Elections 2010 Utafiti wa TCIB: Dk. Slaa aongoza

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Tanzania Citizen's Information Bureau (TCIB) na kutolewa leo umeonyesha Dk Slaa anaongoza kwa asilimia 45, JK asilimia 41,Prof. Lipumba asilimia 10, Hashim Rungwe 2, Peter Mziray 1 na Mutamwega 1.


Utafiti huu umefanyika kwenye mikoa 15 iliyochaguliwa kwa njia ya kinasibu (random sampling ) na kwenye jimbo moja katika kila mkoa wananchi kati ya 60 na 100 walihojiwa. Utafiti umefanywa ndani ya mwezi huu na kutolewa leo Jijini Dar es Salaam.


mnajua kuwa Halima mdee ambaye ni mbunge wa Chadema ni muasisi wa Taasisi hii? iko Mikocheni.imeundwa mwaka jana.hivyo basi kuna Conflict of Interest. Halima ametumia Influence yake kumjenga kisiasa Bosi wake.mimi siamini matokeo haya.
 
Last edited by a moderator:
hapo kwenye red kuna tatizo. ni vyema utafiti ufanywe kwa wale watakaopiga kura na si kuchanganya na watoto wa shule za msingi

na inaonekana hiyo sio random sampling

Sio watoto, bali walioulizwa walikuwa na hizo Elimu. Mwandishi kakosea!
 
No wonder, results reflected the reality. Every body knows that competition is almost half for two rulling party Vs CHADEMA. But many peple know why are we poor, and every thing are so stagnant, fake mine contracts, fake governmental expenditures etc.Tanzanians now this. WE ARE DECLARING THAT ENOUGH IS ENOUGH.
 
Utafiti wa kibwege uliojaa ushabiki tu!! kwa lipi alilonalo Slaa mpaka apate asilimia zote hizo huku ni kujidanganya kiakili, subirini oktoba 31 ndio mtajua Kikwete ni mwisho wa rubishi ya batoto, harakaati za Slaa hazina mafanikio yoyote anapoteza muda ni sawa na harakati za mbwa anaetaka kuzaa na nguruwe
 
Utafiti wa kibwege uliojaa ushabiki tu!! kwa lipi alilonalo Slaa mpaka apate asilimia zote hizo huku ni kujidanganya kiakili, subirini oktoba 31 ndio mtajua Kikwete ni mwisho wa rubishi ya batoto, harakaati za Slaa hazina mafanikio yoyote anapoteza muda ni sawa na harakati za mbwa anaetaka kuzaa na nguruwe

Toa hoja kujadili utafiti umekabwa na simanzi na bado terehe 31 october utajiharishia kabisa wenye nchi hawataki mtu anayeweweseka kuongoza nchi yetu
 
Kura mpya ya maoni: Dk. Slaa ampiku JK
• Wazee wengi ni wa Kikwete, vijana wa Dk. Slaa

