Utajiri na Heshima

Utajiri na Heshima

Joined
Jan 13, 2018
Posts
38
Reaction score
60
Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo, Kmb 8:18

Watu wengi wanasema Mungu hatoi utajiri, huo ni Uongo. Mungu anatoa utajiri, tena watumishi wengi wa Mungu walikuwa ni matajiri.

Umesoma habari za Ibrahim jinsi alivyokuwa Tajiri wa Mali, Mwz 22:18.

Je, umasoma habari za Isaka na Yakobo jinsi walivyokuwa matajiri? Haukusoma habari ya Ayubu jinsi Mungu alivyomtajirisha?

Utajiri na heshima ziko kwangu, naam, utajiri udumuo, na haki pia,
Mithali 8:18.

Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake, 2Kor 8:9.

Kwanini watu wengi wa Mungu hawana utajiri;

Mosi, wengi wanadhani kuwa utajiri ni dhambi au mtu tajiri hana Imani, hayo ndio mafundisho potofu.

Pili, watu wengi wanaomba kupewa utajiri kwa ajili ya manufaa binafsi na sio Mungu kutukuzwa katika huo utajiri, Mungu anataka ukiwa Tajiri ushiriki katika kusaidia kusukuma mbele injili, kutunza watumishi wake na kuimarisha angano lake kwa sadaka.

Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu, Yk 4:3.

Mungu atusaidie tunapopewa utajiri tuweze kuutumia kwa mapenzi yake. Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.

Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo, 1 Timotheo 6:17-18.
 
biblia pia inawatambua masikini, kwenye moja ya maneno yake inasema tuwatendee sawa masikini na tajiri,,sio kwamba masikini akitangulia kuja kanisani hapati hata pa kukaa lakini tajiri hata akichelewa atatafutiwa kiti hata kwa mmoja wa wahudumu wa kanisa

pia kwenye biblia kuna neno linasema "itakuwa ngumu kwa tajiri kuiona pepo ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano" na hiyo yote ni kwasababu matajiri wengi hawaupati utajiri wao kwa halali na ndio maana waamini wengi ni masikini kwasababu njia nyingi za kuupata utajiri ni za kimagendo,pia matajiri wengi ni ngumu kuiyona pepo kwasababu ni ngumu sana kwenda sawasawa na biblia inavyosema kuwa wawe tayari kutoa mali zao pia washirikiane na wengine bila kwa moyo kama inavyosema 1TIMOTHEO 6:17-18.

hivyo basi unaweza ukaipata heshima hapa duniani lakini kwa Mungu usiwe na heshima maana kwake binadamu ni sawa, unahaki ya kuchagua upande
 
Biblia weka pembeni kwani imeandikwa na watu, tumia tu akili yako kwa makini utagundua hakuna utajiri wa Mungu!! Ni maujanja ujanja tu!!
 
Back
Top Bottom