaji wa bangi kupindukia.

Kutokana na uzoefu aliokuwa nao bandarini alitafuta kazi akapata tena ila sasa siyo nafasi ile aliyokuwa nayo hapo awali upigaji upo ila ile nafasi aliyokuwa nayo hapo awali maokoto yalikuwa yanajileta yenyewe.

Umeshawahi kupata bahati ya kutoboa maisha ukaichezea?
 
Ukipata mia usidharau buku ndo kwanza juhudi ongeza.

Siku zote ukiona umepata mchongo wew jiandae kustaafu nimemsifu kujiwekea security akiba.Hapo alicheza
 
Sio bahati hiyo mkuu ninkanuni ya kiungu na kiasili!

Kila mmoja wetu ata experience kufungukiwa na madirisha ya mibaraka maishani katika kipindi chale Cha maisha!

Ndio vile mhubiri anaandika kwamba "nyakati za dhiki zimewekwa Ili kutia akili kichwani""

Yaani neema huja Ili tujipange Kwa ajili ya dhiki zijazo!!

Kikwete alishika hatamu ili tile,tutengeneze ,tusome,tuwekeze!jpm akaja Ili kutia akili kichwani hadi leo Bado hatuja Kaa sawa!!

Kama upo katika kipindi fulani maishani kila unalofanya ni positive TU yaani faida TU,jua madirisha yamefunguka vilivyo!!

Nadhani!
 
Kiukweli nafasi ya kukunja 700k Kwa siku bado.

Ila nipo katika Maombi ili riziki yangu ifunguke zaidi nipate msaidia mdogo angu na Wazazi.

Bandarini kuna ulaji mzuri Sana.
 
Kiukweli nafasi ya kukunja 700k Kwa siku bado.

Ila nipo katika Maombi ili riziki yangu ifunguke zaidi nipate msaidia mdogo angu na Wazazi.

Bandarini kuna ulaji mzuri Sana.
Nikiwa chuo mzee wangu alikua anakunja 2M Kwa siku
Cha maana alichokifanya ni kujenga nyumba 1 ya biashara na kuongeza idadi ya wake.
 
Back
Top Bottom