Utafiti wambeba Magufuli urais 2015

Utafiti wambeba Magufuli urais 2015

Hiyo ndiyo Elimu yetu Tanzania tena ktk kumaliza utaona "LY" kwenye shati zetu wewe he?

Wewe kilaza hiyo akili yako ni mgando acha kuisingizia elimu ya Tz.
Hao maprofesa walisomea Kenya?
 
Katika tafiti inayoendeshwa na NewdealAfrika,utafiti unaonesha kuwa Lowasa ana 74%,magufuli 22% huku asilimia zilizobakia za watu ambao hawajaamua wampigie nani.ingia kwenye lukemusicfactory.blogsport.com utapata ushahidi huu
 
Nipashe toleo la 26/10/15.. Lowasa amgaragaza Magufuli.. Ashinda kwa asilimia zaidi ya 70.. Avuna majimbo zaidi ya 170..
 
Watanzania vijana wa 1980 kuendelea ni wengi kuliko wa zamani, wote wameichoka CCM na ghiliba zake!!
Huko vijini walikuwa hawajui faida ya kura, ugumu wa maisha na dhuluma za watendaji zimekuwa darasa!!
MaCCM hawana pa kutokea wamebanwa, wanapumulia machine, bado muda kidogo tuachane nao!!
Uongo wa mitandao na media hausaidii, kifo cha nyani miti yote huteleza!!
 
Wewe kilaza hiyo akili yako ni mgando acha kuisingizia elimu ya Tz.
Hao maprofesa walisomea Kenya?

Pole pole kwani hakuna jina jingine zaidi ya hilo au matusi ni ktk misamiati yenu Tz ni yetu sote
 
Huu utafiti umefanyika nchi ya msoga sio Tanganyika na Zanzibar
 
Watanzania vijana wa 1980 kuendelea ni wengi kuliko wa zamani, wote wameichoka CCM na ghiliba zake!!
Huko vijini walikuwa hawajui faida ya kura, ugumu wa maisha na dhuluma za watendaji zimekuwa darasa!!
MaCCM hawana pa kutokea wamebanwa, wanapumulia machine, bado muda kidogo tuachane nao!!
Uongo wa mitandao na media hausaidii, kifo cha nyani miti yote huteleza!!

Kwa kauli yako ni kwamba Elimu ya Uraia/Mpiga kura imewafikia wa Tz kwa hiyo FISADI akishindwa msimtafute mchawi
 
View attachment 278949

Utafiti waonyesha Magufuli ana uwezo mkubwa wa kuwa Rais

Na Mwandishi Wetu

WAKATI kesho Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikitarajia kufanya uzinduzi wa kampeni zake kwenye viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, Taasisi ya Maendeleo, Vijana, Uongozi na Utawala Bora(YDG) imetoa utafiti na kuonyesha mgombea wa nafasi ya Urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli anaongoza.

Utafiti huo ulitolewa jana mjini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo, Christopher Maganila, ambaye alisema katika utafiti walioufanya kuwa endapo uchaguzi mkuu ungefanyika leo, Dk Magufuli angeshinda nafasi hiyo.

Alisema matokeo hayo, yanaonyesha Dk. Magufuli angeshinda kwa asilimia 45, huku mgombea wa CHADEMA Edward Lowassa angekuwa na asilimia 10.5, huku asilimia 35 wakisema hawajaamua mgombea gani anaweza kuwa Rais kwa kuwa ni bado mapema mno.

Matokeo hayo pia yalionyesha kuwa wagombea wengine wangepata asilimia 0.1 hadi 5 huku asilimia 8 wakionekana wakisema hawajui ni mtu gani anafaa kuwa Rais kati ya wagombea waliochukua fomu za kuwania nafasi hiyo.

“Huu ni utafiti huru na umefanikiwa kufika kwenye kila mkoa lakini kwa wilaya moja kwa kuwa tumeamua kuwahi ili kuona mwamko wa wananchi katika kupiga kura na kuchagua mgombea wanayemhitaji,’’alisema.

Hata hivyo, Katibu huyo mtendaji alisema sababu nyingi walizoonekana kuzitoa wananchi kuwa Dk. Magufuli atakuwa mtendaji na mtu mwenye upeo mkubwa wa kufanya kazi endapo akipewa ridhaa.

Kwa mujibu wa Katibu huyo, alisema anaamini uchaguzi wa mwaka huu, utakuwa huru na haki kwa kuwa wananchi wameonekana kuwa na mwamko katika kuchagua kiongozi atakayewaongoza.

<Dk. Magufuli ni mtendaji na mtu mwenye upeo mkubwa> maneno kama hayo ndo tunataka kusikia vijana.

#magufuli juuuuuuuuu
CCM juuuuu
Naipenda Tanzania yangu
 
Watanzania vijana wa 1980 kuendelea ni wengi kuliko wa zamani, wote wameichoka CCM na ghiliba zake!!
Huko vijini walikuwa hawajui faida ya kura, ugumu wa maisha na dhuluma za watendaji zimekuwa darasa!!
MaCCM hawana pa kutokea wamebanwa, wanapumulia machine, bado muda kidogo tuachane nao!!
Uongo wa mitandao na media hausaidii, kifo cha nyani miti yote huteleza!!
Acha matusi sisi wazee wa zamani ndio tumeichoka kabisa CCM , usirudie kutuhusisha na CCM.
 
