Utabiri wa REDET na Uchaguzi Tanzania... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utabiri wa REDET na Uchaguzi Tanzania...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbu, Oct 30, 2009.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  KURA YA MAONI NAMBA 10:SEPTEMBA 2005
  MAONI YA WANANCHI KUHUSU UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2005
  [FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]CCM [/FONT][/FONT]
  [FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]75.4% [/FONT][/FONT]
  [FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman](979) [/FONT][/FONT]
  source; http://www.redet.udsm.ac.tz/documents_storage/2008-3-28-13-23-32_opinion%20poll%20sept2005%20swahili.pdf

  NA MATOKEO KAMILI YA URAISI 2005 YALIKUWA HIVI;

  Jakaya Kikwete
  Chama Cha Mapinduzi
  9,102,951
  80.28%

  ...Swali la kujiuliza ni je? Vyama vya Upinzani vimejiwekea mikakati gani kwa chaguzi za 2010-2015 kama kweli wanataka kuleta mabadiliko ya utawala wa Tanzania kuanzia kwa wabunge na wawakilishi,...maana kwenye uraisi hakuna matumaini kwa sasa!

  Ushindi wa asilimia zaidi ya 51 tu ya wabunge wakitoka CCM tayari bunge litakuwa limeelemewa na Chama Tawala...
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hilo la CCM kushinda hai hitaji kura za maoni kujua. Tanzania ina chama kimoja ambacho ndicho "hegemony" na vingine vina kua. Mpaka tuta kapo kua na vyama vingine ukiacha CCM vyenye uwezo wa kushinda basi kura za maoni kama hizi ndipo zitakua na maana.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Pamoja na utu uzima wa CCM hakika wakiingia ulingoni bila mabavu ya FFU , NEC kuwasaidia na wizi wa kura wanaweza kushangazwa kabisa . Redet wanajua hili miaka hii si ya mwaka 2005. CCM imejionea uchaguzi wa mitaa .Wameshinda sana ila hawawezi kutamba wanajua mbinu zao chafu na zina mwisho .
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,429
  Trophy Points: 280
  Yaani! nilitaka kuandika maelezo ambayo yanashabihiana sana na yako ;). Wa kulaumiwa katika hali hii pia ni vyama vya upinzani. Pamoja na kupewa mawazo ya bure na Watanzania juu ya umuhimu wa kuungana na kuunda chama kimoja chenye nguvu ili waking'oe chama cha mafisai madarakani bado wameweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Taifa.

  Wameshashindwa chaguzi tatu sasa za tangu tuingie katika mfumo wa vyama vingi, pamoja na kuwa kunakuwa na zengwe la wizi wa kura, vitisho na vipigo toka kwa matawi ya CCM aka vyombo vya dola, lakini hawakai chini wakatafakari wafanye nini. Labda baada ya kushindwa katika chaguzi 20 au zaidi za vyama vingi ndiyo wataona umuhimu wa kuyafanyia kazi mapendekezo ya Watanzania kuhusu umuhimu wa kuungana.
   
 5. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kwani wakiungana ndio watashinda bana!...vyama uchara vitajiondokea taratibu kwenye whole formula..kitu muhimu hapa ni civil education mfano..kudai katiba mpaya, tume huru ya uchaguzi kwa kutumia civil forums kama NGO, CBOna vyama vya upinzani
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kuunganba nadhani ni jambo jema ila si suluhisho.Mtaungana lakini watu hawaamini katika Muungano itakuwa ni bure .Elimu ya Uraia kwanza itawale kote na watu waelewe klwamba Upinzani na wapinzani ni Watanzania na si zaidi ya hapo . Hili ndilo muhimu na si kuunganisha vyama .Unawezaje kuwaamini CUF ukawaweka sawa na Chadema ? Jamani kuna ugumu hapo
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mkuu, mwenzako sina mashaka na ushindi wa CUF Zanzibar.

  Anyway,...ina maana wananchi hawana imani na vyama (vilivyopo) vya upinzani kwakuwa bado vichanga/vinakua na ndio maana 'tukubaliane' na hali ngumu zilizopo au?

  Bila vyama hivi 'vichanga' kupewa nafasi kwenye ngazi za chini mpaka Ubunge na uwakilishi, kweli tutaweza kuvipima uwezo wao?

  Ndio kusema Imani ya wananchi hasa asilimia 60-approx (ya wapiga kura) waliopo vijijini waendelee na imani hiyo hiyo tu kwamba maendeleo bila serikali ya CCM hayapo?

