Utafiti wangu: Wanaume hawapendi kuoa wanawake wazuri sana...

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,093
Utafiti nilioufanya kwa kutumia vigezo vyangu mwenyewe visivyofanana na vya Synovet wala ESRF unaonyesha kwamba wanaume hawapendi kuoa wanawake wazuri sana.

Sababu kubwa kabisa ni kuogopa pressure zitakazoletwa na hisia za mkewe kutakwa na wanaume wengi hivyo kutokuwa na uhakika wa mwanamke huyo kuwa wake peke yake.

Naruhusu findings za wengine juu ya hili karibuni.....................
 
Wazuri wa nini?
Ntakupa ka mfano fulani hivi ka ukweli bila kujibu swali lako direct,

Mwanamke anapopita wanaume huanza kumwangalia usoni, kisha hushuka kifuani na anapompita humwangalia chini ya kiuno na kisha miguuni............. hizo ndizo sehemu ambazo wanaume huwaangalia wanawake na ndipo ninapopaongelea mimi
 
Uzuri wa nini?

1. Sura
2. Tabia
3. Mavazi
4. ...

Utafiti wako bado haujakamilika ningekuwa lecturer wako ningekupa sup...kiddin

Kaka ndio maana nikasema nimeufanya kwa kutumia vigezo vyangu mwenyewe sio kama vile vya Synovet wala ESRF wala Daima
 
Kwa kweli mwanamke ambaye akipita njiani kila Dick and Tom anamuangalia kwa macho ya matamanio ni pressuer tupu kumuoa,
 
Utafiti nilioufanya kwa kutumia vigezo vyangu mwenyewe visivyofanana na vya Synovet wala ESRF unaonyesha kwamba wanaume hawapendi kuoa wanawake wazuri sana.

Sababu kubwa kabisa ni kuogopa pressure zitakazoletwa na hisia za mkewe kutakwa na wanaume wengi hivyo kutokuwa na uhakika wa mwanamke huyo kuwa wake peke yake.

Naruhusu findings za wengine juu ya hili karibuni.....................
Natofautiana nawewe kabisa, mimi naamini kwamba wanaume wanapenda kuoa wanawake wazuri ndiyo maana wapo tayari kuishi nao. Hivi inaingia akilini kwamba mtu hataki kitu kizuri? labda ungefafanua unaposema UZURI unamaanisha nini. kwasababu to me my wife ndo mwanamke mzuri kuliko wote.
 
haya bwana mie ni exception to ur conclusion
mie bwana ntaka mwanamke beautiful awe wife maana hii hadithi ya kupitiwa mbavuni ata hao wakawaida wanapitiwa sasa tabu ipo wapi.
huyo mzuri atanipa raha provided nampenda na anipenda
so for me nataka a very beautiful wife.
 
Ntakupa ka mfano fulani hivi ka ukweli bila kujibu swali lako direct,

Mwanamke anapopita wanaume huanza kumwangalia usoni, kisha hushuka kifuani na anapompita humwangalia chini ya kiuno na kisha miguuni............. hizo ndizo sehemu ambazo wanaume huwaangalia wanawake na ndipo ninapopaongelea mimi

Hao Huitwa SHOW STOPPER, kama kuna watu wanazungumza wanaumauma maneno wengine wananyamaza, wenyewe wajua pia huongeza mapoz! na kujimwaga kama tausi!!!!!!
 
Ntakupa ka mfano fulani hivi ka ukweli bila kujibu swali lako direct,

Mwanamke anapopita wanaume huanza kumwangalia usoni, kisha hushuka kifuani na anapompita humwangalia chini ya kiuno na kisha miguuni............. hizo ndizo sehemu ambazo wanaume huwaangalia wanawake na ndipo ninapopaongelea mimi

kwahiyo unamaanisha uzuri wa sura, nyonyo, wowowo na miguu au?
 
Kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake hata kama ni pumba.
Mtoa mada unaonekana uwezo wako wa kujieleza ni mdogo mmmmno!

Kwa mwanaume mwenye kujua uthamani wa mwenza kuna vitu vingi vinavyochunguzwa kwa mwanamke kabla hujamuoa. Suala la uzuri unaouongelea sijui ni uzuri upi huo. Wanadamu tonatofautiana katika kuthamini uzuri wa nje wa mwanamke.
Kuna wanaopenda wanawake:-
weusi, wembamba,
weusi, wanene
weupe wembamba,
weupe wanene,
Virema n.k
Ukimuoji kila mtu ana sababu zake zinazomfanya apende aina fulani.
 
Natofautiana nawewe kabisa, mimi naamini kwamba wanaume wanapenda kuoa wanawake wazuri ndiyo maana wapo tayari kuishi nao. Hivi inaingia akilini kwamba mtu hataki kitu kizuri? labda ungefafanua unaposema UZURI unamaanisha nini. kwasababu to me my wife ndo mwanamke mzuri kuliko wote.
Labda hujasoma vizuri nilichosema nimesema wanawake wazuri sana, kwa wanaume wa ukweli wanajua kuwa tukiwa tumekaa kundi la wanaume na akapita mwanamke kuna watakaosema ni mzuri na kuna watakaopinga. Ila kuna wakati kuna mwanamke anapita na kundi zima linakubaliana kwamba huyu ni mzuri, hao sasa ndio nawaongelea mimi
 
kwahiyo unamaanisha uzuri wa sura, nyonyo, wowowo na miguu au?

ehh mzuri km mke wa HAMISI KISHINDINDO...dah nikikumbuka tu nacheka yann..leo rahaaaa kishindindo sikipatii picha kikoje...kifup fup kinene umbo km boksi ivi ..afu kina ndevu km osama enhh?
au kikoje koje jaman,,,,
 
Ahahahahaaaaa…..huyo Mwajuma kakuharibu wewe. Kaa naye mbali.
 
acha hizo, so unataka kusema wote walioolewa ni wabaya? labda mkeo ndo mbaya, kama watu wameshapendana nini kingine kinatakiwa, kwani we hujui kila mtu na mtuwe?
 
Back
Top Bottom