Utafiti wa namna Lowassa atakavyoinufaisha UKAWA

Sasa nani wa kuongea na ACT/ zitto ili aweze kujiunga! Kwa kweli kama zitto angeweza kujiunga ukawa ni kweli ccm na makucha yake tungewang'olea mbali ila sasa tofaiti za itikadi kati ya wakubwa wawili ndiyo zinafanya ACT/UKAWA kutokua pamoja. Najua wakiwa na nia wanaweza kuungana kama lowasa kaweza kuja UKAWA, nia ikiwepo Zitto naye atajiunga na UKAWA
 
Sio hivyo kamanda mimi ni CDM damu damu ila nimetoa huo ushauri kwa sababu katika vyama vya upinzani vilivyo nje ya ukawa zito ndio ana kakundi kakubwa kidogo ka wanaompenda, inaweza kuwa hata ni laki moja chini au zaidi ya hapo nako pia katachangia ushindi wetu ukawa
 
Sio hivyo kamanda mimi ni CDM damu damu ila nimetoa huo ushauri kwa sababu katika vyama vya upinzani vilivyo nje ya ukawa zito ndio ana kakundi kakubwa kidogo ka wanaompenda, inaweza kuwa hata ni laki moja chini au zaidi ya hapo nako pia katachangia ushindi wetu ukawa
Kwa mujibu wa utafiti,ACT mwaka huu haitapata mbunge hata mmoja,haiwezi kupata madiwani zaidi ya watano,na kura za mgombea urais haziwezi kuzidi elfu 16. Hiyo laki 1 imetoka wapi?
 
Labda niseme nawaonea huruma sana sana ,walipobaki ambapo wamekamata ni kivuli cha Dr.Slaa wakiamini atazusha mtafaruku utakaosambaratisha UKAWA ,CCM wanatafuta pakutokea ukweli wamebanwa vibaya sana ,hawajui kama safari hii tunawanyoa kwa kutumia bati chakavu.

Lowasa ni kondoo aliepotea au kupotezwa ,tunasema amerejea ngamani ,na wapo wasomi wengi ambao wamepotezwa na kupotoshwa na siasa za KiCCM ,tunawaona akina Tibaijuka na wengine wengi tu walioingizwa kwenye mikenge na kupoteza fani zao.

Cha muhimi miccm haielewi kinachotaka kubadilishwa ni Chama tawala ambacho ni CCM ,bado wanajipa tamaa kuwa WaTz walio wengi wanapenda CCM ibaki madarakani na kuendelea kutesa ,tunasema kutesa sasa ni kwa zamu ,CCM lazima ikae pembeni tupande punda mwengine hata dereva akiwa yuleyule ,ila PUNDA ni lazima awe mwengine ,Punda CCM imetosha,

Punda CCM aondoke tuweke Punda mwengine ,kwa maana hiyo system nzima ya CCM itaondolewa na kuwekwa benchi ili WaTanzania waendelee katika safari ya kutafuta Punda aneweza kuwavukisha.

Sasa kama ndio Lowasa ameshakuwa muwakilishi au dereva wa Punda mpya hakuna tatizo ,punda huyu ana sera zake ana mikakati yake na WaTz walio wengi wanaendelea kumkubali Punda mpya ,hivyo basi wacha lowassa hata na wengine wakija katika kumkubali Punda huyu basi kutakuwa hakuna mjadala wala mbadala watakubalika na watakaribishwa ,hata hivyo mikakati ya Punda itabaki palepale ,kutupeleka kule kwenye Nchi inayofuata sheria na kulinda haki za binadamu ,kwa maana hiyo hata Lowasa ataweza kuja kushitakiwa kutokana na shutuma alizowahi kutuhumiwa ,inamaana Punda huyu hatakubali viongozi wawe juu ya sheria.

MiCCM karibuni UKAWA .
 
Mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi ni mwananchi fanya maamuzi sasa usiangalie mtu au chama sera na dira je inalikomboa taifa


