mwehu ndama
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 543
- 1,874
Leo nimeona nishiriki nanyi katika darasa hili huru enyi vijana wa enzi hii ya bibi kizimkazi, Naam!!, nisikilizeni nyinyi nyote mnaoteswa na kusononeka juu ya maisha ya kifahari ya watu wengine.
Maisha yetu katika nyakati za sasa yamejawa na ushindani mkubwa tena wa hovyoo na usio na tija hasa kutokana na ukuaji wa teknolojia, watu wamebadilisha dhana zao za mafanikio ya kimaisha kwa kujilinganisha na mfumo wa maisha ya watu wengine, mfano kuangalia wanachokula, wanachovaa, wanachoendesha na wanapolala bila kujifanyia tathimini binafsi na kukubaliana na ukweli kwamba hata walipofika kwa sasa pia ni mafanikio tosha kulinganisha na walipotoka
Jinamizi hili la kuishi ndani ya ndoto za watu wengine linatesa sana, litakufanya upoteze hata kile kidogo ulichonacho kwa kukimbilia vikubwa ili uishi kama wao, na katika nyakati kadhaa utapata upofu na hutoziona fursa ndogo ndogo zilizokuzunguka ambazo pia zingekuvusha taratibu kwa haraka ya kuwa kama hao uwaonao tik tok, instagram na marafiki waliokuzunguka.
Binafsi nayatazama mafanikio ya kimaisha katika mlengo wa mtu kuwa na uwezo wa kujitegemea kimahitaji pasipo kuwa mzigo kwa mtu mwingine, na hapa mahitaji yako nilazima yaendane sawa sawa na kile kinachoingia mfukoni mwako wew.
Ni upumbavu mkubwa, tena ni uhayawani ulio tukuka kwa kijana ambae hujawah hata kujilipia kodi wala kujihudumia kimatibabu, chakula na mavazi kuanza kutamani utajiri na maisha ya kifahari huku ukiwa juu ya kochi la nyumbani kwa shemeji na remote mkononi.
Ewe kijana, Pambana kwanza uweze Kujitegemea, utajiri na ufahari sio wote tutakao vipata ingawa wote tuna nafasi sawa ya kuvipata, ila katika hilo heshimu sana msingi wa kipato chako cha sasa na kamwe usiwe mwepesi wa kuacha shughuli yako hiyo kwa kukimbilia utajiri wa haraka haraka sababu utakapoanguka, anguko hilo huwa baya sana na utatamani walau upate hata nusu ya unachokipata sasa.
Kujitegemea ni raha sana, ni hatua nzuri sana katika maisha kabla ya kuwaza utajiri hakikisha una maintain hiyo hali ya kujitegemea mpaka kifo chako bila kujali kiasi cha kipato chako, hakikisha unakuwa mashindani wa hatua zako mwenyewe na hakika utapiga hatua kubwa bila masononeko!
Vijana tupambanie kujitegemea na sio utajiri