Utafiti: Mnyika kurudi bungeni ni 100%

Utafiti: Mnyika kurudi bungeni ni 100%

Well said stroke, lakini ukumbuke Prof. Lipumba, Mbatia, Mbowe na UKAWA walikuwa na uhakika wa 100% kuwa kura ya maoni April 30 isingewezekana na hawakuwa Mungu wala 'miungu'!!


Hawakua na uhakika bali ili kua ni assumptions based on probability, statements zao hata ungewauliza binafsi wasingekuwa na uhakika 100%, hakina kitu kama 100% mkuu,
 
Wananchi wa Kimara Temboni, Bonyokwa, Suka,wanataka maji na barabara siyo muongozo spika bungeni.
 
kwa kumtetea mnyika apo umebugi mnyika amekuwa mpigaj kelele bungen uku akilinda maslah ya chama na kuwasahau wapgaji kura wake
 
Wananchi wa Kimara Temboni, Bonyokwa, Suka,wanataka maji na barabara siyo muongozo spika bungeni.

Hilo la barabara ni shiiddeeerrr, na vile mvua imeshesha kiaina full aibu wengine inabid tupak sisiem, mbezi ya msuguri na njia ya kwenda mbez makabe inatisha, sema jamaa ana kibur cha kubebwa na kaul ya wanyumban, bado sijaamua kupiga kura uchaguz huu....
 
Blah blah kibao,
wana Ubungo ndio tutaamua,hataki kukanyaga huku anajua maji yalimshinda,na ndio kitakachomuua.
 
Hilo la barabara ni shiiddeeerrr, na vile mvua imeshesha kiaina full aibu wengine inabid tupak sisiem, mbezi ya msuguri na njia ya kwenda mbez makabe inatisha, sema jamaa ana kibur cha kubebwa na kaul ya wanyumban, bado sijaamua kupiga kura uchaguz huu....
Daa!!! Pole sana lakini wanasema Mnyika kaleta maendeleo Ubungo nyie ndio hamuyaoni.
 
Mnyika ni mtu makini na anafaa wanaubungo watamchagua tena kwa kishindo#
 
Hata kama si mwana Ubungo, Mnyika bado anafaa saana
 
Mnyika hafai kabisaa,wanaubungo tunasema basi,dumu la maji tunanunua sh 2000 kwa sasa
Matatizo ya div 5 ndo kama yako.....kazi ya kikatiba ya mbunge ni kutunga sheria, kuisimamia na kuishauri srkl kweny mambo ya kimaendeleo...kiuchumi kinacho justify presence of any govt ni provision of social services kupitia kodi!!!

Suala la tatizo upatknaj wa maji ubungo ni la srkl...mbunge yy ni kueleza amelisea bungeni na srkl amefanya non..then arudishe feedback kwa wananchi kwa maamuzi juu ya watekelezaji.......hope umeelewa kidogo!!!!
 
Kwa Kifupi!,

Propaganda nyingi nimezisikia juu ya John Mnyika. Nyingi zimelenga kusawiri madhaifu yake katika masuala mbalimbali ya kijamii ambayo ameshindwa kuyatatua kama alivyoahidi katika chaguzi mbili zilizopita yaani 2005 na 2010.Mnyika amekuwa akinyooshewa vidole kwa matatizo sugu ya jiji la Dar es salaam kuliko mbunge yeyote. Hii ni kutokana na ahadi zake alizotoa. Wabunge wengine wamekuwa hawaonekani kwa kuwa hawajioneshi. Mnyika anajionesha, ni muwazi, hana desturi ya kunyamaza. Mfano halisi ni takwimu zilizoko kwenye Bunge la 10 ambapo zinaonesha Mnyika ndiye aliyechangia zaidi (mara 540).

Inasemekana anashikilia rekodi toka mfumo wa kibunge umeanzishwa.Hili lilimfanya Mnyika pamoja na kuwa Mbunge wa kitaifa lakini pia ni kama mbunge wa mkoa wa Dar es salaam.Ukienda Ukonga ama Kigamboni kuna watu wanajua mbunge wao ni John Mnyika.Katika utafiti wangu nilitumia njia mbili za kukaa sehemu, kuangalia na kusikiliza (observation), kuhoji watu wa kada mbalimbali (interview) na kuchokonoa mada ili tujadili huku mimi nikichangia kidogo. Nimetembelea wapiga kura wa ubungo na si wasafiri.

Nimetembelea maduka ya ubungo, nimetembelea wafanyakazi mbali mbali wanaofanyakazi ubungo, nimezungumza na wachungaji maarufu wenye makanisa yao ubungo(Ufufuo na uzima, Kanisa la Kakobe). Haya makanisa yana mtaji wa wapigakura zaidi ya elfu ishirini kwa mujibu wao sikwenda kwenye maknisa makongwe na misikiti kwa sababu jimbo la ubungo ni la kipekee nchini. Lina makanisa mengi ya watu binafsi kuliko universal churches and mosques. Vyuo vikuu vilivyoko Ubungo kikiwemo Chuo kikuu cha Dar es salaam, ardhi, St. Joseph na Tumaini.

