ThugMaster
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 1,601
- 2,275
Huwa najiuliza sana utajiri ulio safi ni upi..?
Aisee mbona mi ni tajiri saaaana tena kuliko hata hao unaowajua wewe lakini katika utajiri wangu namba 1 ni Yesu maana ndiye anayenipigania katika kila hali na hatua yoyote ile ya maisha.Kwenye huu uzi ndio utajua kwamba Wana jf wengi si matajiri kama wanavyojitapaga humu!
. Maana sioni hata mmoja anaekuja kuelezea utajirj wake kama ni wa halali au la!
Fanya haraka huko tayari ndugu zake na Mengi washakuja kukutaka uwathibitishie ikiwa ni Freemason kabisa kabisa.Tuaminishe kwa ushahidi kuhusu mengi
Hoja bomba sana MrNdo mana mimi nafaiti faiti niwe na vitu vikuu vitatu tuuuuuuuuuuuuuuuu.
Mke mzuri(na watoto)
Nyumba ya kukaa
Usafiri
Kibiashara cha kuingiza pesa ya kula na kubakia katika levo ambayo sitokaa kuhangaika kula ya siku au wiki au mwezi.
Full stop,hayo mengine sijui uwe na gari kumi,mara hivi na vile mimi siwezi aiseeee
Katika kumaintain status huko ndio unajikuta umeingia kwenye njia tofauti sasaNdio, ila kwa dunia ya sahivi ukiwa tajiri hlf watu wanajua, ku-maintain status ni muhimu, la sivyo ukifilisika unachekwa, unakimbiwa, unadhihakiwa, na kutengwa Khantwe
+1Mimi naamini unaweza kutajirika bila dhuluma lakini wapita njia kama mtoa mada hawataacha kusema ' utajiri wake Una Siri nyingi'
Maneno ya Mungu yanasema hivi.... Ni rahisi kwa ngamia(sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa Mungu....!
Warithi wa ufalme wa Mungu ni akina nani? Wana sifa na vigezo gani? Ni wanyofu na wasafi wa moyo, watenda haki waliojitenga na dhambi na matendo yote ya giza, wasiodhulumu wala kupora cha mhitaji...
Ili uweze kuwa tajiri ama ili uweze kuupata utajiri kwa kiasi kikubwa itabidi ujitenge na matendo ya unyofu, huruma, utu wema na ushikamane na ulimwengu wa giza, makafara dhuluma na ni lazima uwe na roho ngumu na katili japo kwa kificho....!
Itabidi utafute njia za kupata bidhaa kwa bei rahisi sana halafu uuze kwa faida kubwa
Itabidi uwe mkwepa kodi na mdanganyifu kwenye mapato kwa nia ya kutunisha kibubu chako
Itabidi ununue hata kuuza mali ya wizi, dhuluma ama magendo ili tu usitetereke kiuchumi
Itabidi waajiriwa wako uwalipe kidogo lakini wazalishe kingi
Itabidi ufanye makafara na ushirikina kwa nia ya kulinda utajiri na himaya yako
Itabidi utumie mbinu zote halali na haramu ili kuendelea kukuza na kutunisha akaunti zako na biashara zako..
Ukishafanikiwa kimaisha na kuwa mfanyabiashara tajiri kwa viwango tofauti, kiunafiki kabisa na kuficha makucha yako, utairudia jamii kwa kutoa sadaka, misaada na zaka kwenye nyumba za ibada na majukwaa ya kijamii.. Hutafanya kwa siri kwakuwa unataka usafishike mbele za macho ya jamiii... Lakini kile unachokoa ni sehemu ndogo kabisa kwenye kile ulichowaibia wale unaowapa kwa mlango wa misaada....
Yote juu ya yote tunauhitaji utajiri kwa nguvu zetu zote ili kukidhi mahitaji ya natamanio ya kimwili na starehe za dunia, sifa na utukufu wa kununua.... Lakini asikudanganye mtu hakuna utajiri wa haki hata siku moja
Umewaza kimo cha mbilikimo tena huko ndio kuna umafia kuliko unavyodhani... Wao ndio huamua soko liweje kwahiyo wanaweza kuamua kuzalisha kidogo au kingi kulingana na mahitaji ya nyakati... Lakini pia fuatilia vema laana ya mafuta utajua mengiNafikiri hoja yako hii umeitazamia kupitia tundu la ufunguo, utakapofungua mlango utawaona jamaa waliojaliwa utajiri kupitia visima vya mafuta uwani mwao, hawa hawana mganga wa kienyeji wala kumdhulum mtu, wala freemanson,wanachota mali toka ardhini
Wa kabla ya Kanuni mpaya lakiniWastaafu wangeishi hivyo wangeshukuru.
uko sahihi mkuu... hakuna utajiri bila uhalifu!!Nyuma ya kila mafanikio ya utajiri kuna uhalifu.
Mkuu kuna watu hawajakuelewa vizuri mbona wamejikita kwenye ushirikina na FreemasonUmewaza kimo cha mbilikimo tena huko ndio kuna umafia kuliko unavyodhani... Wao ndio huamua soko liweje kwahiyo wanaweza kuamua kuzalisha kidogo au kingi kulingana na mahitaji ya nyakati... Lakini pia fuatilia vema laana ya mafuta utajua mengi
Umewaza kimo cha mbilikimo tena huko ndio kuna umafia kuliko unavyodhani... Wao ndio huamua soko liweje kwahiyo wanaweza kuamua kuzalisha kidogo au kingi kulingana na mahitaji ya nyakati... Lakini pia fuatilia vema laana ya mafuta utajua mengi
Wote tukiwaza hivi tutakua na taifa lamzezeta kwasababu ukipata tatizo tu umejikalia nahakuna wakukusaidiaNdo mana mimi nafaiti faiti niwe na vitu vikuu vitatu tuuuuuuuuuuuuuuuu.
Mke mzuri(na watoto)
Nyumba ya kukaa
Usafiri
Kibiashara cha kuingiza pesa ya kula na kubakia katika levo ambayo sitokaa kuhangaika kula ya siku au wiki au mwezi.
Full stop,hayo mengine sijui uwe na gari kumi,mara hivi na vile mimi siwezi aiseeee
jibu ni kwamba hakuna njia halali ya utajiri.alafu mleta mada ameelezea Kwa kirefu lkn watu wamebezi upande mmoja tu Wa ushirikina .wamesahau kuna kudhulumu .kukwepa kodi. wizi.kuuwa kishirikina au kuwauwa wale wote unaoona ni kikwazo kwako katika kufanikisha biashara fulani ambayo itakupa pesa nyingi nao wanaonekana ni kikwazo.Kwani hamna njia halali au scientific za kulinda utajiri wako?