Utafiti: Mnyika kurudi bungeni ni 100%

Utafiti: Mnyika kurudi bungeni ni 100%

mwenye uhakika wa jambo lolote kwa asilimia 100 ni Mungu tu wengine tunabahatisha, hivyo Mnyika hana asilimia hizo
Well said stroke, lakini ukumbuke Prof. Lipumba, Mbatia, Mbowe na UKAWA walikuwa na uhakika wa 100% kuwa kura ya maoni April 30 isingewezekana na hawakuwa Mungu wala 'miungu'!!

 
Tuache majungu ukweli unauma huyo bwana mdogo ana talanta ya pekee sana mtumieni bila kujali itikadi zenu.
 
Mi binafsi nakaa Arusha na ni mwanachama wa ccm lkn Mnyika namkubal sana wanaubungo tunawaomba msimwangushe huyo kijana kwan anatetea masirah ya nchi nzima!
 
Ufike mda watz tujadili mambo ya msingi na kwa hoja na sio kutukana Tu, kazi ya mbunge Ni kuisimamia kuishauri na kuiwajibisha serikali. Na kwa hapo John mnyika kajitahidi Sana ukilinganisha na wabunge wengine.
 
Nimewauliza wanaUbungo. Wanasema maji ni tatizo sugu toka uhuru.... Hakuna wakati ambao kidogo wamepata nafuu ya maji kama sasa... Miradi miwili ya mto Wami na Ruvu itamaliza tatizo kabisa. Anasimamia utekelezaji kwa karibu.

Hakuna sehemu Ubungo ndoo ya maji inauzwa 2000. Karibu Ubungo uulize.

Mkuu ni bora usingepoteza muda wako ku argue na mtu anaeleta porojo na upuuzi juu,kukaa kimya kwa w.a.j.i.n.g.a kama hawa uwa ni jibu pia!
 
Huwa naangalia sana Bunge ktk TV. Kuna Mh. Mmoja wa jinsia ya kike upande wa kuume wa spika huwa anjifunika na nguo kubwa siku zote nadhani AC ya pale ndani inamsumbuwa.Huyu Mh.hata siku moja sijamuona akichangia kitu chochote kwa miaka mitano sasa.Mh.Mary Chatanda na mchango wake wa utawala bora ndani ya vyama vyetu labda atatusaidia.
 
Sasa hivi kila sehemu anapingwa.

nikukumbushe rafiki yangu Simiyu Yetu
kikao cha ndani alichokifanya mangula ubungo kikao hicho kilikuwa kinajaribu kutengeneza propaganda za kijinga against Mnyika ambayo kazi hiyo walipewa vijana maarufu kwa jina la Book 7 soon tuttayaweka wazi haya kwa wananchi with facts

kama una taarifa waulize mabosi wako
 
Last edited by a moderator:
HAAAAAAHAAA ati mnyika atarudi Bungeni, hii ni ndoto ya mchana kweupe , ubunge atausikia kwenye redio tu, na ndio sababu kaamua kujipa unaibu wa saccos ili abaki na posho ya saccos baada ya kukosa ubunge
 
Mleta mada huna kazi ya kufanya?
Unapoteza muda kuhakiki kwa kitu kilichowazi kama hiki.
Ungetumia muda na rasilimali kutafiti kuhusu majimbo mengine ila sio Ubungo.
Mnyika hana upinzani hata kidogo.

NB.Usipelekeshwe na propaganda za magamba kamanda,dont afford to loose your focus.
Hatihati zipo kwa Akunay,Shibuda and co.
 
Kosa kubwa la Mnyika ni kumuita kihalisia Mkiti wao wa Chama jina la.... (Cybercrime) Vinginevyo mitaahira ya Lumumba kamwe isingekuwa inakesha hapa kutupa taka zao..!!

Wakikurupushwa tu usingizini, kitu cha kwanza wanachowaza ni namna ya kupiga propaganda kwa Mnyika na Dr Slaa, Hata ulikurupushe saizi lile kubwa la Mataahira laki si pesa utasikia tu.!!! Ila wakizama kwenye kona hata wao wanajua hakuna mbunge bora tangu kuanza kwa awamu hii ya tano kama Mnyika nenda uendako.!!!

Kwanini ushindwe kumrudisha Bungeni mbunge kama huyu? Hata Shemeji gsu angekuwa anakaa Ubungo angempigia kura Mnyika.!! Hata kama angeahidiwa Mbege na Kinana.

Mnyika go go go go..

BACK TANGANYIKA

Kusema ule UKWELI Mnyika John ni kiboko yetu.............yaani tuna:A S-cry::A S-cry: tukifikiria tu yaani UBUNGO ndiyo basi tena kama MTOTO ASIYE RIDHIKI vile.........
 
