Utafiti: Kwanini walimu wamefika hapa walipo leo

Utafiti: Kwanini walimu wamefika hapa walipo leo

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,784
Reaction score
6,180
UTAFITI KWANINI WALIMU TUMEFIKA HAPA TULIPO
Wanajamvi ni muda wa miaka kama mitatu nimekuwa nikifanya utafiti binafsi juu ya maendeleo ya walimu nchini Tanzania na kikubwa niliangalia kwanini walimu wapo hivi walivyo leo?.. utafiti huu umeshirikisha baadhi ya walimu walioko kazini, waliostaafu, wanachuo baadhi (wanaosomea ualimu) walimu wapya baadhi na wanfunzi baadhi, kwa haraka haraka nimewahoji watu zaidi ya 150 kwa kipindi hicho nilikuwa mwanafunzi na nikaendelea hadi wakati nimeajiriwa rasmi kama mwalimu na wale niliowakuta kazini pia nilipata nafasi ya kuwauliza? hata hivyo sikuweza kuandika utafiti huu kutokana na sababu mbali mbali

Kuna sababu nyingi zilizosababisha walimu kufikia hapa tulipo sasa?. Kwa nyakati tofauti nimekutana na walimu na mara kadhaa wanachuo mbali mbali wanaosomea ualimu nimejifunza kuwa tupo leo kutokana na sababu zifuatazo..

1. (a) Walimu wenyewe:
Wakati nikifanya utafiti huu nimegundua wapo walimu ambao huona aibu hata kujitambulisha mbele za watu kuwa wao ni walimu? nilijaribu kuwauliza walimu kadhaa swali hili ?unajisikiaje kuwa mwalimu? Ulichagua mwenyewe kazi hii au imetokea tu baada ya kukosa kazi ile uliyoipenda??
Majibu niliyokutana nayo yanasikitisha, idadi kubwa ya walimu walisema kuwa hawakuipenda kazi hiyo na wengine wamediriki kusema wana mpango wa kubadilisha fani! Sasa kama wewe mwenyewe huijali na huipendi taaluma yako nani atakujali? Hebu walimu tubadilike kwa kujiamini kuwa kazi yetu ni bora na ni nzuri JIHESHIMU KWANZA NDIPO UHESHIMIKE!

(b) chama cha walimu Tanzania (CWT)
Chama hiki kilikuwa na malengo mazuri lakini chama hiki hakina madhumuni na nia ya moja kwa moja kumkomboa mwalimu wa Tanzania zaidi ya kutumia mgongo wa walimu wengi kunufaisha walimu viongozi wachache.. katika hili 90% ya walimu wapo tayari kujitoa CWT hata leo.. katika utafiti wangu huu walimu wengi (nikiwemo mimi) nimeipinga CWT hadharani kuwa haina mchango wowote mkubwa kulinganisha na vyama vingine vya wafanyakazi! Mara mia bora chama cha madereva Tanzania kuliko cwt!

(c) maafisa Elimu
Huu ni ukweli mchungu kuwa baadhi ya maafisa elimu wengi ndio wanaosababisha walimu kuonekana vituko mbele ya jamii.. unaweza kwenda ofisini kufuatilia madai yako lakini afisa akakuwekea zengwe utadhani hela analipa yeye! Lakini maafisa wengine hubania walimu kwenda kujiendeleza kimasomo kuhofia nafasi zao! Kitu kinachouma zaidi maafisa hawa WENGI walikuwa walimu lakini ndio wanaongoza kwa kukandamiza walimu wenzao!
(d) walimu hawana umoja
Walimu hawana umoja! Utakuta mwalimu aliyelipwa madai yake hawezi kumsaidia Yule ambae bado! Walimu hawana sauti ya pamoja! Wanaweza kukubaliana wasiingie darasani na wakasaini lakini wengine wakaingia kufundisha! Na yote hii ni kufeli kwa cwt katika kuunganisha walimu kuwa kitu kimoja.
2 .JAMII
Kutokana na walimu kujidharau wenyewe jamii pia huambukizwa tabia hiyo na ndio maana utakuta mzazi anamuuliza motto wake ?mwanangu umekosa hata ualimu?? hapa akimaanisha ualimu ndio ?the cheapest? kuliko ajira zote, na wengine wakaenda mbali kudai kuwa kazi ya ualimu ni kazi ya watu waliofeli! Nakumbuka wakati Fulani nilifundisha shule moja ya English medium darasa la tano siku moja nikawauliza kama wanatamani kuwa walimu, nilishangaa wakikataa kabisa na hata wale wachache waliokubali walichekwa na wenzao! Nilipowauliza kwanini wakasema eti mishahara midogo hahahahaha! Sasa jiulize mtoto mdogo anajua eti walimu wanalipwa kidogo? nikaishia kuwauliza ?who told you??