Kapuku mimi
 
 Hii ndio report
Mnamo mwezi February mwaka huu Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA) waliingia ubia na
kampuni maarufu duniani inayojihusisha na tafiti
za siasa (Political Research) ijulikanayo kama
Greenberg Quinlan Rosner. ( Greenberg Quinlan Rosner Research ).
UKAWA walitaka kujua kama wana nafasi ya
kushinda kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kampuni hiyo ilimaliza utafiti wake mwezi May
mwaka huu na haya ndio yalikua majibu;
1. Ikiwa CCM itamsimamisha Lowassa kugombea
Urais, na UKAWA wakamsimamisha Dr.Slaa, CCM
watashinda kwa 58% dhidi ya 42% za UKAWA.
2. Ikiwa CCM itamsimamisha mgombea mwingine
asiye Lowassa kushindana na Dr.Slaa, CCM
itashinda kwa 54% dhidi ya 46% za UKAWA.
3. Ikiwa UKAWA itamsimamisha mgombea
mwingine ambaye si Dr.Slaa na CCM
ikamsimamisha Lowassa, CCM itashinda kwa 68%
dhidi ya 32% za UKAWA.
4. Ikiwa UKAWA itamsimamisha mtu mwingine
ambaye sio Dr.Slaa na CCM ikamsimamisha mtu
mwingine ambaye sio Lowassa CCM itashinda
kwa 57% dhidi ya 43% UKAWA.
5. Ikiwa watu wote wa CCM wanaotaka Urais
wakiwekwa Pamoja na wa UKAWA wakawekwa
pamoja kisha wapigiwe kura za Urais kama
wagombea huru, Lowassa ataongoza kwa 14%
kisha Dr.Slaa atafuata kwa 09%, Membe 04% na
wengine chini ya hapo.
6. Ikiwa Lowassa atagombea kupitia UKAWA
atapunguza kura za UKAWA kwa 06% lakini
ataziongeza kwa 24%. Hii ina maana kuwa katika
watu 100 wa CHADEMA watu 6 hawataipigia kura
CHADEMA kwa sababu hawamtaki Lowassa.
Lakini Lowassa ataleta watu wapya 24. Yani
CHADEMA itapoteza kura 6 za wanachama wake
lakini itapata kura mpya 24 mpya.
DATA ANALYSIS
Ukisoma vzr huo utafiti hapo juu utagundua kuwa
Lowassa anaongeza umaarufu wa CCM kwa 18%.
Kwa hiyo kuondoka kwa Lowassa kutaipunguzia
nguvu CCM kwa 18%.
Sasa ikiwa CCM yenye Lowassa ina nguvu 58% na
UKAWA yenye Dr.Slaa ina nguvu 42%, maana
yake ni kwamba kumuondoa Lowassa CCM ni
kupunguza nguvu yao kwa 18% yani (58-18) =
40%.
Na kumleta Lowassa UKAWA ni kupunguza nguvu
ya UKAWA kwa 6% lakini kuongeza kwa 24%. Kwa
hiyo chukua 42 toa 06 kisha jumlisha 24 utapata
60%.
Sasa jumlisha 40% za CCM na 60% za UKAWA
kama haiji 100%??
Kwa hiyo UKAWA yenye Lowassa inashinda
uchaguzi kwa nguvu kubwa zaidi kuliko ambavyo
CCM ingeshinda ikiwa na Lowassa. Na hii ni kwa
sababu ujio wa Lowassa utaivunja CCM vipande
vipande.
Na ili uweze kuishinda CCM lazima uivunje
vipande kwanza. Huwezi kuishinda CCM ikiwa
imesimama imara.
Nchini Kenya KANU ilishindwa kirahisi baada ya
kuvunjwa vipande, Zambia UNIP ilishindwa baada
ya kuvunjwa vipande, na nchi nyingine za Afrika
vivyo hivyo.
Na njia rahisi ya kukivunja chama tawala ni kwa
kuondoa watu wenye ushawishi ktk chama hicho.
Fredrick Chiluba alikua mtu mwenye ushawishi
mkubwa akiwa UNIP lakini alipoondoka kwenda
MMD huo ndio ukawa mwisho wa UNIP maana
alikua na ushawishi na aliondoka na kundi kubwa
la watu.
Nchini Kenya akina Najib Balala, George Saitoti,
Musalia Mudavadi, Raila Odinga, Mwai Kibaki etc
walikua watu wenye ushawishi sana ndani ya
KANU. Lakini walipoondoka kwenda NARC hiyo
ndio ikawa mauti ya KANU.
Hii ni kwa sababu watu hawa walipoondoka,
waliondoka na kundi kubwa la wafuasi. Hivyo basi
hata Lowassa atasaidia kuivunja CCM na
hatimaye kuiwezesha UKAWA kushinda kirahisi.
Ikumbukwe Nyerere aliwahi kusema huwezi
kuishinda CCM imara yenye umoja. Kwa hiyo njia
rahisi ya kuishinda CCM ni kuivunja vunja
vipande. Na tayari kazi hiyo imeanza rasmi.
BAADA YA UTAFITI.
Baada ya ripoti ya utafiti huo wa GNR mnamo
mwezi May, UKAWA walikaa na kutafuta njia ya
kufanya. Walijua wazi CCM ikimpitisha Lowassa
UKAWA itaangushwa hata imsimamishe nani. Na
laiti CCM wangeona ripoti ya utafiti huo
wasingefanya kosa la kumkata Lowassa.
Wangempitisha ili waishinde UKAWA kirahisi.
Kwa hiyo UKAWA walikua wanafuatilia sana
mchakato wa CCM huku wakiomba usiku na
mchana wasimpitishe Lowassa. Na kweli Mungu
akajibu maombi yao.
Lakini UKAWA wakatafakari ikiwa
watamsimamisha Dr.Slaa kushindana na Magufuli
bado UKAWA itashindwa kwa kupata 46% dhidi ya
54% za CCM kama utafiti unavyoonesha.
Kwa hiyo ili kuishinda CCM ni kufanya nini? Ili
kuishinda CCM ni kumshawishi Lowassa ajiunge
na chama kimojawapo kinachounda xm ili apewe
nafasi ya kugombea na kuiwezesha UKAWA
kushinda. Na ndivyo ilivyotokea.
Kwa hiyo kwa mujibu wa utafiti huo UKAWA
itashinda kwa 60% na CCM 40% kwenye uchaguzi
mkuu wa mwaka huu.
 
