ni kweli kuna comments humu nikiziangalia najisikia kulia hususani wale wote wanaotetea CWT
Nakubaliana na utafiti wako kwa asilimia 45 lakini napingana nawewe kwa asilimia 40 hasa pale unapo kifananisha CWT na chama cha madreva maana were mwenyewe unatamani kuwa dreva kuliko fani yako ya ualimu.
Chama cha walimu ni trade union ambayo lengo kuu nikumtetea mwalimu nakudai haki ya mwalimu kutoka kwa mwajiri kwa vile tunaamini umoja ni nguvu.Angalia ni jinsi gani unavyoshirikiana na mwakilishi wa CWT mahala pako pa kazi.CWT pamoja na changamoto zake iko imara kuliko chama kingine cha wafanyakazi Tanzania.
Ndio maana mnadharauliwa. Wakuu wa shule sio walimu?Walimu wengi wanapenda kujipendekeza kwa wakuu wa shule ili wapendekezwe kwenda kazi maalumu
JAMII IMEKARIRISHWA KUWA WALIMU WALIFELI MITIHANI.NI DHANA POTOFU. WANAOFIKIRI HIVYO HAWAJITAMBUI!!Mliowaponda walimu katika Uzi huu wote mabwege na marofa, Mimi ni Mwl. nimesoma chuo hostel mwaka wa kwanza niliishi room Moja na walimu wenzangu wa3, wote tulikuwa na division one form 6, mwaka wa pili nikaishi na jamaa aliesomea tourism na BBA wote walikuwa na division three form six, mwaka wa tatu tulikuwa wa4 walimu tupu, watatu tuna one na mmoja two, sasa sijui mnazungumzia walimu wa miaka hii ya Distinction na Merit, sijaelewa.
wengine wana dhiki kuliko hao walimu wa madarasani mf. ni vigumu kwao kufanya biashara ndogo ndogo kuhofia kugaragaza hadhi yao but wale wa madarasani wanafanya.Kwanza nipende kuwapongeza walimu wenzangu mmekuwa na lugha nzuri hasa kuwajibu wale wanaokuja na kejeli...pili tunasalitiwa na walimu wenzetu waliopewa madaraka..mfano ukienda halmashauri wale asilimia kubwa ni walimu lakini ona wanavyotunyanyasa,ona wakuu wa shule jamanii tabu tupu utadhani wanapata ma bilioni ya pesa...dah
Mimi huwa sielewi mtu mwenye fani yake akiambiwa alifeli .Kufeli maana yake nini?Engineer alifeli kufanya kozi nyingine akafaulu kuwa engineer aidha mwl alifeli kufanya ikozi nyingine akafaulu kuwa mwalimu.WALIOFELI HAWAJUFANYA KOZI YOYOTE.tena nasema mimi ni mwalimu wala sikufeli anayesema walimu wote wamefeli hayupo sahihi..ILA NASEMA HAKUNA YEYOTE KATIKA WATU ATAKAYE NI SUMBUA AWE ANACHEO AU LAAH..NAJIAMINI NA KUJIKUBALI TENA SIKUBAHATISHA...KWANGU WAJIPANGE SAAANA...KARIBUNI KILINDI
Ww inaonekana ulifaulu sana eee, labda tuweke matokeo yako na cc ili tujue upo sahihi ama nn, frankly speaking mie ni mwalimu but ni mwalim wa kufaulu vizuri o level Nina dv two,advance one .sasa utaropokaje eeee walimu ni watu waliofeli? Acha dharauwe we ulipata darajaa ngap??? hebu tuanzie halo acha longolongo
malengo ya CWT yapo kwenye maandishi tu na si kiutekelezaji. UIMARA unaozungumza wewe ni upi? uimara wa kutetea maslahi ya walimu au uimara wa kuwakata walimu makato kila mwezi tena wengine bila hata kujiunga?Nakubaliana na utafiti wako kwa asilimia 45 lakini napingana nawewe kwa asilimia 40 hasa pale unapo kifananisha CWT na chama cha madreva maana were mwenyewe unatamani kuwa dreva kuliko fani yako ya ualimu.
Chama cha walimu ni trade union ambayo lengo kuu nikumtetea mwalimu nakudai haki ya mwalimu kutoka kwa mwajiri kwa vile tunaamini umoja ni nguvu.Angalia ni jinsi gani unavyoshirikiana na mwakilishi wa CWT mahala pako pa kazi.CWT pamoja na changamoto zake iko imara kuliko chama kingine cha wafanyakazi Tanzania.