Nitaeleza katika sehemu tatu kwa kifupi kwa nini Mnyika atashinda.-kazi alizofanya na ambazo hakuanya.-Turufu yake yaani mtaji alionao wa wapiga kura.-Mvuto na uwezo binafsi wa Mnyika.UTEKELEZAJIMnyika aliingia na slgan ya neno "AMUA" Akifafanua kama.A- Akili (Elimu bora) na afya boraM- Maji (Upatikanaji maji)U- Usafiri (Kupunguza adha ya usafiri)A- Ardhi (kupunguza migogoro ya ardhi.Katika suala la Elimu kupitia mfuka wa maendeleo ya jimbo, Mnyika ametoa zaidi ya madawati 1000 shule za ubungo. Kwa upande wa afya Mnyika ameendelea kuibana serikali katika mpango wa Ujenzi wa zahanati na vituo vya afya kujengwa ubungo (rejea michango yake bungeni) Parliament of Tanzania.

Kwa mujibu wa katibu wa Mnyika ndg. Azizi Himbuka jumla ya zahanati 5 zimejengwa Ubugo na zingine mbili ziko kwenye hatua za mwisho, huku mbili zikipanda hadhi kuwa vituo vya afya.MAJI.Kwa kipindi cha Januari 2011 hadi hivi sasa jumla ya miradi mitano ilibuniwa. Mitatu imekamilika kupeleka maji Chuo Kikuu Mlimani, ardhi na NIT-chuo cha usafirishaji.Hivi sasa kuna miradi 2 mikubwa itakayomaliza kabisa tatizo la maji Ubungo kutoka Mito ya Ruvu na Wami.

Mnyika anweza kuomba subira ya wananchi ili akamilishe miradi hiyo. Hata Roma haikujengwa Siku mmoja... Wana ubungo wanakumbka jinsi alivyojenga hoja juu ya upatikanaji maji Dar es Salaam... Kilio chake kimesikika.. Maji hayo yanakuja. Akiyaeleza haya kwa ufasaha bila kigugumizi Mnyika ni 100%.USAFIRIHapa Mnyika Kafanikiwa kuliko alivyoahidi. Ameondoa bughdha ya wasafiri wa mikoani na ndani ya jiji. Kukamiliaka kwa Ujenzi wa stendi ya daladala Mawasiliano-Sinza kumefanikisha kupungua kwa msongamano mkubwa wa magari stendi kuu ya ubungo. Pia amesimamia hadi kukamilika barabara za Mbezi Mwishi-Goba hadi Tangibovu. Msewe hadi Baruti na nyingine Kibao. Hivi sasa kuna ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendokasi.

Anasimamia.ARDHIkuhusu ardhi Mnyika amefanikiwa pia. Hivi sasa migogoro ya ardhi imepungua sana na wananchi wanaohamishwa kupisha miradi hufidiwa kwa wakati kutokana umakini wa Mwakilishi wao.Yeye binafsi amekuwa na kawaida ya kuandaa michezo kama Mnyika Cup,.... Amefanya mengi na ataendelea kuyafanya.TURUFU YAKE.Mimi si mkabila ila uchunguzi wangu umegundua kuwa jimbo la ubungo ni la makabila yote. Ukitaka kufika Dar es salaam lazma upitie Ubungo.

Ila nimegundua kati ya wenye uwezo wa kupiga kura kutokana na pilika za ubungo ni watu wenyebiashara na makazi ubungo. Hawa ni wafanyakazi, wafanyabiashara hasa wa maduka, watumishi wa serikali... Watakaopiga kura kwa uchache ni wapiga debe, wamachinga na wauza vyakula kutokana na aina za kazi zao.. Utakuta wengi hawatajiandikisha.Wenye maduka wengi kwa Ubungo ni wachaga, wapare na wakinga na si wahindi kama ilivyo kariakoo... Wachaga husingiziwa kuwa wenye Chadema, na Mnyika ni Mpare kwa asili...

Ndio maana Mnyika hana wasi wasi.Pili ushawishi wa Marafiki wa Chadema ambao ni wachungaji Gwajima na Kakobe ni mtaji mwingine. Kitu kingine kitachombeba ni UKAWA. Pia ameanikiwa kuwafikia wanavyuo.

MVUTO NA UWEZO WA KUJIELEZA.Hapa atawavutia kwa jinsi navyomfahamu wale wasiokuwemo kwenye makundi Tajwa...

Kwa makadiro Mnyika ataingia kwenye kinyang'anyiro na mtaji wa kura 75, 000.

Nawsilisha

hilo nalo jibu
 
Mnyika hafai kabisaa,wanaubungo tunasema basi,dumu la maji tunanunua sh 2000 kwa sasa

10.jpg


Baada ya serikali ya ccm kushindwa kuwapatia wananchi maji, chama kimeanza utaratibu wa kuwapelekea wananchi maji kwa madumu, tangu mwezi uliopita ninaletewa madumu mwili asubuhi na jioni madumu mawili, kama bado hupati huduma hii wasiliana na ofisi ya chama iliyo karibu.
 
Kumbe Darasa la Saba.. Ndo maana huelewi.

hakuna mtanzania yeyote wa kisasa ambaye hakupita hilo darasa mkuu , japokuwa hivi sasa namiliki vijidigrii viwili , halafu kwa ushenzi sijawahi kuomba kazi kwenye serikali hii , bali namiliki kiwanda na kugawa ajira kwa wengine zaaidi ya 300 .
 
Mnyika hata hasipo fanya kampeni sisi wana ubungo tunamchagua 100%
 
Wananchi wa Kimara Temboni, Bonyokwa, Suka,wanataka maji na barabara siyo muongozo spika bungeni.
Sa wananchi kama hawaoni relationship iliyopo kati ya matatizo waliyonayo na kuomba mwongozo bungeni basi ni tatizo la akili ndogo tuuu!!!! Kwani walimchagua akasemee wapi hayo matatizo yao????
 
Back
Top Bottom