Mleta mada manu umenichanganya kabisa. Mi siku zote najuaga huyo JJ Mnyika ni mbunge wangu huku Mafia. Jamani mweee kweli Ubungo mna mwakilishi. Sio sie huku bora liende.
 
Last edited by a moderator:
tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi ubungo hawajawahi kuwa na mbunge kama mnyika kamwe
. mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Mnyika atagombea na kushinda chaguzi zote.mpaka atakapostaafu kama Ndesamburo.
 
Kwa Kifupi!,

Propaganda nyingi nimezisikia juu ya John Mnyika. Nyingi zimelenga kusawiri madhaifu yake katika masuala mbalimbali ya kijamii ambayo ameshindwa kuyatatua kama alivyoahidi katika chaguzi mbili zilizopita yaani 2005 na 2010.Mnyika amekuwa akinyooshewa vidole kwa matatizo sugu ya jiji la Dar es salaam kuliko mbunge yeyote. Hii ni kutokana na ahadi zake alizotoa. Wabunge wengine wamekuwa hawaonekani kwa kuwa hawajioneshi. Mnyika anajionesha, ni muwazi, hana desturi ya kunyamaza. Mfano halisi ni takwimu zilizoko kwenye Bunge la 10 ambapo zinaonesha Mnyika ndiye aliyechangia zaidi (mara 540).

Inasemekana anashikilia rekodi toka mfumo wa kibunge umeanzishwa.Hili lilimfanya Mnyika pamoja na kuwa Mbunge wa kitaifa lakini pia ni kama mbunge wa mkoa wa Dar es salaam.Ukienda Ukonga ama Kigamboni kuna watu wanajua mbunge wao ni John Mnyika.Katika utafiti wangu nilitumia njia mbili za kukaa sehemu, kuangalia na kusikiliza (observation), kuhoji watu wa kada mbalimbali (interview) na kuchokonoa mada ili tujadili huku mimi nikichangia kidogo. Nimetembelea wapiga kura wa ubungo na si wasafiri.

Nimetembelea maduka ya ubungo, nimetembelea wafanyakazi mbali mbali wanaofanyakazi ubungo, nimezungumza na wachungaji maarufu wenye makanisa yao ubungo(Ufufuo na uzima, Kanisa la Kakobe). Haya makanisa yana mtaji wa wapigakura zaidi ya elfu ishirini kwa mujibu wao sikwenda kwenye maknisa makongwe na misikiti kwa sababu jimbo la ubungo ni la kipekee nchini. Lina makanisa mengi ya watu binafsi kuliko universal churches and mosques. Vyuo vikuu vilivyoko Ubungo kikiwemo Chuo kikuu cha Dar es salaam, ardhi, St. Joseph na Tumaini.

Nitaeleza katika sehemu tatu kwa kifupi kwa nini Mnyika atashinda.-kazi alizofanya na ambazo hakuanya.-Turufu yake yaani mtaji alionao wa wapiga kura.-Mvuto na uwezo binafsi wa Mnyika.UTEKELEZAJIMnyika aliingia na slgan ya neno "AMUA" Akifafanua kama.A- Akili (Elimu bora) na afya boraM- Maji (Upatikanaji maji)U- Usafiri (Kupunguza adha ya usafiri)A- Ardhi (kupunguza migogoro ya ardhi.Katika suala la Elimu kupitia mfuka wa maendeleo ya jimbo, Mnyika ametoa zaidi ya madawati 1000 shule za ubungo. Kwa upande wa afya Mnyika ameendelea kuibana serikali katika mpango wa Ujenzi wa zahanati na vituo vya afya kujengwa ubungo (rejea michango yake bungeni) Parliament of Tanzania.

Kwa mujibu wa katibu wa Mnyika ndg. Azizi Himbuka jumla ya zahanati 5 zimejengwa Ubugo na zingine mbili ziko kwenye hatua za mwisho, huku mbili zikipanda hadhi kuwa vituo vya afya.MAJI.Kwa kipindi cha Januari 2011 hadi hivi sasa jumla ya miradi mitano ilibuniwa. Mitatu imekamilika kupeleka maji Chuo Kikuu Mlimani, ardhi na NIT-chuo cha usafirishaji.Hivi sasa kuna miradi 2 mikubwa itakayomaliza kabisa tatizo la maji Ubungo kutoka Mito ya Ruvu na Wami.

