Utaikumbuka CCM kwa lipi baada ya 2015?

Utaikumbuka CCM kwa lipi baada ya 2015?

Viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani, watumishi wa mungu na watu wenye misimamo tofauti na ccm kutekwa, kuteswa, kupigwa mabomu, risasi za moto, mapanga na hata wengine kuuawa tena mbele ya polisi lakini hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa kwa sababu tu si waumini wa chama cha mapinduzi. Rejea tukio la mwangosi, mapadri zanzibar, mabomu olasite na soweto, pia matukio mengine mengi katika chaguzi ndogo ndogo.
 
Ni dhahiri harakati zinazofanya na vyama vya siasa vya upinzani kwa ujumla wake zinatishia uhai wa ccm pamoja na ccm kutumia mbinu za kihafidhina na kuwatumia makukulimbwe kama Mwigulu bado uhai wake ccm umeteteleka.

Kiti kiko wazi wa upinzani.unadhani utaikumbuka ccm kwa lipi liwe jema ama baya.

Mimi kama mimi nitaikumbuka ccm kwa kuweza kuwadanganya wananchi bila woga.

""Where we dare to talk openly""

nitaikumbuka kwa kuvuruga mchakato wa katiba ya nchi yetu . kuweka misingi ya watawala kutawala nchi milele na walalahoi kutawaliwa milele. hiki ndio kitu kibaya katika tanzania.mengine yote yanaangukia ktk hili la kuandaa mchakato wa katiba mbaya
 
Augustine,
Nimesema unapenda kuongeza chunvi panapokupendeza na nitakwambia kwa nini na mifano yake! Unafananisha uzuri wa mke wangu kwa mke wako... wapi na wapi?...kinachotupendeza TZ sii lazima kiwe sawa na Kenya...chongo kwao sii kilema. Nipe mazuri ya baba Mkapa kulinganisha na baba JK! na sio nyumba ya pili Kenya.
Quote yako ya kwanza:-
Kupata uhuru sawa sii hoja kwani kuna watu wamezaliwa siku moja saa moja na dakika moja bado mmoja akawa amezaliwa ktk mazingira bora kuliko mwenzake! Hii ndio hali tuliyokuwa nayo Tanzania, ikiwa utapima basi pima walioyafanya Kenya baada ya Uhuru. Kenya kila kitu wamekikuta kama vile mtoto wa Freeman, Kingunge bila kumsahau Mkapa huwezi kulinganisha mafanikio yao na ya mwanao kama utaweka fadhila na urahisi waliopata toka kwa wazazi wao.