  Sijui wenye mawazo ya Upinzani wanayaonaje maoni haya, au nao ndio wameshakata tamaa kama wewe :)
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Oct 31, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,563
  Likes Received: 3,858
  Trophy Points: 280
  Well said

  Mwakani utashangaa Chadema na wenzao wanaingia kwenye uchaguzi huku katiba haijabadilika na tume ya uchaguzi siyo huru,

  wakati mwingine huwa nashangaa credibility za hivi vyama, unaingia kwenye ulingo ili hali unajua utashindwa , kama si kutaka ruzuku ni nini?
   
 9. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hayo ya katiba mpya na tume huru si yanapitishwa kwanza bungeni? sasa imagine zaidi ya 51% wataopiga kura ya kupinga ni wabunge wa CCM!...

  mabadiliko yanatakiwa yaanzie bungeni kwanza...
  Vyama vya Upinzani vielekeze nguvu kwenye kutwaa majimbo ya CCm kwanza ili kuupa nguvu upinzani Bungeni...

  Urahisi wa hili ni kumsimamisha mbunge mmoja wa upinzani anayekubalika na wananchi wa jimbo husika, badala ya wanavyofanya sasa kila chama kumsimamisha mgombea wake kupambana na mgombea wa CCM... watashindwa tu!

  wengine sijui ni hii Ruzuku inawasumbua?...:mad:
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Mkubwa,

  apart from CHADEMA, CUF na TLP kwa wapinzani sioni chama kingine kinachopiga kelele hadharani kwa sasa kupingana na CCM.

  Zitapofikia siku za chaguzi, vyama vyote vilivyolala utaona vinaibuka kama uyoga eti navyo vinakimbilia Ruzuku tayari kwa uchaguzi. Kama sio kuharibiana Kura ni nini?

  Kuna mambo mengine wala hayana haja ya kusubiri chaguzi 20 kuyabaini kwamba uchaguzi unahujumiwa kwa makusudi na hivyo vyama pandikizi sababu tu 'penye udhia inapenyezwa rupia!'...

  Wakemewe wenye vyama hivyo, na wananchi tujitokeze kuvipinga na kuvikataa hadharani! mfano; (matokeo yao hawa, eti walishindana na CCM kiti cha uraisi!)...


  Democratic Party -Kura 31,083
  0.27%

  PPT Maendeleo -Kura 18,783
  0.17%

  National League for Democracy -Kura 21,574
  0.19%

  Demokrasia Makini -Kura 17,070
  0.15%

  Sauti ya Umma -Kura 16,414
  0.14%

  Kama hayo yangekuwa matokeo ya darasani si wangekuwa wesharudishwa makwao hao? Wanatuletea utani wakati sisi wananchi tunaendelea kuteseka na matatizo lukuki nchini!
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu hakuna ugumu kabisa ktk kuunganisha Chadema na CUF isipokuwa wote wameingizwa mjini na UDINI.
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ubaya wenyewe huyo anayewaingiza mjini wanamjua na itikadi yake, sema wamemfumbia macho!...

  Tatizo kubwa lipo kwa CUF, Kila wakijaribu kujitoa kwenye rangi ya udini, wanapakwa rangi ya Upemba... Mpaka hapo watapoweza kujinasua kwenye rangi hizi ndipo 'Kinyonga' atapojulikana...
  kinyume na hapo Ushindi wao utaendelea kuishia Chumbe! Inashangaza chama hiki chenye wasomi kushindwa kuzuia 'propaganda' chafu hizi kiasi kwamba 'majority' wanaamini kweli CUF ni HIZBU!

  Ama kwa CHADEMA nawasifu kuweza kujinasua kwenye dhana enzi zile za Ukabila hususan Uchagga, mpaka sasa wanajionyesha sura ya utaifa zaidi...

  Vyama hivi vikiamua kuungana kiukweli, watamshinda adui anayewapaka rangi kwa propaganda za Ukabila, i.e walivyotaka kuwatumia watu wa Musoma dhidi ya Kilimanjaro hususan kwenye zengwe la Mar Chacha Wangwe nk...

  UMOJA NI NGUVU, ...Upinzani hawajalijua hilo (?)
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu kwanza hizo kura za maoni za REDET siziamini sana mpaka hapo nita kapo jua size ya sample ilikua ni ngapi, maswali gani yaliulizwa na ni watu wapi haswa wameulzwa.