3.VIONGOZI WA SERIKALI
Baada ya hayo yote viongozi wa serikali wamewafikisha walimu hapa walipo leo hii, walimu wametumika kama daraja kupitisha viongozi wengi ambao hutoa ahadi kedekede lakini baada ya hayo huwadharau walimu! Ni mwalimu yupi asiyekumbuka kauli ya Madam Mwantum Mahiza? Ni mwalimu yupi aliyesahau kauli ya Raisi kikwete uchaguzi wa 2010? Sasa kauli za kuvunja moyo kwa walimu zinapotolewa na viongozi wakubwa ndipo sasa hata wanafunzi wa chekechea wanachukia ualimu!

MAPENDEKEZO:
1. Mwalimu jiheshimu mwenyewe kuanzia unavyokula, unavyovaa, unavyoongea, usipende maisha ya shida shida sana hata kama mshahara ni mdogo? kuna kipindi nilienda halmashauri nikakutana na mwalimu kavaa yebo yebo anaenda kuchukua mshahara! Sasa hapa watoto wakikuona watatamani kazi yetu kweli!!?

2. Walimu tupiganie kujitoa CWT hebu tuanze kwanza kupinga 2% ya mshahara kuliwa kienyeji na wahuni wachache.
3. Walimu tuwe na umoja, umoja uanzie shuleni, kasha kwenye kata zetu kisha wilaya kasha nchi nzima, wakuu wa shule msiwe kimbele mbele kuwachongea walimu wenu halmashauri kuweni wa kwanza kuwatetea hebu cheki.. Rais JPM kaenda ofisi ya fedha kauliza wafanyakazi wengine wako wapi kajibiwa wameenda kunywa chai! Lakini mkuu wa shule akiulizwa wako wapi walimu wako wawili atasema ?hata mimi sijui, tena wana siku ya tatu leo hawajaonekana kazini mheshimiwa!?
MWISHO.
Yapo mambo mengi lakini sikuyataja hapa kwa kuhofia uzi huu kuwa mrefu sana na kuchosha watu? hata hivyo nina mpango wa kuchapa makala kuhusu utafiti huu. Nasubiri maoni na mtazamo wenu.
Mwalimu allan
allanclement6@gmail.com
 
Mimi ni mwalimu sekondari niliajiriwa mwaka 2012,mwanzo nilikuwa najiamini na ualimu wangu,baada ya kuona nakosa vinono hapa Dar,tena nina maisha mazuri,nikasema isiwe tabu na shida sijarudia tena kuupenda ualimu na kujitambulisha kama mwalimu sasa jiji la Dar siwezi kukosa chochote,nikiulizwa unafanya kazi gani jibu ni Biashara na kilimo,walimu tuna hali ngumu
 
Chanzo kikuu cha matatizo mengi ya walimu ni Bongo ndogo, Mengine yote ni nyongeza tu.

Amini au usiamini kuna walimu wengi sana ni mizigo kiasi kwamba unakuwa na hofu kuu unaposikia ndio wanaomfundisha mtoto wako.

Kwa mfano nilipara kuwauliza walimu 2 wa shule ya msingi swali kwamba MLIMA MERU UPO mkoa wa Arusha au Manyara? wote wakasema upo Manyara. Kwa hiyo walimu hawa ambao hawaelewi vitu vilivyo wazi hivi watawezaje kuvutia kuheshimiwa na watu wengine?

Naishauri serikali kuwa kuanzia mwakani ambapo elimu itatolewa bure kuanzia chekechea hadi kidato cha 4 ni bora pia ikaanza kuajiri walimu waliopata daraja la kwanza au la pili katika mitihani ya kidato cha nne na sita hapo ndiyo taaluma ya ualimu itaheshiika.

Na ili walimu wenye sifa hizo wapatikani ni lazima pia mpunga wao wa kila mwezi uwe mwingi.
 
Last edited by a moderator:
Hii inanifaa sana kuiwasilisha kwa ndugu zangu, maana ukoo wangu umejaa walimu karibia asilimia 90.
 
Umejieleza vizuri,ukweli %kubwa ya walimu ni wale waliofeli!!!!
 
Nilishangaa mkoa fulani kipindi kile cha mgomo wa walimu, Afisa elimu aliagiza vyeti vya walimu vikaguliwe kuanzia fom four hadi vyuo!

Nikashindwa kupata correlation ya mgomo na vyeti.
 
