Utajiri halali! Dhana isiyo na chembe ya ukweli

Utajiri halali! Dhana isiyo na chembe ya ukweli

Wewe si ndio ulikubali hakuna utajiri halali? Au hujui utajiri ni riziki ?
Sio kweli pacha, riziki na utajiri ni vitu viwili tofauti unaweza kuwa unapata riziki yako na usiwe tajiri
 
Maneno ya Mungu yanasema hivi.... Ni rahisi kwa ngamia(sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa Mungu....!
Warithi wa ufalme wa Mungu ni akina nani? Wana sifa na vigezo gani? Ni wanyofu na wasafi wa moyo, watenda haki waliojitenga na dhambi na matendo yote ya giza, wasiodhulumu wala kupora cha mhitaji...
Ili uweze kuwa tajiri ama ili uweze kuupata utajiri kwa kiasi kikubwa itabidi ujitenge na matendo ya unyofu, huruma, utu wema na ushikamane na ulimwengu wa giza, makafara dhuluma na ni lazima uwe na roho ngumu na katili japo kwa kificho....!
Itabidi utafute njia za kupata bidhaa kwa bei rahisi sana halafu uuze kwa faida kubwa
Itabidi uwe mkwepa kodi na mdanganyifu kwenye mapato kwa nia ya kutunisha kibubu chako
Itabidi ununue hata kuuza mali ya wizi, dhuluma ama magendo ili tu usitetereke kiuchumi
Itabidi waajiriwa wako uwalipe kidogo lakini wazalishe kingi
Itabidi ufanye makafara na ushirikina kwa nia ya kulinda utajiri na himaya yako
Itabidi utumie mbinu zote halali na haramu ili kuendelea kukuza na kutunisha akaunti zako na biashara zako..

Ukishafanikiwa kimaisha na kuwa mfanyabiashara tajiri kwa viwango tofauti, kiunafiki kabisa na kuficha makucha yako, utairudia jamii kwa kutoa sadaka, misaada na zaka kwenye nyumba za ibada na majukwaa ya kijamii.. Hutafanya kwa siri kwakuwa unataka usafishike mbele za macho ya jamiii... Lakini kile unachokoa ni sehemu ndogo kabisa kwenye kile ulichowaibia wale unaowapa kwa mlango wa misaada....

Yote juu ya yote tunauhitaji utajiri kwa nguvu zetu zote ili kukidhi mahitaji ya natamanio ya kimwili na starehe za dunia, sifa na utukufu wa kununua.... Lakini asikudanganye mtu hakuna utajiri wa haki hata siku moja

Mkuu hapo unaposema kwny hii verse Ngamia (sio mnyama) unamaanisha nini mkuu?

Luke 18:25
Indeed, it is easier for a camel to go through the eye of a needle than for someone who is rich to enter the kingdom of God.”

Mbona kwny english bible imetumia neno (CAMEL),hapo walimaanisha nini?
 
Wengine hawaamini uwepo wa Mungu sasa ukileta habari za Mungu kwenye discussion kama Kwa watu wengine ni irrelevant
Aisee, lakini ukiwaambia wametokana na asili ya nini au wameumbika vipo ikiwa hawawezi hata kujiumba wenyewe au hata kuumba siafu wanachemka kukufafanulia?

shetani anafanya kazi kweli kweli kupitia wakala wake
 
Mkuu nakubaliana na wewe asilimia zote. Jaribu alilopitia Yesu la kuonyeshwa milki ya dunia na kuambiwa kusudu inampata kila mwanadamu kwa viwango tofauti. Kuna watu wanajikinga miili yao, kuna watu wanakinga mali zao, kuna watu wanadhulumu,kuna watu wanaiba, kuna watu wanahonga kupata vyeo,kuna watu wanapata upendeleo wa kujuana. Yaani full ushetani.
Luka 4:5-8 "Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.6Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.7Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.8Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake
Kama shetani anamwambia Yesu kuwa utajiri na Enzi yote na fahari yake ipo mikononi mwake naye humpa yeyote kama apendavyo.wewe ni nani uupate utajiri bila kupewa na shetani na atakupa bure?
 
Sio kweli pacha, riziki na utajiri ni vitu viwili tofauti unaweza kuwa unapata riziki yako na usiwe tajiri
Riziki ndio inaleta utajiri, ni kiwango tu cha riziki ndio tofauti ya masikini na tajiri.
 