View attachment 278949

Utafiti waonyesha Magufuli ana uwezo mkubwa wa kuwa Rais

Na Mwandishi Wetu

WAKATI kesho Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikitarajia kufanya uzinduzi wa kampeni zake kwenye viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, Taasisi ya Maendeleo, Vijana, Uongozi na Utawala Bora(YDG) imetoa utafiti na kuonyesha mgombea wa nafasi ya Urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli anaongoza.

Utafiti huo ulitolewa jana mjini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo, Christopher Maganila, ambaye alisema katika utafiti walioufanya kuwa endapo uchaguzi mkuu ungefanyika leo, Dk Magufuli angeshinda nafasi hiyo.

Alisema matokeo hayo, yanaonyesha Dk. Magufuli angeshinda kwa asilimia 45, huku mgombea wa CHADEMA Edward Lowassa angekuwa na asilimia 10.5, huku asilimia 35 wakisema hawajaamua mgombea gani anaweza kuwa Rais kwa kuwa ni bado mapema mno.

Matokeo hayo pia yalionyesha kuwa wagombea wengine wangepata asilimia 0.1 hadi 5 huku asilimia 8 wakionekana wakisema hawajui ni mtu gani anafaa kuwa Rais kati ya wagombea waliochukua fomu za kuwania nafasi hiyo.

“Huu ni utafiti huru na umefanikiwa kufika kwenye kila mkoa lakini kwa wilaya moja kwa kuwa tumeamua kuwahi ili kuona mwamko wa wananchi katika kupiga kura na kuchagua mgombea wanayemhitaji,’’alisema.

Hata hivyo, Katibu huyo mtendaji alisema sababu nyingi walizoonekana kuzitoa wananchi kuwa Dk. Magufuli atakuwa mtendaji na mtu mwenye upeo mkubwa wa kufanya kazi endapo akipewa ridhaa.

Kwa mujibu wa Katibu huyo, alisema anaamini uchaguzi wa mwaka huu, utakuwa huru na haki kwa kuwa wananchi wameonekana kuwa na mwamko katika kuchagua kiongozi atakayewaongoza.
Walifanyia wapi utafiti huo? Ni kwanini CCM pekee ndo mmeuona? Wameupublisize wapi?
 
Magufuli ikiwa atachaguliwa kuwa rais ni uwezo wa kusimamia miradi ya maendeleo. Magufuli ni mtu wa namna hiyo na ametuonyesha katika sekta ya ujenzi na hasa katika eneo la barabara. Moja ya masuala ambayo nayaona kama mafanikio makubwa ya serikali ya Kikwete ni ujenzi wa barabara, ukiniuliza, nitakwambia jambo hili ndilo Kikwete anapaswa kujivunia atakaporudi nyumbani kwake pale ‘Msoga’. Lakini aliyeleta mapinduzi hayo kiusimamizi ni Magufuli.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa “ikitolewa tenda ya ujenzi wa barabara nchini Tanzania na India halafu nchi zote zikakabidhi tenda hizo kwa watoto wa marais wa nchi, kule India walau barabara ya ‘kudanganyishia’ itajengwa lakini hapa Tanzania unaweza usione hata kokoto” (tafsiri yangu). Dhana hiyo ina maana kwamba huku kwetu wizi na kujijazia manoti ndivyo vitu vinavyoshamiri na kwa tafsiri ya Mwalimu “ilipasa Magufuli awe anaongoza kwa kuchukua noti za barabara na kuzijaza tumboni kwake”, jambo ambalo limekuwa nadra kutokea na kama liliwahi kuwepo ndiyo tutajua sasa wakati watu wataanza kutoa taarifa zake kwa sababu anataka kwenda Ikulu. Kwa uwezo huu wa kiusimamizi namuona Magufuli akisimamia miradi ya serikali kwa ustadi mkubwa hata kama siyo “waziri wa miradi”
Hakuna kitu kama hicho. Rangi ya kijani ni tatizo kwa maskini. Mfumo wa rushwa kubwakubwa atauweza wapi?
 
Acha matusi sisi wazee wa zamani ndio tumeichoka kabisa CCM , usirudie kutuhusisha na CCM.

Hahahaaaaa, hata bibi yangu kijijini anasema anawapa Chadema kura yake.
Na kuna mgombea wa ubunge kupitia CCM wanadai hawataki hata kumsikia.
 
Ben Sanane aliamini hayo ya JF akaenda Rombo muulize kilichomkuta

Wee &#128023;&#128023; Ben Saanane ni wa CDM... that was battle within CHADEMA...

This is Lowassa, Ukawa... acha ushoga, Lowassa, Ukawa ni issue nyingine kabisa... Hiyo comparison yako ya ki kipuuzi...!!!

Lowassa tuko 80% and above kwa Magufuli...!!! Magufuli kumlinganisha na Lowassa ni dhambiii...!!!

Magufuli hana hata sifa ya kuwa kiongozi bora.. Chato kata zote except 1 tu imebakia CCM... na hapo ndio lilikuwa jimbo lake...!!!

Acha kuwa kichwa kondoo...
 
Back
Top Bottom