Mnyika anweza kuomba subira ya wananchi ili akamilishe miradi hiyo. Hata Roma haikujengwa Siku mmoja... Wana ubungo wanakumbka jinsi alivyojenga hoja juu ya upatikanaji maji Dar es Salaam... Kilio chake kimesikika.. Maji hayo yanakuja. Akiyaeleza haya kwa ufasaha bila kigugumizi Mnyika ni 100%.USAFIRIHapa Mnyika Kafanikiwa kuliko alivyoahidi. Ameondoa bughdha ya wasafiri wa mikoani na ndani ya jiji. Kukamiliaka kwa Ujenzi wa stendi ya daladala Mawasiliano-Sinza kumefanikisha kupungua kwa msongamano mkubwa wa magari stendi kuu ya ubungo. Pia amesimamia hadi kukamilika barabara za Mbezi Mwishi-Goba hadi Tangibovu. Msewe hadi Baruti na nyingine Kibao. Hivi sasa kuna ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendokasi.

Anasimamia.ARDHIkuhusu ardhi Mnyika amefanikiwa pia. Hivi sasa migogoro ya ardhi imepungua sana na wananchi wanaohamishwa kupisha miradi hufidiwa kwa wakati kutokana umakini wa Mwakilishi wao.Yeye binafsi amekuwa na kawaida ya kuandaa michezo kama Mnyika Cup,.... Amefanya mengi na ataendelea kuyafanya.TURUFU YAKE.Mimi si mkabila ila uchunguzi wangu umegundua kuwa jimbo la ubungo ni la makabila yote. Ukitaka kufika Dar es salaam lazma upitie Ubungo.

Ila nimegundua kati ya wenye uwezo wa kupiga kura kutokana na pilika za ubungo ni watu wenyebiashara na makazi ubungo. Hawa ni wafanyakazi, wafanyabiashara hasa wa maduka, watumishi wa serikali... Watakaopiga kura kwa uchache ni wapiga debe, wamachinga na wauza vyakula kutokana na aina za kazi zao.. Utakuta wengi hawatajiandikisha.Wenye maduka wengi kwa Ubungo ni wachaga, wapare na wakinga na si wahindi kama ilivyo kariakoo... Wachaga husingiziwa kuwa wenye Chadema, na Mnyika ni Mpare kwa asili...

Ndio maana Mnyika hana wasi wasi.Pili ushawishi wa Marafiki wa Chadema ambao ni wachungaji Gwajima na Kakobe ni mtaji mwingine. Kitu kingine kitachombeba ni UKAWA. Pia ameanikiwa kuwafikia wanavyuo.

MVUTO NA UWEZO WA KUJIELEZA.Hapa atawavutia kwa jinsi navyomfahamu wale wasiokuwemo kwenye makundi Tajwa...

Kwa makadiro Mnyika ataingia kwenye kinyang'anyiro na mtaji wa kura 75, 000.

Nawsilisha

Umemaliza?
 
Kurudi au kutorudi bungeni sio hoja kubwa sana lakini naamini binadamu mwenye akili timamu kwenda kwenye kituo cha kupiga kura na kuiona picha ya Mnyika kisha ukamtick mwingine tofauti, ni kutokutendea haki maisha yako!

Maisha gani?
 
Mnyika hafai kabisaa,wanaubungo tunasema basi,dumu la maji tunanunua sh 2000 kwa sasa

yaani ulivyo mpuuzi hujui kuwa serikali yenu ya CCM ina jukumu la kuwapatia wananchi maji safi na salama

Mbunge ni mwakilishi wa wananchi

Anawawakilisha kudai haki zao kule panapostahili

Kazi ya Uwakilishi Mnyika ameifanya kwa umakini mkubwa....

Mnyika amekuwa mstari wa mbele kudai suala la maji katika jimbo lake...

Katika kipindi chake tumeona mashinikizo mengi sana kwenda kwa waziri wa maji

Ametoa Hadi hoja binafsi bungeni kwa suala la maji Dar es salaam
 
Nimekaa ubungo miaka kumi sasa namkubali sana huyu kamanda Mnyika. Maji yakikatika tunaenda kudai akiwa mstari wa mbele na dawasco wananywea maji wanatoa. Chezea Mnyika wewe

Kumbe we umekuja juzi tu hapa! ah! tunabishana na wakuja tu, we humjui hata mzee Mfuga mbwa wa tip top, hupajui hata kwa mkata kimeo, we pale kwe daraja la manzese hujui kama ndio msufini, huwajui hata waimba mnanda wa mwanzo Hisani gari kubwa, kifupi hujui hata biti kaenga mwenyewe wa Mburahati alikuwa anakaa wapi, Jimbo la Ubungo limeharibiwa na siasa za kitoto za huyo dogo, sidhani kama atarudi mjengoni labda kwa kuteuliwa.
 
Back
Top Bottom