Utafiti: Waislam walisusia sensa kwa asilimia 60% | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafiti: Waislam walisusia sensa kwa asilimia 60%

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by thatha, Sep 1, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Uchunguzi wakawaida utagundua idadi kubwa ya waliokosoa serekali kutaka kipengele cha dini ktk sensa ni wasomi wa kiislam waliopitia vyuo vikuu vya taifa ambao wanaujua mfumo mzima wa serekali unavyoendeshwa na athari yake kwa taifa.
  ndio wasomi walioibua athari ya MOU kwa taifa.
  . Lkn pia inaonyesha idadi kubwa ya jamii ya kiislam wamesusia sensa ingawa liziutumika nguvu na wengine kuhesabiwa kwa mtutu wa bunduki wakiwa wameelekezewa.
  kipindi kirefu nilipokuwa nasikiliza redio za kiislam hakuna hata redio moja iliowahi kuhamasisha sensa tofaut na redio za Umma kama TBC, redio Uhuru, redio one , Redio Free Africa na Clouds fm, times na nyengine.
  lkn hata redio za waumini wa kikiristo kama redio Tumaini na Wapo redio zilikuwa zinatoa matangazo ya sensa kila wakati.
  chakushangaza hata redio Qurani inayomilikiwa na BAKWATA nayo haikuwahi kutoa tangazo lolote la sensa huku redio Kheir, redio imaan wao wakiwaweka masheikh wanaopinga SENSA, Redio Nuur,redio Adhana nazo Zikipiga qasida wala hujui kama kuna sensa
  .
  hata hao masheikh na watu wa Takwimu ambao wakihamasisha sensa wakitumia TBC au redio one na sio kwenye vyombo vya habari vya madhehebu ya kiislam ambapo jamii kubwa ya kiislam ndio inasikiliza.
  huu ni ushahidi kwamba waislam walilazimishwa tu, na wengi wanapendekeza uchaguzi 2015 serekali itumie nguvu kwa wale wote wanaokataa kumchagua Mbunge au rais wa nchi kwa manufaa ya taifa kama ilivyosensa
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,080
  Trophy Points: 280
  Na uchaguzi mkuu wasusie kwa 80%.
   
 3. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  waache wasuse tuu, sisi tujenge taifa lenye nguvu za kiuchumi baasiii
   
 4. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Umesahau kudokesa Kuwa vipo vyombo vilivyojitahidi kuhamasisha sensa hata kwa kuvunja sheria mfano Tarehe 24-25 August 2012 Tanzania Daima,Habari leo na Mtanzania kwenye kurasa za mbele ilitoa tangazo feki kuonesha kuwa Katibu wa Jumuiya ya Taasis za Kiislam (sheikh Ponda) anawataka waislam washiriki sensa, hiyo nguvu ya kuhamasisha sensa ielekezwe pia kwenye kilimo kwanza!
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  ili wakiristo waichagua chadema kiulaini?
   
 6. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Matangazo kawaida huwa yanalipiwa airtime hamna vya bure. Iweje mabilioni yatumeke na radio za kiislamu wasigawiwe hata fungu la kupigia debe sensa? Kwani hizo radio hawalipii leseni na kodi nyenginezo serikalini? Hapa ndio ieleweke vile uislamu na vyombo vyao vinavyopigwa vita hata na serikali.
   
 7. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa hapo ndio umetuthibitishia kuwa waislamu wamegoma kwa asilimia 60??? mbona ni porojo tupu? GREA THINKER WA SIKU HIZI NOMA!!!
   
