Utafiti: Watanzania tunaweza kutawaliwa na Wakenya kwa miaka ijayo usalama wa Taifa upo hatarini

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Juzi nilifika Mkoani Mara hasa wilaya ya Tarime maeneo ya vijijini karibu na mpakani mwa Tanzania na Kenya

Nilifika vijiji vya Gwitiryo,Pemba,Borega na kwingineko na nilicho baini katika vijiji hivi,mambo yanayofanyika hapa ni hatari kwa usalama wa Taifa kwa sasa na baadae

Jamii ya wakurya wanaokaa hapa wameanzisha utamaduni wa kuoa wanawake kutoka nchini Kenya ambao tayari wana watoto zaidi ya watatu na kuendelea

Yaani wanaume wa vijiji vya mpakani wanaenda Kenya wanachukua wanawake waliokwisha zaa huko Kenya na watoto wao na kuwahamishia upande wa Tanzania na hao watoto huhesabiwa kama watoto wa Mwita Chacha wa Tanzania na hupewa majina ya ukoo kwa upande wa Tanzania, watoto hawa wengine huwa wana umri mkubwa

Mmoja wa mwanakijiji niliyekutana katika kijiji cha Nyabitocho alinisimulia kuwa watoto walio olewa pamoja na mama zao ni wengi tu,na isitoshe tunawafahamu na wengine ni wajumbe wa serikali ya kijiji na wengine ni viongozi kwenye vyama vya siasa wanawafahamu lakini wananyamaza tu na ukifuatilia hawana vibali vya kuishi Tanzania

Mwingine aliniambia kipindi anasoma chuo kikuu Dodoma wamesoma na kijana ambaye waliolewa na mama yake huku Tanzania lakini baadae akili ilipo pevuka akarudi Kisii Kenya kwa ndugu zake hata hivyo kupitia elimu ya Tanzania alisoma hadi chuo kikuu na mkopo akapata ila cha ajabu likizo alikuwa anaenda kisii Kenya na alipinga yeye kuolewa na mama yake ila anashukuru kupata mwanya wa kusoma Tanzania hadi chuo kikuu kupitia mama yake

Nikataka kujua kama kuna watanzania wanaolewa Kenya na watoto wao,walisema upande wa Kenya hakuna kitu kama hicho,Kenya wanasheria kali kuhusu wahamiaji ,hakuna mtanzania anaweza kujiita mkenya ila wakenya wengi wanajiita Watanzania

Nimebaini kuwa kwa miaka kadhaa ijayo usalama wa Taifa la Tanzania utakuwa hatarini,je hao wanawake wanao olewa kutoka Kenya na watoto wao wakija Tanzania wanasoma na kuanza kutambulika kama Watanzania Idara ya uhamiaji inalijua hilo? Na wamechukua hatua gani? Viongozi wa vijiji wapo tu hawachukui hatua

Hizi familia zinazo olewa kutoka Kenya ni hatari kwa usalama wa Taifa ,kuna siku usalama wa Taifa tutawakabidhi wakenya nionavyo miaka ijayo

Wakurya acheni kuoa wanawake wa Kenya na familia zao,mnahatarisha usalama wa Taifa
 
Hayo mambo mbona yapo sana tena miaka mingi tu kwa jamii za mipakani kuingiliana mfano kuna ndugu wawili waliwai kushika nyadhifa kubwa ndani ya Serikali ya Uganda na Kenya katika vipindi tofauti

Suala la uzalendo ni pana sana ndio maana kuna wabongo wanaipenda USA kuliko nchi yao
 
Kwenye mambo ya kitaifa hasa usala wa Taifa tuweke vyama pembeni
Mipakani Ni kitu Cha kawaida Sana mipakani.Ujue mipaka ilikatwa vibaya Masai wa familia moja Kijiji chake kinakatwa na wakoloni vipande viwili mmoja akawa Masai wa Kenya kajiado mei

Mwingine Tanzania loliondo!!!!!! Watu wa familia moja

Mfano kulitokea kituko Kati ya mpaka wa Kenya na Uganda .Raisi Moi wa Kenya walizaliwa na mdogo wake mama mmoja Moi akiwa Raisi Kenya mdogo wake akawa waziri Uganda!!!
Mipakani Wana ndugu kila upande na hujuana vizuri tu.

Jaluo wa Tanzania na wa kenya Ni walewale,mkurya wa Tanzania na Kenya walewale nk
 
Hao jamaaa wana moyo kweli,yani unaoa mtu mwenye watoto na unamtoa mbali hivyo.
 
Nilijua tu siasa lazima ziingizwe hapa,zisingeingizwa ningejitoa jf...haya uzi ushaharibika tayari.
 
Wakurya endeleeni kufanya hivo, nchi ikiwa na machanganyiko wa watu vizur, labda siku moja bongo tutaacha uwoga na kuwa wajasiri kwa kila maswala ya kijamii,
 
Tanzania chini ya utawala wa Ccm ni kama tu shamba la bibi! hivyo lolote linawezekana.
 
Wengine watoto wetu wamepata nafasi Emperial Collage, Oxford na Cambridge kwasababu tuliolewa na wazungu.
 
Back
Top Bottom