Utafiti: Nusu ya wanaume nchini wagumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafiti: Nusu ya wanaume nchini wagumba

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by sumasuma, Feb 8, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Florence Majani
  UTAFTI mpya umebaini kuwa nusu ya wanaume nchini ni wagumba ukipingana madai ya wengi kuwa tatizo hilo linawaathiri zaidi wanawake.Kwa mujibu wa utafiti huo, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili kati ya mwaka 2009 na Septemba 2010 unaonyesha, asilimia 47.05 ya wanaume wanaokwenda kupima afya zao za uzazi, hawana uwezo wa kutungisha mimba.Malengo ya utafiti huo uliosimamiwa na Dk Henry Mwakyoma, yalikuwa ni kubaini ni kwa kiasi gani wanaume huweza kuathiriwa katika via vyao vya uzazi na hatimaye kushindwa kutungisha mimba.

  Utafiti huo ulionyesha kati ya wanaume 221 waliopimwa, asilimia 30.03 walikuwa na mbegu dhaifu na asilimia 17.02 walikuwa hawana kabisa mbegu zenye uwezo wa kutungisha mimba, zaidi ya maji tu.
  Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Dk Mwakyoma alisema, ugumba kwa wanaume limekuwa tatizo sugu katika miaka ya hivi karibuni.

  “Nasisitiza kuwa, pengine mwanaume aliwahi kupata watoto hapo awali, lakini sasa hivi hapati, bado atakuwa mgumba,” alisema Dk Mwakyoma.Alisema hapo awali ilikuwa vigumu kupata idadi kamili ya wanaume wenye ugumba kwa sababu walikuwa hawajitokezi kupima.“Angalau sasa hivi wanakuja na tunawapima, ingawa ni kazi ngumu kuwapa majibu yao,” alisema Mwakyoma.

  Sababu za ugumba
  Mwakyoma alitaja sababu za ugumba kwa wanaume kuwa ni uambukizo katika tezi inayozalisha manii.
  Alitaja sababu nyingine kuwa ni kemikali zinazoingia katika miili yetu, mionzi na wakati mwingine ajali inapoathiri tezi hiyo.

  Dk Mwakyoma aliongeza kuwa, wanaoathirika zaidi ni wanaofanya kazi migodini, jeshini au wanaozungukwa na kemikali kwa muda mrefu.“Sababu nyingine ni joto kuzidi katika sehemu za siri za mwanaume, kubeba laptop, unene kupita kiasi na mazingira,” alisema.

  Dk Mwakyoma akifafanua jinsi kitengo chake kinavyopima manii ili kujua kama zina matatizo au zipo salama, alisema, " rangi ya mbegu pamoja na umbile huangaliwa ili kutambua ubora wake. Hata kwa kuziangalia tu, mbegu zenye rangi aidha kijivu au nyeupe si salama.”

  Kwa upande wake, Dk Innocent Mosha, ambaye ni daktari wa uchunguzi wa magonjwa katika Hospitali ya Muhimbili alisema, wamefanikiwa kupata takwimu hizo kutokana na wanandoa wengi kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kujua sababu ya kutokuwa na watoto katika ndoa yao."Mara nyingi matokeo huonyesha tatizo liko kwa mwanaume. Lakini kuna tabu ya kuwaeleza ukweli, wengi hawataki kukubali," alisema Dk Mosha.

  Aliongeza, “Kesi kama hizo huleta migogoro ya kifamilia, kwani huenda mwanamke huyo amekwishamzalia mumewe watoto ambao kimantiki si wa kwake,” alisema Dk Mosha.

  Dk Mosha alisema, kuna ugumba wa aina mbili; wa kuzawa nao na ugumba unaopatikana ukubwani.
  “Wapo wanaozaliwa na ugumba, yaani mbegu zao aidha ni dhaifu au hawana kabisa mbegu tangu kuzaliwa kwao,” alisema Dk Mosha.

  Shirika la Afya duniani (WHO) linathibitisha kuwa, ujazo wa manii anaopaswa kuwa nao mwanaume ili aweze kutungisha mimba ni milligram moja na nusu hadi nne na nusu na kuongeza, “Ujazo wa manii ukipungua au ukizidi basi mbegu hizo zina matatizo” alisema Dk Mwakyoma.

  Naye Dk Joshua Noreh wa kituo cha upandikizaji cha jijini Nairobi (IVF centre) alisema, tatizo la ugumba alianza kuliona tangu mwaka 2006 baada ya kupokea wanandoa wengi kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania waliofika kutafuta huduma ya upandikizaji wa mbegu ili kupata watoto.

  Utafiti uliofanywa na WHO mwaka 2009 duniani, ulibainisha kuwa, mwanaume mmoja kati ya saba wanaofika kupima afya ya uzazi hugundulika na matatizo ya ugumba.

   
 2. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mmmmmmmhhhhhh,
  ........sisi ndo wanaume bana....Aspirin,njoo umwage hoja hapa ueleze kisa na mkasa.
   
 3. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,093
  Likes Received: 10,449
  Trophy Points: 280
  du! kazi ipo.
   
 4. Typhoid

  Typhoid JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heheh uzuri nina mtoto sina wasiwasi! Kazi kwako usie na mwana! Nafanana na mwanangu utafikili mdogo wangu hivo najiamini!
   
 5. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Ni habari nzuri kubadilishamtazamo wa jamii kuwa wanawake ndio wagumba. lakini we should interprete these findings with caution until we clear doubts in the sampling scheme. kama watu walikuja wakiwa wanajishuku wana matatizo ya uzazi, then matokeo hayo huwezi kuyageneralise kwa entire population. Pia kama ulisample vulnerable groups kama aliyoyataja-wanamigodi, wanaozungukwa na chemicals etc then na hiyo inaleta mashaka kufanya population generalisation. Anyway it is a good start to change community perception on infertility being a female issue!!!
   
 6. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mh hapa tulipofikia sio pazuri kabisa kama hali yenyewe hii...laptop 24/5 ipo mapajani
   
 7. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  hahaha........na wengi hawatak kukubali hali hii...
   
 8. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  UMEJUAJE?Kufanana si hoja, hujaonaga mke na mume wanafanana?
   
 9. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,070
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 180
  laptop mapajani 24/5. hahahaaa..
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nna mashaka sana na credibility ya 'utafiti' huo kama ulifanywa na madr hawahawa wanaogoma na kupasua watu vichwa badala ya miguu.
   
 11. K

  KVM JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Aliyeandika makala hii amekosa uwezo kupambanua matokeo ya utafiti uliofanywa. Matokeo yanasema nusu ya wanaume wanaume wanaokwenda kupima afya zao za uzazi, hawana uwezo wa kutungisha mimba. Nusu hiyo inawahusu wale waliokwenda kupima wakijihisi wakiwa na tatizo hilo na siyo Watanzania wote.
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,221
  Trophy Points: 280
  acha maskhara wewe
   
 13. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  isije ikawa dogo lako ndo limefanya kweli..
   
 14. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kazi kweli kweli mambo si mambo,white collar job gani isiyo na laptop?nafkiriaakuenda kulima kuliko kazi hizi.
   
 15. M

  Marytina JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hasa wa DSM
   
 16. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Sitaki kukataa kwamba tatizo hakuna lakini huu utafiti na generalization (wa)aliyofanya (sijui ni mwandishi au ndo daktari mwenyewe) sio sawa. Watafiti wengi wanakubali kuwa sample yenye angalau 1/3 ya population nzima inaweza kutosheleza na kuwa na uwezo wa kuwakilisha. Sasa hii sampo yao ya wanaume 221 kwa nchi hii nzima ya TZA na inawezekana wote wametoka hapo Dar, inasema nini hapa?

  Wanawezaje kufanya generalization kwa kutumia sample ndogo kiasi hicho? It is almost ineligible!
   
 17. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wengi wa wanaume wanapenda TIGO na majibu ya kupenda hiyo kitu ndo hayo ....
   
 18. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wanaume kuwa wagumba inatisha eeh! Kwa kuwa ni wanaume mpaka tujihakikishia methodological and population sample studied. Kazi kweli kweli, sasa kilichotufanya tuamini wanawake ni wagumba zaidi ya wanaume ni swala gani zaidi haswa?

  Kwa sasa utafiti huu unakua mgumu kutafsiri kwa sababu hatujui kama kunaongezeko ama laa. Faida, ya utafiti huu zaidi ni kuondoa dhana ya ugumba ni kwa mwanamke zaidi. Mambo yanabadilika pia katika jamii japo kidogo. Miezi 8 iliyopita jamaa yangu alienda hospitali na mkewe kupima baada ya kukaa kwenye ndoa miaka 5 bila mtoto. Mume alibisha sana mara ya kwanza, lakini baada ya kwenda, kushauriwa na kufanyiwa tiba mke leo ni mjamzito wa miezi 3.

  Dhana hizi zikiondoka matatizo ya ugumba yanaweza kupungua kiasi chake.
   
 19. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ubabaishaji tu
   
 20. Mghoshingwa

  Mghoshingwa JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  ugumba ,dah.
   
Loading...