Utafanyaje ukigundua mimba yako ilitaka kutolewa ili usizaliwe?

raiswenu

JF-Expert Member
Apr 20, 2018
794
1,429
Umeshakuwa mtu mzima sasa unajitambua, harakati za maisha zinaendelea kama kawaida, mara unakuja kugundua kuwa wewe ni abortion survivor, mama yako alitaka kuitoa mimba yako. Na wahusika ni baadhi ya ndugu unao ishi nao. How will you react?

Iko hivi nakumbuka nilikuwa kwenye mahusiano na binti flani, tumuite Irene (siyo jina lake halisi), baada ya miezi kadhaa akawa amebeba ujauzito. Kwa mila na tamaduni zetu za kiafrika mtu mstaarabu inabidi ukajitambulishe kwenye familia husika, hivyo nikamtaarifu kuwa ninampango wa kutuma wazee. Kilichonishangaza sasa:oops:, alikataa akaniambia subiri kwanza, nilichukulia poa maana nilikuwa sijui ni nini kinaendelea.

Kumbe bwana huyu mdada alikuwa na mchumba anayefahamika mpaka nyumbani, hivyo mimi kwenda kujitambulisha ulikuwa mtihani kwake. Hiki kitu kilinistress sana, maana sasa sikuwa na uhakika na hiyo mimba ni ya kwangu au ya mchumba? Nihudumie au nisihudumie? Niikatae au niikubali? Duh . ila yeye alibaki na msimamo kuwa mimba ni yangu na huyo mchumba ni kwa sababu nyumbani wanamlazimisha kuolewa nae. Mwisho wa siku niliamua kumhudumia.

Sijui ni kukwepa aibu ama nini! Mama yake alianza kulazimisha mimba itolewe, ilikuwa ni vuta nikuvute, mimi nilimkomalia hakuna kutoa mimba, iwe yangu isiwe yangu hakuna kutoa(mtoto hana makosa). Yule mama alishafanya mpaka mpango kwa daktari mimba itolewe binti akagoma kwenda kutoa. Vidonge vya kutoa mimba vililetwa binti akagoma kumeza.

Kufupisha stori, I am a father of a beautiful daughter….very beautiful & intelligent. Juzi huyu binti (Irene)kanitumia video clip mama yake akifurahia kucheza na mjukuu wake(vicheko kama vyote) wakati alitaka kumuua (unafiki). Mjukuu anafurahia kujitupa kwenye miguu ya bibi yake laiti kama angejua kama she wanted her dead. I hope hakuna atakayemwambia , imagine ungekuwa wewe umetambua hiki kitu. How would you react?

Abortion is evil……..!
 
Mimba zinatolewa sana siku hizi yaan sana. So ashukuriwe mama wa mtoto maana hakuwa tayari kutoka moyon kuua mwanae,,wewe hukuokoa ila ulisaidia kuokoa(ila muhusika hakuamua kufanya ivo) .....kuhusu swali lako...acha kufufua makaburi mwache mtoto aliyeandikiwa kuishi,aishi kama watoto wengine bila background chafu.
 
Kwa mazingira niliyozaliwa na miaka hiyo, suala la utoaji mimba lilikuwa nadra, nikiambiwa hivyo sitaamini kwa asilimia nyingi sana.

Kwa kizazi hiki cha dotcom hili jambo ndio limeshika kasi.
 
Mimba zinatolewa sana siku hizi yaan sana.So ashukuriwe mama wa mtoto maana hakuwa tayari kutoka moyon kuua mwanae,,wewe hukuokoa ila ulisaidia kuokoa(ila muhusika hakuamua kufanya ivo) .....kuhusu swali lako...acha kufufua makaburi mwache mtoto aliyeandikiwa kuishi,aishi kama watoto wengine bila background chafu..
Siwez kufukua makaburi mkuu, mimi ni muumini wa upendo na amani
 
Sometimes you need to focus on now.

Past haisaidii zaidi ya kukutia roho mbaya tu na chuki.

Looking at now ndo unapojua kuwa kuna sababu Mungu alikuumba and no matter what challenges ulipitia you are here, Now so make the best of it.
That's it
 
Labda nione evidence ya video wakibishana, ila otherwise i wont care, it is what it is
 
Back
Top Bottom