Aisee, lakini ukiwaambia wametokana na asili ya nini au wameumbika vipo ikiwa hawawezi hata kujiumba wenyewe au hata kuumba siafu wanachemka kukufafanulia?

shetani anafanya kazi kweli kweli kupitia wakala wake
Huu mjadala mrefu tuuache. Ila elewa Tu wapo wasioamini vitabu
 
Kama mtu haamini uwepo wa Mungu mada haimhusu kwa kuwa mtoa mada ameiweka mada yake kwa misingi ya Mungu tena ameanza kabisa 'Neno la Mungu linasema' sasa hapo maana yake kwa mtu asiyeamini hii discussion kwake ni irrelevant
Wengine hawaamini uwepo wa Mungu sasa ukileta habari za Mungu kwenye discussion kama Kwa watu wengine ni irrelevant
 
Zipo njia nyingi tena halali za kuleta utajiri hebu muache huru mkulima wa korosho akauze mwenyewe anapotaka na bei apange mwenyewe kama hakuwa tajiri, halafu KODI ambayo haimnufaishi mtoa kodi kwa nafuu ya chochote ni WIZI.
yaani ulime mwenyewe upange bei mwenyeee pia.sasa unamuuzia nani.labda mapera ndio unaweza kufanya hivyo lkn sio mazao ya biashara.
 
Riziki ndio inaleta utajiri, ni kiwango tu cha riziki ndio tofauti ya masikini na tajiri.
Lakini zote ni riziki. Ila ipo riziki ya matajiri na maskini, kwa hiyo kuwa na riziki si lazima uwe tajiri ila tajiri maana yake ana riziki
 
Lakini zote ni riziki. Ila ipo riziki ya matajiri na maskini, kwa hiyo kuwa na riziki si lazima uwe tajiri ila tajiri maana yake ana riziki
Nafurahi ulikiri kuwa zipo riziki halali. Kuwa tajiri haibadilishi unalali wa riziki. Wewe unapopatia riziki yako unapewa kiasi fulani,mwingine anapewa mara elfu hio haifanyi riziki yake kuwa sio halali.
 
Wewe si ndio ulikubali hakuna utajiri halali? Au hujui utajiri ni riziki ?
kuna tofauti ya riziki na utajiri.ebu kuweni waelewa kidogo Ndugu zangu. riziki ya halali ipo ila utajiri Wa halali hakuna.nasema hivyo Kwa msisitizo mkubwa kabisa .naomba Kwa yeyote aliyejaribu kuutafuta utajiri aseme kama hajawahi kufanya jambo lolote ambalo ni chukizo Kwa Mwenyezi Mungu. hata kama huo utajiri ukuupata lkn utakuta ulijaribu kukwepa kodi.kama ni kazini wengine wanatengeneza ata mazingira ya rushwa ili wapande cheo. au biashara unajua fika mwenzanko pia anaitaka Ili wanae waende Choo lkn kwakua unatamani kupata pesa nyingi unaichukua yote na kumwacha mwenzako hajapata chochote.
 
Duh Kiswahili kigumu. Riziki maana yake nini? Kiwango cha upataji riziki ndio tofauti ya masikini na tajiri. Kama unaamini hamna utajiri wa halali Sawa,hio ni Imani yako. Huwezi kunilazimisha niwe na Imani kama yako.
 
Aisee, lakini ukiwaambia wametokana na asili ya nini au wameumbika vipo ikiwa hawawezi hata kujiumba wenyewe au hata kuumba siafu wanachemka kukufafanulia?

shetani anafanya kazi kweli kweli kupitia wakala wake
We jamaa unahamishia hapa kila ulichokaririshwa na unatamani kila mmoja aamini hivyo, jamaa kakujibu vema kuwa hapendi kuingilia imani za watu so tafazali jikite kwenye somo la leo.... ukikua utafikia kuzaa ndo utajua una uwezo wa kuumba au laah..!!
 
Duh Kiswahili kigumu. Riziki maana yake nini? Kiwango cha upataji riziki ndio tofauti ya masikini na tajiri. Kama unaamini hamna utajiri wa halali Sawa,hio ni Imani yako. Huwezi kunilazimisha niwe na Imani kama yako.
unapwaya sana Ndugu. hapa hakuna mtu anaemlazimisha mwingine kukubaliana na mawazo yake.na ndio sbb ukawa mjadala uliowazi .
 
Nafurahi ulikiri kuwa zipo riziki halali. Kuwa tajiri haibadilishi unalali wa riziki. Wewe unapopatia riziki yako unapewa kiasi fulani,mwingine anapewa mara elfu hio haifanyi riziki yake kuwa sio halali.
Unapewa riziki na nani
 
We jamaa unahamishia hapa kila ulichokaririshwa na unatamani kila mmoja aamini hivyo, jamaa kakujibu vema kuwa hapendi kuingilia imani za watu so tafazali jikite kwenye somo la leo.... ukikua utafikia kuzaa ndo utajua una uwezo wa kuumba au laah..!!
Ukimya nao ni jibu
 
Hiyo ya ngamia alimaanisha ngamia mnyama.
"for it is easier for a CAMEL to go through the eye of a needle.
Camel=ngamia mnyama na sio ngamia kamba kama baadhi wadhanivyo.
 
Back
Top Bottom