Utafiti Tanzania: Mimba milioni moja zisizotarajiwa utungwa kwa mwaka, 39% huharibiwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Licha ya sheria kukataza utoaji mimba, vitendo hivyo hufanyika na mara nyingi kwa njia zisizo salama. Pamoja na kwamba takwimu zinaonesha tatizo la vifo vya uzazi linapungua, bado kuna baadhi ya mambo yanachangia liendelee kuwepo ikiwemo suala la utoaji mimba usio salama ambao unachangia tatizo hilo kwa asilimia 13.

Akizungumzia zaidi Daktari Bingwa katika Masuala ya Afya ya Mama na Mtoto, Dkt.Peter Kibacha anasema kuna sababu nyingi zinazochangia vifo vya uzazi kama utokwaji damu usio wa kawaida, tatizo linalochangia kwa asilimia 24, kifafa cha mimba asilimia 12 na utoaji mimba au uviaji asilimia 13.

Anasema kuwa kuna mimba milioni 20 zisizotarajiwa hutolewa kwa njia isiyo salama duniani hususani katika nchi zisizoendelea kila mwaka hili ni tatizo kubwa.

Watafiti waligundua kwamba utoaji mimba kwa siri hutokea mara nyingi na huchangia kwa kiasi kikubwa kwenye vifo na kuumia kwa wajawazito.

Utafiti huo, uliofanywa na watafiti kutoka Taasisi ya Guttmacher ya Marekani, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili zilizoko hapa Tanzania.

Dkt.Kibacha, pia alielezea ukubwa wa tatizo hilo nchini kuwa kila mwaka kuna mimba milioni moja zisizotarajiwa na kati yake asilimia 39 huharibiwa.

Anasema kwa mujibu wa takwimu zilizopo, takribani asilimia 50 ya mimba zisizotarajiwa hutolewa katika njia isiyo salama.

Alielezea madhara ya tatizo hilo kwa wasichana na wanawake kuwa ni kupata maumivu makali, mlango wa uzazi kushindwa kuhimili na mimba kuharibika, kuharibu kizazi na mimba kutunga nje ya kizazi.

Daktari huyo, alielezea namna ya kukabiliana na tatizo hilo nchini kuwa ni waandishi wa habari kusaidia serikali na asasi ziziso za kiserikali (NGOs), ili kupunguza tatizo ni wakati sasa wa kutolewa elimu kwa jamii kuhusu tatizo hilo na namna ya kukabiliana nalo, kudhibiti ukatili wa ngono, matumizi ya uzazi wa mpango, kuepusha vishawishi kwa wasichana na kudhibiti ukatili wa ngono.

Mwanasheria Julius Titus, anasema kuwa ipo haja ya kuchanganua sheria zilizowekwa nchini zinazohusiana na mfumo wa udhibiti wa haki ya afya ya uzazi ikiwemo sheria ya Makosa ya Jinai inayotoa adhabu kali kwa wale wote wanaojihusisha na utoaji mimba usio salama.

"Ni kweli sheria hii inatambua kuwa mtu anaweza kutolea mimba endapo itahitajika kunusuru maisha yake, lakini pia inadhibiti utoaji mimba usio salama kwa kutoa adhabu kali ikiwemo kifungo cha miaka minne kwa mtoa huduma za afya atakayemtoa mtu mimba na anayetolewa mimba kifungo cha miaka saba," anasema.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Afya, matokeo ya Utafiti wa Hali ya Afya na Watu (TDHS) yaliyotolewa mwaka 2015/2016 yalionesha kuwa vifo vitokanavyo na uzazi nchini ni 556 kwa kila vizazi hai 100,000.

Kwa mujibu wa tafiti hizo, zaidi ya asilimia 90 ya wasichana walio katika uhusiano na zaidi ya mwanaume mmoja, ndio wanaongoza kwa kutoa mimba na wachache sana ndio hukubaliana na hali inayoweza kuwatokea kutokana na uhusiano huo na kuamua kuzaa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanyvwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya wanawake milioni 21.6 duniani kote walio katika umri wa miaka 15 hadi 44 hutoa mimba kwa njia za vichochoroni kila mwaka na kwamba, tatizo ni kubwa zaidi katika nchi zinazoendelea.


Chanzo: Majira
 
Back
Top Bottom