Ya pili, infastructure yao ilikwisha jengwa na mkoloni, wenzetu waliendeleza system ya kodi iliyowekwa na Mkoloni (kodi za kichwa n.k) wakati Tanzania tuliondoa kabisa minyororo hiyo na kutumia UJAMAA kama njia bora ya kukuza maisha ya wananchi. Kenya kila raia wake ana kitambulisho ambacho kinatumika kama social security number kinaitwa - KIPANDE, hii imewasaidi sana hali Mkapa na elimu yake kashindwa kuanzisha kitu hicho zaidi ya kugawa mirathi yetu. Kumbuka pia ukusanyaji wa kodi hauhesabiki kwa total amount ulizokusanya ila ufanisi ktk ukusanyaji wa hizo kodi. Mathlan kuna watu millioni mbili wanaotakiwa kulipa kodi, TZ ikakusanya billioni nne toka kwa wananchi milioni moja na nusu hali Kenya ikaweza kukusanya mara tatu ya kiwango cha TZ lakini toka watu millioni tu. Wao watakuwa na uzembe pamoja na kuwa wamekusanya nyingi zaidi yetu!
Hii yote inategemea walipaji, asilimia pamoja na wingi wa kodi hizo. Kuna kodi ambazo zipo Kenya hatuna TZ na nyingine tunazo sisi Kenya hawana! - nadhani upimaji mzuri wa kodi ni ule unaowahusu viongozi wa nchi moja say..Mkapa na JK katika kipindi cha budget ya rais huyo! Pia kumbuka kukusanya kodi kubwa sio mafanikio ikiwa kodi hizo ni mzigo kwa wananchi, hii sio maendeleo wala sifa wakati mwingi ktk uchumi unafuu wakodi huzidisha uwekeshaji na kuwahamasisha wananchi wazalishaji kufanya kazi na kuzalisha zaidi. Kwa hiyo kila sera ina matokeo tofauti kiuchumi.
Quote ya Tatu,
Ikiwa kweli ukusanyaji mzuri wa kodi ndio umewasomesha Wa Kenya imekuwaje Mkapa kashindwa kusomesha Watanzania hali umedai kwamba ukusanyaji wake ni mzuri?... tazama mada ya elimu!
Quote ya nne,
Tapeli msomi huzifanyia kazi?... mbona wezi wote ktk serikali ya Mkapa ni hao wasomi na billioni zao hazionekani. Akina Sumaye na Mkapa mwenyewe hizo fedha wanalipa kodi gani wakti fedha zao ziko benki ya Uswiss? Tapeli asiyekuwa msomi hana access ya benki hizo kwanza hajui kama zipo. Hawezi kuiba kodi isipokuwa msomi wa TRA ambaye anaweza kucheza na figures ndani ya PC... wameyafanya haya na bado wanayafanya wengine wanakimbilia nchi za nje baada ya kulipua. Tapeli asiyekuwa msomi ofisi yake ni Kongo street! Akikamatwa kwa tuhuma tu hana bond, maisha yake jela bila hukumu hali msomi ataweka wakili na kutoka nje hata kama ushahidi unamfunga...kesi yake itachukua miaka na mwisho wake kufa, ndio ya akina Mkapa hayo utumiaji nguvu kuondoa report ya Warioba na kuita wananchi wavivu na wajinga!..ATC,TTCL, NBC yote yamefanywa na wasomi na itachukuwa miaka kumi ijayo kuweza kukusanya hata robo ya fedha tulizopoteza.
Quote ya nne,
tupe hesabu ya kutosha kuhusu mafanikio ya Mkapa... For the first time TZ tumeweza kuwa na watoto wanaoitwa CHOKORAAA!.. majambazi ni dalili kubwa ya watu kutokuwa na mbinu za kimaisha kwani elimu hawana ktk ulimwengu wa biashara. Darwin's nightmare na hao World vision ni dalili kubwa ya umasikini wa ELIMU. Elimu sii wingi wa kukaa darasani ila uwezo wa kuanzisha na kuendesha miradi ya uzalishaji.
Quote ya tano,
Ubora wa elimu tazama tena mada yako ktk ELIMU...jibu unalo mwenyewe.
Quote ya sita,
Bado unalinganisha wingi wa machungwa na ndimu ndani makapu mawili!...Kenya wakikusanya mara kumi yetu bado haina maana wanafanya vizuri ikiwa hatufahamu ni kiasi gani kinatakiwa kukusanywa kwao pia kama kodi hizo zinaongezauzalishaji nchini mwao ama zinaathiri!..Kupanda kwa kodi 30% unakokuzungumzia Je, unaweza kutupa umezipata wapi?..I mean toka Jan to March 2006.

Ulimboka; kibanda etc
 
Ulimboka alivyong'olewa kucha na meno bila ganzi na Kibanda alivyonyofolewa jicho na kukatwa kidole bila ganzi.
 
Naikumbuka na nitaendelea kuikumbuka kwa uongozi bora.ccm oyeeeeeee.
 
Nitakumbuka CCM kwa kuwa Chama cha Siasa Kikongwe kilichokufa mwaka 1999 na kuzikwa na yaliyokuwa mawazo ya mwenyekiti wa chama!

Nitakumbuka CCM kwa kuwa taasisi iliyodumaza akili za wanazuoni wengi of whom baada ya kumaliza tafiti zao walikuja kukalia tasnifu zao ama kuzihifadhi ndani na kwenda kulundikana CCM.

Nitaikumbuka CCM kama uchochoro wa kuinukia kimaisha kwa kupeana fadhila huku watawala wakiwadharau wananchi kwa kuwagawia kanga na vipande vya sabuni kama vile wanahisi ni wachafu na ama hawana namna nyingine ya kujisetiri.

Nitaikumbuka CCM kama Chama cha wanafamilia na marafiki wa Familia ambao wanatumia mwavuli wa chama kujineemesha wao,familia zao na marafiki huku wanachama wasiojitambua wakiendelea kupasuka magaga tu wakihubiri ujamaa pasi kujua ujamaa ulikwishapotea miaka 40 kama si hamsini iliyopita.

Nitamkumbuka Jakaya Kikwete kwa kuwa mwenyekiti wa chama ambaye anaendesha nchi kama anayeendesha mikutano ya halmashauri kuu ya chama chake na pia kuteka aliloliita Bunge maalum la katiba kwa kuandaa katiba ya chama cha mapinduzi badala ya katiba ya Wananchi.
 
mkuu ccm haikumbukiki ! Mambo yaliyofanywa na chama hiki yanamshangaza hata shetani !
 
Uhuru wa kuongea sasa hivi kila mtu anaongea bila hofu tofauti na tawala zilizopita watu walizibwa midomo
 
Kumnunua Shivji wakati taifa linapohitaji zaidi mchango "sober" wa intellectuals..
 
tutaikumbuka kwa ufisadi,rushwa,ujangili,na biashara ya unga!
 
Mtaikumbukaje wakati itatawala miaka 200 mbele??
 
Back
Top Bottom