na Bakari Kimwanga


KURA nyingine ya maoni iliyoendeshwa na taasisi ya Tanzania Citizens Information Bureau (TCIB) inaonyesha kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ndiye mgombea anayekubalika zaidi katika uchaguzi wa mwaka huu kuliko mwingine yeyote.
Matokeo ya kura hiyo ya maoni yaliyotangazwa jana jijini Dar es Salaam yanaonyesha kuwa Dk. Slaa alikuwa ndiye mgombea aliyekuwa akipewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda urais mwaka huu na ambaye pia angepigiwa kura na watu wengi zaidi waliohojiwa katika utafiti huo.
Akitangaza matokeo ya kura hiyo ya maoni katika Hoteli ya Courtyard, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Vincent Leyaro, alisema utafiti huo ulikusanya maoni ya wananchi katika mikoa 15 ya Tanzania Bara kwa kuchagua jimbo moja kila mkoa, kata mbili mbali na vijiji na mitaa miwili katika majimbo husika.
Dk. Leyaro alisema miongoni mwa watu 3,047 waliohojiwa katika utafiti huo ulioendeshwa katika kipindi cha kati ya Septemba 27 na Oktoba 10, asilimia 48 walimpa Dk. Slaa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu, huku mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete akipata asilimia 38 na nafasi ya tatu ikishikwa na Profesa Ibrahimu Lipumba anayegombea kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) ambaye alitajwa na asilimia 9 ya waliopiga kura hiyo ya maoni.
Mbali ya hilo, utafiti huo uliwauliza waliohojiwa iwapo uchaguzi ungefanyika siku walipohojiwa wangemchagua mgombea gani kuwa rais, asilimia 45 walimtaja Dk. Slaa, asilimia 41 wakisena watampigia kura Kikwete na asilimia 10 wakimtaja Profesa Lipumba.
Matokeo hayo ya TCIB, taasisi inayojumuisha wanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanamfanya Rais Kikwete kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano kuporomoka kutoka katika kuongoza kura za maoni hadi kushika nafasi ya pili nyuma ya mgombea kutoka kambi ya upinzani.
Akiendelea kueleza namna walivyofanya utafiti wao, Dk. Leyaro alisema katika washiriki wote 3047 waliohojiwa, asilimia 18.3 walisema wao ni wanachama au mashabiki wa CCM, wakati asilimia 15.6 walijitanabahisha na CHADEMA na asilimia 12 wakijifungamanisha na CUF.
Mbali ya hao watafiti hao walisema asilimia 31. 6 ya watu wote waliohojiwa walijitaja kuwa watu ambao hawakuwa wanachama au mashabiki wa chama chochote cha siasa miongoni mwa vyama 18 vilivyo katika daftari la msajili wa vyama.
Katika uchambuzi wa upigaji kura kwa mtazamo wa vyama, matokeo ya kura hizo za maoni yalionyesha kuwa asilimia 72 ya watu waliohojiwa ambao walisema walikuwa hawafungamani na chama chochote cha siasa walimtaja Dk. Slaa kuwa ndiye chaguo lao, akafuatiwa kwa mbali na Kikwete aliyepata asilimia 11 na Lipumba akapata asilimia 10.
Katika eneo jingine kura hiyo ya maoni inaonyesha kuwa wakati Kikwete anaungwa mkono na asilimia 80 ya wapiga kura wa ndani ya CCM, Dk. Slaa alikuwa akiungwa mkono na asilimia 90 ya wana CHADEMA huku Lipumba akiungwa mkono na asilimia 38 ya mashabiki na wanachama wa CUF.
Utafiti huo ulitoa matokeo mengine ya kushangaza baada ya kuonyesha kwamba asilimia 15 ya wanachama na wapenzi wa CCM walikuwa wakimuunga mkono Dk. Slaa wa CHADEMA huku wana CUF wafikao asilimia 48 wakimuunga mkono Kikwete badala ya mgombea wao wa urais, Profesa Lipumba.
Dk. Leyaro alisema utafiti huo pia ulifanya uchambuzi wa wahojiwa kirika na kubaini kuwa vijana wengi zaidi miongoni mwa waliohojiwa walisema watamchagua Dk. Slaa, huku sehemu ya kundi la watu wa umri wa zaidi ya miaka 50 likisema kuwa litamchagua Kikwete.
“Tulipofanya uchambuzi kwa makundi ya umri wa wahojiwa, ilijitokeza kuwa vijana wengi walimchagua mgombea wa CHADEMA (Slaa) wakati wahojiwa wa umri wa zaidi ya miaka 50 walimchagua mgombea wa CCM,” alisema Dk. Leyaro.
Katika eneo hili, utafiti huo ulibainisha kwamba asilimia 25 ya wahojiwa wenye umri wa chini ya miaka 25 walisema watamchagua Kikwete wakati asilimia 55 ya waliohojiwa wenye umri wa miaka chini ya miaka 50 walisema watamchagua Dk. Slaa. Utafiti huo ulionyesha pia kwamba kwa wahojiwa wenye umri wa kati ya miaka 46 na 55 asilimia 50 walisema watamchagua Kikwete huku watu wa kundi hilo wapatao asilimia 35 wakimtaja Dk. Slaa, hali inayoonyesha kwamba mgombea wa CCM alikuwa akiungwa mkono zaidi na wagombea wenye umri mkubwa na wazee wakati Dk. Slaa akiungwa mkono zaidi na vijana na watu wenye umri wa kati. Kwa upande wa mikoa na namna wagombea hao walivyoonekana kuungwa mkono, Kikwete aliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko wengine katika mikoa ya Dodoma (59.3%), Lindi (43.4%) Mbeya (50%), Rukwa (54.3%), Ruvuma (55%) na Tabora (42%).
Wakati Kikwete akiongoza katika mikoa hiyo sita, Dk. Slaa yeye aliongoza katika mikoa minane ya Arusha (60%), Dar es Salaam (42%), Iringa (58.2), Kagera (49%), Kilimanjaro (71%), Mara (54%), Manyara (79.8%) na Mwanza (42.1%) huku Profesa Lipumba akiwa haongozi katika mkoa wowote na akafanikiwa kushika nafasi ya pili katika mkoa mmoja tu wa Lindi (38.1%).
Hata hivyo Dk. Leyaro, alisema kuwa matokeo hayo ni kura ya maoni sio lazima yawe taswira halisi ya siku ya kupiga kura na kusisitiza kuwa hali halisi ya matokeo itajulikana baada ya wananchi kupiga kura katika uchaguzi ulio huru na haki.
Alisema taasisi hiyo haitarajii wagombea na wapiga kura wao kubweteka au kukata tamaa kwa sababu ya matokeo ya kura za maoni na kutoa changamoto kwa kufanywa mara nyingi kwa kura hizo za maoni na mashirika mengi ambayo ni huru yasiyoegemea upande wowote.
Hata hivyo alisema matokeo hayo yanaweza kusaidia wagombea kujikita vizuri katika muda wa kampeni uliobaki kwa kuzingatia wapi wanakubalika zaidi na makundi gani ili waweze kuelekeza nguvu zao ipasavyo katika muda wa kampeni.
Wiki chache zilizopita taasisi ya Synovate ikionyesha mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Slaa, kupanda kwa alama nne, huku mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, akishuka kwa alama 10.
Matokeo hayo yalipishana na yale yaliyotolewa na taasisi ya Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) ambayo ilimpa Kikwete asilimia 71.2, Dk. Slaa (12.3) na mgombea wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (10.3).


h.sep3.gif


juu
blank.gif
 
We hizi taasisi za kikatoliki unategemea zitaongea utumbo gani zaidi ya kumsifia mchungaji mwenzao Slaa na chama chao cha kanisa ???? to hell!!!
 