  Mimi nadhani vyama vya upinzani lazima vijijengee jina haswa in rural areas ambapo ndiyo asilimia kubwa ya wapiga kura wapo. Kama umegundua kelele nyingi za ufisadi nk zina toka kutoka population za mijini ambapo wana access na habari mbali mbali. Hivi haujiulizi kwa nini watu wana piga kelele lakini bado CCM inashinda? Kwa sababu sisi tunaopiga kelele tuna represent asilimia ndogo sana ya wapiga kura wote.

  Sawa labda CCM ina fanya faulo za hapa na pale lakini siamini kabisa kwamba kuna chama cha upinzani kina uwezo wa kuchukua idadi kubwa ya wabunge na uraisi. Kwa huko Z'bar sijui....
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Divide and conquer seems to work well for CCM.
   
 15. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  Na hilo jukumu la kutoa civil education ni la nani kama siyo vyama vya upinzani? Tuwe wakweli bwana nani atampa advantage mpinzani wake? CCM na serikali yake lazima inajua kuwa civil education will work against them so usi tegemee hata siku moja wao wataipa kipaumblele.
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kwa mujibu wa hiyo link wanasema hivi;

  ...Mkubwa, huko Zanzibar hasa Pemba CCM wanapelekeshwa mchakamchaka kila chaguzi! Kukubalika kwa Upinzani hakutokani na Uwezo pekee wa kushinda, ni pamoja na kukubalika vilevile...

  Kwa mfano, jiulize kwanini katika wilaya ya Temeke tu hapa Dar CCM inapelekeshwa mchakamchaka iwapo (CCM) wanakila uwezo wa kushinda -wakitaka! ...si kuwajengea tu mabarabara, maji, umeme wa uhakika nk 'labda' wananchi watawakubali?...
   
 17. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu CCM kushinda mimi nime maanisha kushinda kiujumla kama kuwa na majority bungeni na kushinda uraisi. Siku maanisha hata kidogo kuwa watashinda kila jimbo.....that's impossible. Hilo swala la barabara, maji nk nakubaliana na wewe but I seriously doubt it kwamba upinzani ungeingia wangeweza pia kufanya yote hayo. Anyway ni mtazamo tu tuendelee kujadiliana.
   
 18. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,689
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Jamani,

  Mimi nimepata funzo kutoka kwenye uchaguzi wa vitongoji/mitaa; sikuwa nawasikia CHADEMA, CUF etc... In fact akina CHADEMA walikuwa busy na kujitafutia masifa binafsi! Kama walivyo vinara wawili wanaopenda majisifaaaa.... yet hawakisaidii chama.
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hawataweza kufanya yote lakini angalau wanaweza kutoa changamoto yafanyike angalau nusu ya haya...


  Ufisadi kwenye ununuzi wa Radar, Umeme wa Richmond, Mkataba wa Mgodi wa Buzwagi, Tuhuma za EPA,... na mengineyo yameibuliwa machoni mwa watanzania kwa juhudi binafsi za wabunge wa Upinzani.


  Tatizo lililopo sasa, baada ya kuibuliwa hayo hatua gani zinachukuliwa kwa wahusika? kwa walio wepesi kusahau, kuna maneno 'matamu-matamu' yalitamkwa;

   
 20. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #20
  Oct 31, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM kamwe hawawezi kubadilisha katiba au kuweka tume ya uchaguzi iliyo huru kwa hiari yao. Hawako civilized kiasi hicho. Lakini yapo mambo mawili ambayo yatawezesha hayo kufanikiwa. Moja, ni kuingia kwenye uchaguzi hivyo hivyo na kupambana nao kwa muda mrefu, kujijenga na hatimaye kuwa na viti vingi bungeni. Halafu kujenga hoja bungeni mpaka wabunge wa CCM wenye hekima kuiunga mkono hiyo hoja, tupate kura za kutosha, katiba ibadilishwe. Au wafadhili kuwalazimisha kuwa na uchaguzi uliyo huru kama tulivyolazimishwa kuachana na siasa za chama kimoja na kuwa na siasa za vyama vingi. Sasa hatuwezi kukaa na kusubiri wafadhili, inabidi tupambane nao hivyo hivyo. Juhudi zikionekana, wafadhili wakaingilia, mchakato utaharakishwa.

  Jukumu la kutoa civil education ni LAKO, langu, la mashule yetu, asasi za kijamii, TAMWA, HAkielimu, madhehebu ya dini, vyama vya wafanyakazi, kwa ujumla ni letu sote wenye uchungu na nchi hii. Vyama vya siasa vitoe hiyo elimu kwa uwezo upi? Inahitajika pesa, itoke wapi?

  .
   
Loading...