Hapa nitangulie kusema kwamba, binafsi nimeuelewa sana utafiti uliofanywa na Maprofesa wa Idara ya Sosholojia ya Chuo Kikuu cha Chicago!
Kwa ufupi utafiti huo unasema kwamba uhusiano unaoanzia mtandaoni huenda ukawa ndio bora zaidi kulinganisha na ule wa kawaida!!! Hoja yao ni kwamba, Online Dating inatoa uwanda mpana zaidi wa kuchagua mwenza sahihi kuliko uhusiano unaotokana na njia za asili!
Wanachojaribu kutuambia hapa ni kwamba, ingekuwa mtu anatafuta gari apendalo basi online dating ni sawa na kuingia kwenye mtandao wa nyumbani (local website) unaouza magari huku mtandao huo ukiwa ume-upload magari ya aina na sifa mbalimbali. Hapo mteja anapata fursa ya kuchagua gari apendalo kwa umakini zaidi kutoka kwenye maelefu ya magari yaliyokuwa uploaded kabla hajatembelea yard iliyohifadhi magari hayo na kuchunguza kwa ukaribu zaidi gari alilolipenda mtandaoni hapo kabla!
Kinyume chake, uhusiano kwa njia za asili ni sawa na mtu anayesimama barabarani au kituo cha magari kama vile Ubungo Terminal huku akijaribu kuchagua gari apendalo kutoka kwenye magari kadhaa yaliyo kwenye mwendo au yaliyoegeshwa kabla hajaenda yard kuchunguza gari husika kwa umakini zaidi!!
Je, ni nani miongoni mwa hao ana uwezekano wa kupata gari bora zaidi? Yule ambae kabla hajaenda Yard amelichunguza umakini gari husika mtandaoni au yule aliyetega barabarani?
Aidha, utafiti huo unaendelea kusema kwamba 7.6% ya ndoa za wanandoa waliokutana kwa njia za kawaida zilivunjika ukilinganisha na 6% ya ndoa zilizovunjika kwa wanandoa waliokutana mtandaoni! Kwa maana nyingine, Watafiti hawa wanatuambia risk ya kuvunjika ndoa za wale waliokutana kwa njia za kawaida ni kubwa zaidi ukilinganisha na wale waliokutana mtandaoni!
Unakubali au unakataa?! Kwanini unakubali au kwanini unakataa?
Kuisoma makala hii kwa urefu: Tujadiliane: Je, unadhani mapenzi ya kukutana mtandaoni ni salama kiasi gani?