 8. N

  Nil Member

  #8
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TUANZISHE TENA KIJIJI CHA NGENGEMKENI MITO MINGI
  Kwa kuwa umenihakikishia kuwa waliogomea sensa ni wasomi, nachelea kusema kwamba tuanzishe tena kijiji cha Ngengemkeni Mitomingi. Wale wasomi waliosoma kitabu cha penzi kitovu cha uzembe, wanajua maudhui ya kitabu hicho, moja ya maudhui ni ya wananch wa kijiji hicho kugomea sensa wakidai kuwa anayehesabu watu anataka kuwaroga. Nachelea tena kusema kwamba, hata waislam waliogomea sensa sababu yao ni ile ile, kwamba wakihesabiwa bila kuwepo na kipengere cha dini basi wanarogwa kimaendeleo.
  Binafsi, sikuona haja ya vyombo vya habari vya kidini kulazimika kuitangaza sensa, kwani sensa ni zoezi la Kitaifa, si la kidini, ila kama chombo cha dini kitatangaza, sawa tu, kisipotangaza, sawa pia.
  Binafsi, hainishtui eti wasomo nao wamegomea sensa, wala isikupe moyo na kuona kuwa kuna usahihi,"kusoma si kuelimika" na ktk karne hii, Tanzania kuna wasomi wengi wenye ugonjwa ktk kupambanua masuala yahusuyo dini na mustakabali wa Taifa.Nachelea tena kusema wasomi wa namna hiyo wana ugonjwa mbaya sanausio na tiba rahisi, na mara nyingi ukiwapima wana uwezo mdogo hata ktk Taaluma walizozisomea, bila kujali kiwango cha Taaluma walizonazo. Natambua kwamba wapo wenye kiwango cha juu cha Taaluma zao, na hao ukiwasikia wanashindwa kupambanua masuala hayo, wanafanya maksudi kwa maslahi ya kisiasa.
  MWISHO. Serikali ilitakiwa kuwakusanya wote waliogomea sensa na kuwalundika ktk kijiji maalum kitakachopewa jina la Ngengemkeni Mito Mingi, kwa makumbusho ya kihistoria.
   
 9. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UMESEMA KWELI.kama wanasusa sisi twala inga waliogoma ni wachache sana tena waliosoma kiongoongo. waislamu wanao ujua uislamu wote wamehesabiwa.waliogoma aibu kwao.
   
 10. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Mahindi yangegoma kukua ningeogopa njaa.
   
 11. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  ....Kina Ponda hawajauona mtego waliojiwekea wenyewe; leo wanatamba kwamba wamefanikiwa kususia sensa, lakin kesho watakuwa na wakati mgumu kuushawishi umma wa watanzania kuwa waislam ni wengi nchi hii maana majumuisho ya sensa yanaweza onesha kwamba tupo mil.45. Hapo watu watakuwa na sababu ya kuamini kwamba wakristo na wapagani ndo wengi zaidi!
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Basi kulikua na haja gani ya kuweka kipengele cha dini kwenye sensa? Kama mmeweza toa takwimu kuwa asilimia 60 walisusia basi inamaana mna jua asilimia 100 ya waislamu ni wangapi...
   
 13. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi ningaliiona sensa ya maana kama serikali inatumia raslimali zake kuinua uchumi na hali duni ya watanzania. Unaspend hela nyingi kuhesabu watu wakati shule hazina hata madawati? Unamhesabu mtu leo kesho anakufa kwa kukosa dawa ya kutuliza maumivu? Wamama wanaenda kujifungua wanalundikana kama ng'ombe kwenye chumba kimoja bila vitanda wala huduma muhimu? Kama huwezi kumhudumia hata mjamzito unamhesabu nani?
  Kwenda kuwahesabu watanzania ni usanii mtupu. Kwanza serikali ishughulikie mahitaji muhimu kama elimu, mahospitali, barabara hadi vijijini then ituhesabu. Watanzania tumekata tamaa kwani viongozi wanajilundikia mali huku sisi tukifa duni. Unamhesabuje mwananchi ambae hutibiwi hospitali moja nae? Ni kwa nini wasiwahesabu wale wanaopokea matibabu India tukajua ni kiasi gani cha kodi kinahitajika kwa mwaka ili tujikunje kufanikisha matibabu hayo?
  Sensa ya kitanzania ni kama mtu anasesabu tu mbuzi. Haina manufaa yeyote kwa raia wake. Kama mtu anagoma kuhesabiwa ni sawa kabisa na ni haki yake. Tuache unafiki na tuambiane ukweli. Wanaonufaika na uchumi wa Tanzania sii watanzania hata kidogo.
  Kama serikali inafanya kazi ya serikali basi ikiita watu kuhesabiwa wataenda tena bila ubishi wowote, ila kama ni huu usanii na unafiki wa kujinufaisha binafsi na familia zenu wengi watawagomea. Tunahitaji serikali itakayoweka system in order ili mtoto akizaliwa ajulikane amezaliwa. Mtu akifa ajulikane amekufa na sii ujinga wa kusukumana na watu eti unawahesabu huku huwahudumii hata katika mahitaji ya msingi.
  Jengeni shule bora, hospitali za maana na njia bora za usafiri kwanza. Wapeni wanetu elimu bora. Jengeni vyuo bora na sii kuwakimbiza watoto wenu kusoma nje kwa garama ya mashule yetu. Rudisheni kwanza usafiri wa reli ili wananchi wasafirishe mazao na bidhaa zao bila usumbufu wa kulipia malori ya ridhimoja na vituo vyake vya mafuta.
  Acheni unafiki. Hii serikali haina lolote la maana hata kama tungalihesabiwa wote kabisa. Sensa itajikamilisha yenyewe kama serikali inaihudumia jamii iliyoiweka madarakani. Bila hivyo hata tungalijipanga wote kwenye mstari na kuhesabiwa kwaq pamoja ni bure.
   
