Utafiti: Wanawake wengi wanaogopa wadudu

Utafiti: Wanawake wengi wanaogopa wadudu

Wakuu habari za leo,

Uzoefu katika maisha ni moja ya taasisi kubwa za kielimu.Nimeishi miaka mingi na kugundua mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ujasiri wa wanawake mbele ya wadudu wadogo.

Wanawake wengi wanaogopa wadudu wafuatao:
1- Mende
2- Chura
3- Kiwavi
4- Jongoo

Kwa kawaida mwanamke anaeogopa wadudu,anapokabiliana nae akiwa katika mazingira yafuatayo,tegemea ajali ama mayowe:

1- Akiwa anaendesha gari
2- Akiwa ameshikilia sahani ya chakula mkononi
3- Hata akiwa anafanya mapenzi
b3f91254316afc3c470d241d31711aa5.jpg

Juu yenu iwepo amani.
 
Chura na jongoo siyo wadudu! Thread yko ina ukweli pia kuhusu wanawake kuogopa viumbe mbalimbali ukilinganisha wanaume ingawa wanataka 50 kwa 50 ikiwezekana hata kesho!
 
me wife akiona nyoka hata kwenye TV ujue siku hiyo tunalala macho huku tumewasha taa ya chumbani isee,wanawake ni viumbe vinavyohitaji caring na unyenyekevu wa hali ya juu sana.
 
Nachukia wadudu vibaya mno. mwili unasisimka kweli nikikutana na mdudu au bahati mbaya sijamuona na yupo karibu yangu. agrrrrr!!
 
1.Mende:
Kingdom-animalia.
Phylum-anthropoda.
class-insecta

Mende ni mdudu.

2.Chura:
Kingdom-animalia.
Phylum-chordata.
class-amphibia.

Chura si mdudu ni amfibia.

3.Kiwavi wa kipepeo.
Kingdom-animalia.
Phylum-anthropoda.
Class-insecta.

kiwavi ni mdudu.

4.Jongoo:
Kingdom-animalia.
Phylum-anthropoda.
Class-diplopoda.

Jongoo si mdudu.

5.Nyoka:
Kingdom-animalia.
Phylum-chordata.
Class-reptilia.

Nyoka si mdudu ni reptile.
 
Back
Top Bottom