Utafiti uliomponza SLAA 2010

Kuna ukweli ambao yeyote hata kama si mpenzi wa CDM kama mimi ninakiri kuwa slaa alikuwa mbunge mahili sana na aliweza kutoa michango hai bungeni pamoja na kujenga hoja katika lile jumba la kifahari "BIG BROTHER", lakini watu wengi wamekuwa wakihoji ni kipi kilichompelekea Dr. Yule aliyeruka toka diploma hadi Phd kugombea urais, Leo nitawaeleza siri kubwa ambayo ndio motive behind slaa kugombea.
Inasemekana CDM haikuwa na mpango wa kumsimamisha mgombea wa urais mwaka 2010, katika kikao chake kilichofanyika arusha baadhi ya viongozi walimpendekeza mboye ambaye alikataa, lakini pia wapo wajumbe walioshauri kuelekeza nguvu katika ubunge, udiwani na kukijenga chama zaidi, hoja hii ya pili ilipata nguvu sana na ndio lilikuwa azimio lisilo rasmi katika kikao kile.


Slaa alipatikanaje?
Inasemekana alishauriwa na baadhi ya wasisi wa CDM na pia katika kundi hilo walikuwepo viongozi wa "Watakatifu", inasemekana Dr. hakushawishika na ushauri huo na aliomba ifanyike tathmin sahihi na aelezwe option zote ikiwemo nini atapata in return kama atakosa urais. Katika tathmini na upembuzi wao wataalamu wakaja na mambo yafuatayo


  1. Bila kujua kuwa walikuwa wanatumia daftari la kudumu la wapiga kura la zamani, hesabu za watu kwa kutumia majina yao(Sijui kwa nini walitumia majina), zilionyesha slaa anaweza kupata 52% ya kura zote kama mikakati itafanikiwa
  2. In case atakosa uongozi, atalipwa malipo yake yote kama alivyokuwa akipata akiwa mbunge (yaani 7.5 Milions)
  3. "Watakatifu" waliahidi full support kwa kutumia nafasi zao walizopewa ili slaa awe chaguo la mungu baada ya JK
Mapendekezo yalikuwa mengi ila hayo ni yale makubwa na baada ya mapendekezo hayo, ndio Dr. alipokubali kuyavulia nguo maji,


Udhaifu wa mapendekezo:
Kwa hakika lile lilikuwa kosa kubwa sana, moja ni kwasababu wengi wa watanzania hawapigi kura na huwezi kutegemea ushindi kwa watu hao, lakini baada ya mwezi mmoja kupita, TUME HURU YA UCHAGUZI ikatoa updated daftari la kudumu la wapiga kura likiwa na idadi kubwa zaid ya ile ya awali , kama mnakumbuka ilizusha malalamiko mkubwa na lilikuwa pigo la kwanza kwa CDM kwa kuwa kwa hesabu zilezile za majina lilipelekea mgombea wa CDM kuwa down.

Mwisho namshauri slaa next time 2015, agombee ubunge tena kwa kuwa tumeliona pengo lako bungeni na usipoteze tena muda wako na kugombea urais kwa kuwa ilikuwa kosa la kihistoria.

Asanteni
Trojan Downloader

Nafikiri watafiti bado wanahangaika kupata aina ya magonjwa mapya.
 
Back
Top Bottom