 14. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hiyo asilimia sitini inakujaje?

   
 15. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,134
  Likes Received: 10,484
  Trophy Points: 280
  We umehesabiwa?
   
 16. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Halafu wewe unayezungumza uongo huu unajifanya unazungumza kwa niaba ya imani ya kiislamu?
  Hebu tueleze ulivyoipata hiyo asilimia 60 kama si umbea, ufitini na majungu yanayopigwa vita na uislamu? Ulipata wapi muda wa kukutana na waislamu wote nchini ndani ya siku saba za sensa na kuipata hiyo asilimia unayodanganya imefikiwa? Ama kweli adui wa uislamu yu ndani ya uislamu wenyewe kwani kwa kukosa umakini baadhi wanaudhalilisha uislamu wakidhani wanautetea! Kuna faida gani kususia sensa wakati tunagombania vitambulisho vya uraia? Hamuoni kugoma kujiandikisha ni kuzihujumu jumuia tuishizo ambapo idadi ya watu itachukuliwa ya wale waliojiandikisha wakati wa sensa na mipango yao ya maendeleo kukadiriwa kwa idadi iliyopatikana katika sensa husika wakati nyinyi kwa makusudi mmejipunguza lakini mtahitaji huduma zilezile? Ama kweli wajinga ndiyo waliwao.
   
 17. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  HIVI KUWEKA KIPENGELE CHA DINI KUNA UGUMU GANI JAMANI...MAANA MIE NIMESHUKA JUZI TOKA SAYARI YA MARS NILIKUA SIJUI KWA NINI WAMEGOMEA SENSA HAWA JAMAA......

  Kama ilikua inawezekana kuweka hicho kipengele na bila kumbugudhi mtu au dini nyingine basi nadhani hawa jamaa wapo sahihi....KWA NINI TUKATAE,,,JE TUKIKUBALI KUNA UBAYA GANI....NA TUKIKATAA KUWEKA HICHO KIPENGELE KINA UBAYA GANI
   
 18. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acha porojo na majungu ,kama mmefanya utafiti na kugundua mpo asilimia sitini mliogomea sensa mbona miaka yote mmeshidwa kujijua mko wangapi.
   
 19. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu umenikumbusha mbali kidogo lakini Ngekemkeni mito mingi sio jina la kijiji bali ni jina la character (Baba Mazoea) ambaye alikuwa mjumbe aliyempokea Ngoswe.
  Anyway, nadhani ishu ya kugomea sensa kuna jambo ambalo limejificha ndani yake pengine hata waliogomea hawalijui.
  Nilipata kuongea na rafiki yangu mmoja ambaye na yeye alikuwa ni mmoja wa wagomaji.
  Nilimuuliza anipe sababu za yeye sababu ya kugoma alinijibu kwa kifupi tu kuwa anafuata maagizo ya kiongozi wake.
  Full stop.
   
 20. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Mimi niligoma kuhesabiwa (japokuwa sikutanganza) lakini si kwa sababu ya kipengee cha dini (mimi si muumini wa Kiislamau wala wa Kikristu, ninajiweka katika kundi la Wajadi) bali ni kwa sababu naiona sensa ya Bongo kama usanii tu nami sitaki kuwa sehemu ya usanii huo. Ninaomba unipe sababu mbili kuu kwa nini nisigome kuhesabiwa!
  Mwaka 2002 nilihesabiwa mimi na familia yangu lakini nikipita mitaani ninakuta watoto wa shule za msingi wamekalia mawe darasani kama si kukaa sakafuni huku wakiwa wamerundikana katika chumba kimoja cha darasa kama maguni ya maharakwe kwenye Fuso! Nikipita vijijini akina mama na wasichana wadogo bado wanatembea maili zaidi ya sita kutafuta maji ya kunywa na kupikia! Leo hii watawala wetu wanatuhamasisha kuhesabaiwa kwa madai kuwa sensa inawasaidia kupanga maendeleo!! Mimi ninafikiri hata Masheikh waliogomea sensa kwa msingi wa dini wamedhihirisha welewa wa hali ya juu wa uchambuzi wa masuala ya kidunia zaidi ya nyie mnaotaka kuhesabiwa tu bila kujua kwa nini mnahesabiwa alimradi amesema Rais kama kama sio Rahisi.
   
Loading...