Walimu wengi ni wanafiki na wazandiki maana Mimi mwenyewe ni mwalimu nipo hapa mbeya sekondari ya kata.... Inasikitisha sana kuona mwalimu wa degree kumuogopa mkuu wa shule hata kuhoji mambo madogomadogo tu wanaogopa......
 
kuna mambo madogo madogo ambayo poa yanasababisha walimu kuzalaulka ikiwemo weledi wa kutenda kazi zao.kwa mfano hiki kilichoandikwa hapa sio research report bali ni malalamiko na mtazamo wa mtoa mada.

kanuni za kuandika ripoti zinajulikana,kwanza hujasema title ya utafiti wako,research methodology,objectives,target population, literature review nk.kwa ufupi huu sio utafiti ila ni malalamiko kama kawaida yenu walimu.

kama walimu hamuwezi kufanya hata research ndogo kama hii msitegemee jipya kutoka serikalin.lieni tu.
 
kuna mambo madogo madogo ambayo poa yanasababisha walimu kuzalaulka ikiwemo weledi wa kutenda kazi zao.kwa mfano hiki kilichoandikwa hapa sio research report bali ni malalamiko na mtazamo wa mtoa mada.

kanuni za kuandika ripoti zinajulikana,kwanza hujasema title ya utafiti wako,research methodology,objectives,target population, literature review nk.kwa ufupi huu sio utafiti ila ni malalamiko kama kawaida yenu walimu.

kama walimu hamuwezi kufanya hata research ndogo kama hii msitegemee jipya kutoka serikalin.lieni tu.

Cc Kipilipili
 
Last edited by a moderator:
...na hatuwezi kuendelea pia ikiwa tuna watu wanaojifanya kujua kila kitu na kukurupuka kujibu ilihali hawajui chochote mfano wewe Rutorial k... nimesema wazi kuwa sijaandika kila kitu hapa kwakuwa uzi ungekuwa mrefu... je ulitaka niandike utafiti wote niweke sampling ya watu zaidi ya 150 hapa wewe mwenyewe ungekuwa wa kwanza hapa kusema uzi huo ni mrefu.... unasema mimi nimetoa malalamiko badala ya utafiti? hahahahaha! nahisi wewe ni mojawapo ya wale waliokwazika na ukweli huu... pole sana.
 
Last edited by a moderator:
Chanzo kikuu cha matatizo mengi ya walimu ni Bongo ndogo,Mengine yote ni nyongeza tu. Amini au usiamini kuna walimu wengi sana ni mizigo kiasi kwamba unakuwa na hofu kuu unaposikia ndio wanaomfundisha mtoto wako.Kwa mfano nilipara kuwauliza walimu 2 wa shule ya msingi swali kwamba MLIMA MERU UPO mkoa wa Arusha au Manyara? wote wakasema upo Manyara. Kwa hiyo walimu hawa ambao hawaelewi vitu vilivyo wazi hivi watawezaje kuvutia kuheshimiwa na watu wengine?.Naishauri serikali kuwa kuanzia mwakani ambapo elimu itatolewa bure kuanzia chekechea hadi kidato cha 4 ni bora pia ikaanza kuajiri walimu waliopata daraja la kwanza au la pili katika mitihani ya kidato cha nne na sita hapo ndiyo taaluma ya ualimu itaheshiika.Na ili walimu wenye sifa hizo wapatikani ni lazima pia mpunga wao wa kila mwezi uwe mwingi.

Hao wanaoshindwa hata kutambua mlima!Ni wale makanjanja natilia mashaka vyeti vyao kuwa ni halali? fani imeingiliwa.
 
Chanzo kikuu cha matatizo mengi ya walimu ni Bongo ndogo,Mengine yote ni nyongeza tu. Amini au usiamini kuna walimu wengi sana ni mizigo kiasi kwamba unakuwa na hofu kuu unaposikia ndio wanaomfundisha mtoto wako.Kwa mfano nilipara kuwauliza walimu 2 wa shule ya msingi swali kwamba MLIMA MERU UPO mkoa wa Arusha au Manyara? wote wakasema upo Manyara. Kwa hiyo walimu hawa ambao hawaelewi vitu vilivyo wazi hivi watawezaje kuvutia kuheshimiwa na watu wengine?.Naishauri serikali kuwa kuanzia mwakani ambapo elimu itatolewa bure kuanzia chekechea hadi kidato cha 4 ni bora pia ikaanza kuajiri walimu waliopata daraja la kwanza au la pili katika mitihani ya kidato cha nne na sita hapo ndiyo taaluma ya ualimu itaheshiika.Na ili walimu wenye sifa hizo wapatikani ni lazima pia mpunga wao wa kila mwezi uwe mwingi.

we we ulipata darajaa ngap??? hebu tuanzie halo acha longolongo
 
Back
Top Bottom