Huo utafiti uko vizuri.. Lakini kuna mamluki wa ccm humu watajifanya kuvuka barabara huku wamefumba macho.. #tukutane october, tunachukua dora asubuhi na mapema.
 
Huo utafiti uko vizuri.. Lakini kuna mamluki wa ccm humu watajifanya kuvuka barabara huku wamefumba macho.. #tukutane october, tunachukua dora asubuhi na mapema.
 
Mimi nnaona Lowasa kainunuwa chadema.
Mimi nionavyo kulingana na Utafiti wa kitaalmu hapo juu ni kwamba EL, amekodishwa na CHADEMA ili kufanikisha kutimiza ndoto ya Mabadiliko ya vyama vyote vya UKAWA,
...isipokua EL ameinunua FISiEMu toka long time sana hadi jengo lake URT inalitegemea kama OFisi ya Ubalozi huko Kwa MAdiba, manake kutoka kwake tu CCM na kuacha kuwekeza, naona Chama sasa hivi kina ha ha ile mbaya kusimama pamoja ili kumuuza Makufuli kwa wananchi. N
a hapo Bado EL hajachukua wafanyakazi wake Woote Wapatao wabunge zaidi ya 205 na wakuu wa mikoa 18, na maafisa kadhaa.Trust Me.. Akiwachukua CCM haitabaki vilevile. Tena hata Mkulu amshukuru sana MZee EL, manake kama sio yeye angeusikia Umagogoni kwenye BOmba.
 
All in all Mbowe hawezi kuwa amempokea EL bila consideration (especially in monetary terms), na kama EL akishindwa Mbowe hana cha kupoteza kwa sababu bado chama kitapata ruzuku na yeye ataendelea kuwa mwenyekiti.

Mbowe hawezi kuwa mjinga kuanza kumsafisha Lowassa tu bure bure, hivi vyama ni miradi ya watu, watu wameweka hela zao kuvianzisha, wamefanikiwa kuset up succession plan nzuri kiasi kwamba in more than 20 years bado chama kiko mikononi mwa familia ya mwanzilishi na faida imeanza kupatikana.

Chama hakina sera tena, isipokuwa sera iliyobaki ni kuitoa CCM madarakani wakale wao.

Nionavyo mimi, Afrika tuna matatizo yanayofanana, viongozi wote upinzani na tawala njaa zinatangulizwa mbele badala ya maslahi ya taifa. Bado sana uhuru.
 
All in all Mbowe hawezi kuwa amempokea EL bila consideration (especially in monetary terms), na kama EL akishindwa Mbowe hana cha kupoteza kwa sababu bado chama kitapata ruzuku na yeye ataendelea kuwa mwenyekiti.

Mbowe hawezi kuwa mjinga kuanza kumsafisha Lowassa tu bure bure, hivi vyama ni miradi ya watu, watu wameweka hela zao kuvianzisha, wamefanikiwa kuset up succession plan nzuri kiasi kwamba in more than 20 years bado chama kiko mikononi mwa familia ya mwanzilishi na faida imeanza kupatikana.

Chama hakina sera tena, isipokuwa sera iliyobaki ni kuitoa CCM madarakani wakale wao.

Nionavyo mimi, Afrika tuna matatizo yanayofanana, viongozi wote upinzani na tawala njaa zinatangulizwa mbele badala ya maslahi ya taifa. Bado sana uhuru.

wewe wasemaaa
 
Back
Top Bottom