Ongeza na haya ya Mtandao wa Gazeti la Mwananchi

Kuongoza Tanzania 2010-2015 kura yako utampa nani?
Select Poll Select a poll from the listNi gazeti lipi unaloliamini zaidi?Nani atakuwa Rais wa awamu ya sita Zanzibar?Waziri kupiga goti na kutoa shikamoo ni ishara ya unyenyekevu wa kweli?Kuongoza Tanzania 2010-2015 kura yako utampa nani?

poll.png
Kuongoza Tanzania 2010-2015 kura yako utampa nani? Willibrod Slaa - CHADEMA 2572 72.2%
Jakaya Mrisho Kikwete - CCM 794 22.3%
Ibrahim Lipumba - CUF 162 4.5%
Hashim Rungwe - NCCR-Mageuzi 18 0.5%
Mutamwega Mugahywa - TLP 17 0.5%

Number of Voters : 3563 First Vote : Tuesday, 12 October 2010 11:18 Last Vote : Saturday, 16 October 2010 14:05
 
We hizi taasisi za kikatoliki unategemea zitaongea utumbo gani zaidi ya kumsifia mchungaji mwenzao Slaa na chama chao cha kanisa ???? to hell!!!

Unaweza kusoma tu siolazima ukachangia,,
Ukatoliki umetoka wapi hapa,,naona umelewa uislam wako mpaka unakuwa mvivu wa kufikiri na kuelewa,, na ndo maana kila siku mtaishia kulalamika tu. Inakera saana mnapohusisha kila kitu na Ukatoliki as if katoliki ndio dini pekee Tanganyika.
 
Utafiti wa kibwege uliojaa ushabiki tu!! kwa lipi alilonalo Slaa mpaka apate asilimia zote hizo huku ni kujidanganya kiakili, subirini oktoba 31 ndio mtajua Kikwete ni mwisho wa rubishi ya batoto, harakaati za Slaa hazina mafanikio yoyote anapoteza muda ni sawa na harakati za mbwa anaetaka kuzaa na nguruwe


Halafu wewe mkuu unaclose that line...Kuna mbwa wangu hata nguruwe anawapa dozi tuu nimempa jina la DOZI...Slaa haangalii kama KIWETE sorry keyboard yangu haina K...na usitukane mambo kabla hujavuka mto...DR Slaa ni mbwa mwitu lazima azae na KIKWETE.
 
Lazima KIWETE sorry MS kama upo ila keyboard yangu haina K,lazima aondoke bila kuingia awamu ya pili...uleule Dr slaa,hale hale dr slaajuuu juu dr slaa...diiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii DKT KIWETE....
Note...
DR. and DKR. are two words with two different meanings.
 
Asante Mungu na wewe ndio umekuwa propaganda za ajabu baada ya kujibiwa na Kakobe sasa mnatafuta visingizio kibao. Mungu ameona Tanzania CHAGUA CHADEMA
 
Every cloud has silver lining BUT we need to vote wisely based on logic and not emotions.
 
GREAT THINKERS? AIBU!

IFUATAYO NI ORODHA YA WATU WA CHADEMA WALIOHUSIKA KWENYE UTAFITI MOJA KWA MOJA.

1. HALIMA MDEE .................................HUYU NI MJUMBE WA BODI YA TCIB

2. EDWARD KINABO............................HUYU NI MWENDESHA MAFUNZO KWA VIJANA WA CHADEMA. ENEO LAKE LA UTAFITI LILIKUWA NI ROMBO NA MOSHI MJINI.

3. ZABLON.............................................HUYU NI MSEMAJI WA DR. SLAA

4. JACKLINE MATERU..............................HUYU NI LIASON PERSON WA CHADEMA KWA WANAFUNZI WA UDSM NA MAKAMU WA RAIS WA DARUSO.

KIKAO CHA TATHMINI YA REACTION NA IMPACT KIMEFANYIKA LEO PALE JENGO JIPYA LA MAKAO MAKUU YA CHADEMA WALILONUNUA PALE KINONDONI.

WALIOHUDHURIA NI PAMOJA NA TCIB (WAFANYA UTAFITI!!!!!!!). TCIB pia ndiyo waliopewa dhima ya kuandaa midahalo mikoani. AIBU, UNAJITEKENYA MWENYEWE NA KUCHEKA!
KILA LA KHERI DK. SLAAAA!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom