Utafiti: Mnyika kurudi bungeni ni 100%

Utafiti: Mnyika kurudi bungeni ni 100%

Kumbe we umekuja juzi tu hapa! ah! tunabishana na wakuja tu, we humjui hata mzee Mfuga mbwa wa tip top, hupajui hata kwa mkata kimeo, we pale kwe daraja la manzese hujui kama ndio msufini, huwajui hata waimba mnanda wa mwanzo Hisani gari kubwa, kifupi hujui hata biti kaenga mwenyewe wa Mburahati alikuwa anakaa wapi, Jimbo la Ubungo limeharibiwa na siasa za kitoto za huyo dogo, sidhani kama atarudi mjengoni labda kwa kuteuliwa.

Wewe siasa zako za kiutu uzima ni zipi?
 
Mnyika hata siku moja hawezi kushinda uchaguzi. Hapa Ubungo hakina maji miaka yote. Barabara zote ni mbaya mfano barabara ya kwenda Kibangu. Mnaotaka kujifurahisha mjifurahishe na topic zenu mitandaoni.

Hao waliokuwa wabunge Wa ubungo toka Uhuru waliwajengeen barabara ?acha kufikiri kwa kutumia ma.ka.li.o
 
Kwahiyo mnabana ili ashindwe kutimza ahadi mseme ameshindwa? By the way nimekuwa nasikiawatu mitaani huk kimara wakisem CCM wana roho mbaya sana wanatunyim maji ksa tumechagua upinzani serikali za mitaa. Kwa hiyo muwe macho watu ni waelewa siku hizi. Mnategemea mtese watu kwa sababu wametimiza uhuru wao kidemokrasia halafu muende kuwaambia eti Mnyika ameshindwa. Hamtafulu! Watu wana hasira snana nyie washenzi!

Maccm ni mamtu ya ajabu sana.yanabana upatkanaji Wa Huduma ktk majimbo yaliyo chini ya upinzani.cha ajabu yakipata kuongoza majimbo hayo,Huduma hayaleti pia.sijui yamelogwa.

Ktk majimbo ya dar yanayozungumzwa zaid ni ubungo.vp kuhusu ilala kinondoni segerea kigambon ambayo yako chini ya ccm?yana hali mbaya sana na wabunge wao ni mizigo.ktk Tanzania,mbunge anaefahamika na watanzania kutoka majimbo ya dar,ni JJ mnyika.kijana anauwezo mkubwa sana kusimamia Maendeleo na Huduma kwa wananchi wake.
 
Kama ubungo hawamtaki watuletee ukonga huku hatuna mbunge tunahitaji mbunge kama Mnyika aje atuokoe
 
Bora nikose mshahara kwa miaka mitano kuliko kuvumilia kuongozwa na gamba Ubungo
 
Nimekaa ubungo miaka kumi sasa namkubali sana huyu kamanda Mnyika. Maji yakikatika tunaenda kudai akiwa mstari wa mbele na dawasco wananywea maji wanatoa. Chezea Mnyika wewe
Siasa, yaani maji yanakatika mnaandamana na mbunge maji yanatoka! Siku nyingine yakikatika mcharazeni bakora tuone itakuwaje. Punguzenu maandamano.
 
Wananchi wa Kimara Temboni, Bonyokwa, Suka,wanataka maji na barabara siyo muongozo spika bungeni.
Kazi ya mbunge ni kujenga barabara?

Na kazi ya meya na Halmashauri yake ni nini?

Kazi ya mbunge ni kuwakilisha interests za wapiga kura wake bungeni, na kuchangia uboreshaji wa miswada ya sheria inapoletwa bungeni. Kazi hizi Mnyika amezifanya kuliko mbunge mwingine yeyote.

Lakini najua tatizo lako, kama mbunge si wa imani yako huwezi kumkubali. Nasikia Zitto eti alikuwa anatoa hoja bungeni, lakini Mnyika akitoa eti si kazi ya mbunge. Double standards at its best!!!
 
Kazi ya mbunge ni kujenga barabara?

Na kazi ya meya na Halmashauri yake ni nini?

Kazi ya mbunge ni kuwakilisha interests za wapiga kura wake bungeni, na kuchangia uboreshaji wa miswada ya sheria inapoletwa bungeni. Kazi hizi Mnyika amezifanya kuliko mbunge mwingine yeyote.

Lakini najua tatizo lako, kama mbunge si wa imani yako huwezi kumkubali. Nasikia Zitto eti alikuwa anatoa hoja bungeni, lakini Mnyika akitoa eti si kazi ya mbunge. Double standards at its best!!!
Kumbe hizi ndiyo kazi za mbunge sasa ilikuaje Mnyika atoe ahadi au ndiyo utapeli wa kisiasa.

Mkuu labda wewe mbunge tofauti na imani yako ndiyo haumkubali mimi sipo hivyo mbona namkubali sana Kafulila A.K.A Sisimizi A.K.A Tumbiri.
 
Siasa, yaani maji yanakatika mnaandamana na mbunge maji yanatoka! Siku nyingine yakikatika mcharazeni bakora tuone itakuwaje. Punguzenu maandamano.
Soma katiba ya Jamhuri ya Muungani Ibara ya 20. Katiba hii ambayo ni sheria mama, inasema maandamano ni haki ya msingi ya kila raia.

Maandamano si uhalifu, na sheria yoyote inayoyakataza inavunja katiba, ni sheria ya kidikteta.

Pia
Sheria Na. 64 ya 1961 kifungu cha 5; 3 cha 1995

(1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara , kwa muda usiopungua saa
48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:-
(a) sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;
(b) dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na
(c) maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa mara kwenye gazeti la Serikali, kuainisha.
 
kwa mnyika jamani tuweke unafiki pembeni kazi yake imeonekana na kama kuna sehemu kashidwa si kwa sababu ya uzembe wake bali mfumo uliopo ndo tatizo ila kwa mamlaka ya mmbunge kwa kweli mnyika amefanya vizuri

kwa kazi gani ya maana aliyofanya mnyika labda kazi za chadema lkn si za wana ubungo, wakaulize wakazi wa , ubungo makoka, mpaka kirungule nenda mpa baruti hatutaki hata kumsikia. tunajutia kura zetu kwake, yupo bize na miongozo amabyo haitusaidii wana ubungo kabisa.
 
Siasa, yaani maji yanakatika mnaandamana na mbunge maji yanatoka! Siku nyingine yakikatika mcharazeni bakora tuone itakuwaje. Punguzenu maandamano.
Soma katiba ya Jamhuri ya Muungani Ibara ya 20. Katiba hii ambayo ni sheria mama, inasema maandamano ni haki ya msingi ya kila raia.

Maandamano si uhalifu, na sheria yoyote inayoyakataza inavunja katiba, ni sheria ya kidikteta.

Pia
Sheria Na. 64 ya 1961 kifungu cha 5; 3 cha 1995

(1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara , kwa muda usiopungua saa
48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:-
(a) sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;
(b) dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na
(c) maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa mara kwenye gazeti la Serikali, kuainisha.
 
Kumbe hizi ndiyo kazi za mbunge sasa ilikuaje Mnyika atoe ahadi au ndiyo utapeli wa kisiasa.

Mkuu labda wewe mbunge tofauti na imani yako ndiyo haumkubali mimi sipo hivyo mbona namkubali sana Kafulila A.K.A Sisimizi A.K.A Tumbiri.
Mnyika hakutoa ahadi ya kuanza mradi mpya wa maji. Mnyika alitoa ahadi ya kufuatilia kukamilisha miradi ya maji. Ndivyo wabunge wote wanavyofanya.

Mnyika amefuatilia sana na rekodi zipo. Mnyika alipeleka hata hoja binafsi bungeni ya kuangalia hatua za dharura za kutatua tatizo la maji. Aliyekwamisha tunamjua, si Mnyika.

Tunajua ubaguzi wako, na roho ya chuki kwa wasio waislamu, na tutakuwa tunakumbusha hili kila mara.

Barua ya Mwisho ya Mnyika kwa JK

Mheshimiwa Rais,

Ikulu

Dar Es Salaam


Shikamoo!. Nimelazimika kukuandikia moja kwa moja kutokana na udhaifu wa Ofisi yako kutokujibu barua ya wazi (nakala imeambatanishwa) niliyowaandikia tarehe 16 Aprili 2014 . Barua hiyo, suala tajwa hapo juu lahusika, niliomba ionwe na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu Ofisi ya Rais kwa niaba yako.


Kwa unyenyekevu kupitia ujumbe huu nakukumbusha uitishe kikao tajwa kabla ya kumalizika kwa mwaka 2014. Hii ni kwa kuzingatia haja ya wananchi ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi katika Jiji la Dar Es Salaam na ahadi yako kwamba kikao hicho ungekiitisha Machi 2013.

Mwaka mmoja na miezi saba imepita bila ahadi yako kutekelezwa hali ambayo ikiendelea itabidi nichukue hatua za ziada za kibunge na za kuunganisha umma kutumia mamlaka yao.


Wako katika uwakilishi wa wananchi,


John Mnyika (Mb)

16 Disemba 2014
 
Kazi ya mbunge ni kuifuatilia serikali kutimiza majukumu yake kwa wananchi. Mnyika amefanya hili vema sana.

Tatizo la maji Mnyika alitoa hoja hii, serikali ndio iliyoshindwa.

Kumb: OMU/MJ/19/01 17/01/2015

Spika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi Ndogo Dar Es Salaam:
Mheshimiwa,

YAH: KUFUATILIA UDHAIFU WA UTEKELEZAJI/UTENDAJI WA WIZARA YA MAJI, DAWASA, DAWASCO NA EWURA KUHUSU HATUA ZA HARAKA ZA KUBORESHA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI NA USHUGHULIKIAJI WA MAJI TAKA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM.

Utakumbuka kwamba tarehe 4 Februari 2013 niliwasilisha Hoja Binafsi ya kutaka hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar Es Salaam.

Baada ya kuwasilisha hoja hiyo Waziri wa Maji badala ya kuchangia kwa kujibu hoja kama kanuni ya 53 (6) (c) aliwasilisha hoja tofauti kwa kutumia kanuni ya 57 (1) (c) ya kuiondoa hoja yangu isiendelee kujadiliwa kwa maelezo kwamba "tayari kuna mpango maalum uliotengewa fedha nyingi na Serikali ya CCM na kwa kuzingatia kuwa utekelezaji wa mpango huo unaendelea vizuri sana".

Waziri alikiuka kanuni za Bunge kwa kuwasilisha hoja hiyo kwa kuwa kanuni ya 57 (4) badiliko hilo lilikuwa linapingana na hoja kwa kuwa linaiondoa hoja yenyewe na kanuni ya 58 (5) ambayo inaelekeza kwamba hoja ikishawasilishwa anayeweza kuondoa hoja ni mtoa hoja mwenyewe tu tena kwa idhini ya Bunge.

Aidha, Waziri wa Maji alitoa maelezo yenye kulidanganya bunge, kujenga matumaini hewa fedha za kutosha zimetengwa na utekelezaji unakwenda vizuri sana. Hiyo ilikuwa kinyume kabisa na maelezo yake mwenyewe bungeni tarehe 10 Julai 2012, 7 Novemba 2012 na nyaraka nilizonazo za ndani ya Serikali za Januari 2013.

Pia, Waziri wa Maji hakutoa maelezo kuhusu mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha (Dar es salaam Water Supply and Sanitation Project-DWSSP) uliotumia dola milioni 164.6 hata hivyo mpaka sasa katika maeneo mengi mtandao wake maarufu kama mabomba ya Wachina, hautoi maji huku kukiwa na upungufu katika uzalishaji, upotevu wakati wa usafirishaji, udhaifu katika usambazaji na tuhuma za ufisadi katika matumizi.

Hakujibu pia iwapo Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) atafanya ukaguzi maalum wa matumizi ya fedha matumizi ya bilioni 96.4 za mradi wa maji safi na mazingira vijijini katika Jiji la Dar es salaam na Halmashauri zingine na kuwezesha hatua za ziada kuchukuliwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha pamoja na kasoro zingine katika utekelezi wa Programu ya Maji Safi na Mazingira Vijijini (RWSSP) ikiwemo katika Manispaa za Jiji la Dar es Salaam ilipaswa kutekelezwa kuanzia mwaka 2005/2006 na kukamilika mwaka 2010/2011.

Kwa ujumla, hakueleza hatua zozote ambazo Serikali ingetarajia kuchukua kutokana na hatua tisa za haraka nilizopendekeza kwenye hoja yangu na masuala niliyotaka yazingatiwe kutoka katika maelezo yangu ili kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es salaam.(Nakala ya Hoja nimeiambatanisha).


Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 23 Machi, 2012 nilishiriki ziara ya kikazi kukagua shughuli za DAWASA na DAWASCO ambapo wakati wa ziara hiyo nilipatiwa maelezo kuhusu mpango maalum wa kulipatia maji Jiji la Dar es Salaam, ambao utekelezaji wake ulianza mwaka 2011.

Katika ziara hiyo nilitembelea Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu, na baadaye chanzo cha maji cha Ruvu Chini kuona kazi ya upanuzi ya mtambo wa maji wa Ruvu Chini inavyoendelea.

Hata hivyo, nilibaini kwamba kasi ya utekelezaji wa mradi haikuwa inaridhisha hivyo mwezi Oktoba 2012 niliwasilisha taarifa ya hoja binafsi kutaka Bunge lipitishe maazimio ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar Es Salaam.


Uamuzi wangu uliifanya Wizara ya Maji itoe kauli ya Serikali Bungeni tarehe 7 Novemba 2012 kuhusu Mpango wa Haraka wa Maji katika Jiji la Dar Es Salaam na kutoa ratiba ya utekelezaji.


Lakini, baada ya kufuatilia kwa miezi miwili na kubaini kwamba hatua hizo za haraka hazichukuliwi kikamilifu tarehe 4 Februari 2013 niliwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar Es Salaam.


Uamuzi huo uliifanya Wizara ya Maji, DAWASA na DAWASCO kuchukua hatua nyingine za ziada kabla, wakati na baada ya hoja hiyo ambazo nashukuru zimeboresha upatikanaji wa maji safi katika baadhi ya maeneo na kuongeza jitihada za kutekeleza miradi mbalimbali ya maji pamoja na kuwa Waziri wa Maji alisema uongo bungeni na kupendekeza hoja hiyo iondolewe.


Hata hivyo, yapo maeneo mengine ambayo bado matatizo yanaendelea na kwa ujumla Wizara imekuwa haitekelezi kikamilifu ahadi zake ilizotoa bungeni kwa nyakati mbalimbali miaka ya 2011, 2012, 2013 na 2014.

Aidha, kumekuwa na udhaifu wa utendaji katika Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na hivyo kupunguza ufanisi ambao ungewezesha hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar Es Salaam.

Hivyo, kwa kuzingatia Kanuni ya 5 (1) na Nyongeza ya Nane Kanuni ndogo ya 7 (1) (c) (e) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Aprili 2013 naomba uelekeze Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji katika vikao vinavyoendelea kabla ya Mkutano ujao wa Bunge ifuatilie utekelezaji wa Wizara, DAWASA, DAWASCO, EWURA kwa kurejea hoja binafsi niliyowasilisha bungeni, udhaifu unaoendelea mpaka sasa na malalamiko ya wananchi.


Izingatiwe kuwa mradi wa upanuzi wa Ruvu Chini ulipaswa kukamilika kabla ya mwezi Machi 2013; hata hivyo kutokana na udhaifu mbalimbali mradi huo haujakamilika mpaka sasa.

Aidha, kumekuwepo na udhaifu katika utekelezaji wa mradi wa ulazaji wa Bomba Kuu la kipenyo cha milimeta 1,800 kutoka mtambo wa Ruvu Chini hadi Jijini Dar Es Salaam ambapo ilipaswa maji yawe yamefika jijini ikiwemo katika Jimbo la Ubungo Januari 2014 kwa gharama za Shilingi bilioni 192.68.

Kwa upande mwingine, pamoja na Serikali ya Tanzania kupata fedha kutoka Serikali ya India dola za Kimarekani milioni 178.125 sawa na Shilingi bilioni 289.45 kwa ajili ya upanuzi wa chanzo cha maji Ruvu Juu kumekuwepo na udhaifu wa utekelezaji ambao Wizara ya Maji na DAWASA wanapaswa kutoa maelezo kwa Kamati tajwa ya Bunge.


Mradi huo unahusisha ulazaji wa bomba kuu kutoka Mlandizi hadi Kimara; na Ujenzi wa tanki kubwa katika eneo la Kibamba; usanifu na ujenzi wa mabomba ya usambazaji katika maeneo ambayo hayana mtandao wa maji.


Ujenzi wa mradi huo ulipaswa kuanza toka Agosti 2013, hata hivyo mwezi huo ulipita bila ujenzi kuanza hali ambayo ilichelewesha hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi.

Hata baada ya kusainiwa Januari 2014 kwa mikataba ya ujenzi wa Bomba kati ya Serikali na kampuni ya Megha Engineering and Infrastructural Ltd na wa upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji Septemba 2014 kati ya Serikali na Kampuni ya VA-TECH WABAG kuna udhaifu wa utekelezaji.

Kadhalika usanifu na utayarishaji wa vitabu vya zabuni kwa ajili wa ujenzi wa bwawa la Kidunda Mkoani Morogoro ambalo litachangia kuboresha upatikanaji wa maji katika mkoa huo na mikoa ya Pwani na Dar Es Salaam haukukamilika mapema 2013 kama ambavyo Wizara ya Maji iliahidi.

Serikali imekuwa ikisuasua kutenga kwa ukamilifu fedha za ujenzi wa bwawa tajwa zinazokadiriwa kufikia Shilingi bilioni 179.7 hali inayohitaji Bunge kushauri na kuisimamia Serikali ipasavyo.

Wakati huo huo, kwa miaka mingi kumekuwepo pia udhaifu katika kuchukua hatua za kupunguza uvujaji wa maji na maji yasiyolipiwa (non-revenue water) ambapo ilipaswa toka mwaka 2010 kupunguzwa kutoka katika ya 50-60 mpaka asilimilia 25 lakini mpaka sasa utekelezaji ni hafifu.

Tafsiri ya hali hii ni kwamba kwa kuondoa tu upotevu wa maji unaohusisha pia ufisadi na biashara haramu, bila hata kuongeza kiwango cha uzalishaji nusu ya tatizo la maji katika Jiji la Dar Es Salaam ingeweza kupungua au walau hata robo. Hatua hii inahitaji shilingi bilioni 17 tu ambazo Wizara ya Maji, DAWASA na DAWASCO wamekuwa wakisuasua kuzitenga na kutekeleza mipango kwa wakati.

Iwapo hatua zote hizo za haraka na zingine zingechukuliwa maeneo ambayo mabomba yalilazwa na kukarabatiwa ambayo hayapati maji na maeneo yote ambayo hayana mtandao wa maji kwa sasa yangepata maji ya kutosha.

Hatua hiyo ingeambatana na kuhakikisha maeneo mengine yanajengewa mtandao mpya wa mabomba ya majisafi hususani Kiluvya, Kibamba, Mbezi Luisi, Mbezi Msumi, Msakuzi, Makabe, Mpiji Magohe, Saranga, Malambamawili, King'ong'o, Matosa, Bonyokwa, Kibangu, Kinzudi na Goba katika Jimbo la Ubungo.

Hatua hizo zingenufaisha pia wananchi wa majimbo mengine katika Jiji la Dar Es Salaam na Mkoa wa Pwani ikiwemo wa Kinyerezi, Kipawa, Kiwalani, Vinguguti, Uwanja wa Ndege, Ukonga, Gongolamboto, Pugu, Chanika, Tegeta, Bahari Beach, Boko, Bunju, Salasala, Mbezi Juu, Madale, Kisota, Mabwepande, Mpiji, Vikawe, Mapinga, Zinga, Kilombo, Bagamoyo, Kibaha na Mlandizi ambayo hayakufikiwa na miradi ya awali.

Hivyo, kikao na Kamati ya Bunge kitawezesha hatua za haraka za kutolewa kwa kiasi cha Shilingi bilioni 138.85 zinazohitajika kufanikisha kazi hiyo.

Yapo masuala mengi mengine ambayo ni muhimu yakazingatiwa na Bunge kuhusu hatua za haraka za uboreshaji wa upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar Es Salaam ambayo nitayawasilisha kwa Kamati husika ya Bunge ikiwaita viongozi na watendaji wakuu wa Wizara ya Maji, DAWASA, DAWASCO na EWURA.


Wako katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)
 
kwani yeye ndo anakusanya kodi? je maji wakati wa nyuma yalikuwa hayasumbui?

Alipoahidi alikuwa hajui yeye sio mkusanya kodi? Btw thats not how it works brother,he doesnt need to be mkusanya kodi kutatua tatizo la maji he know that ndio mana akaahidi,kibaya ni kwamba ameshindwa kutimiza ahadi yake.
 
Back
Top Bottom