Utabiri wa mrithi wa Shekhe Yahaya..

kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
8,132
5,785
Mrithi wa aliyekuwa mtabiri na mganga wa kienyeji marehemu Shekhe Yahaya Hussein, Hassan Yahaya ametabiri mambo mbalimbali yatakayotokea mwaka 2014,kubwa amesema ametabiri kiongozi mkubwa wa chama cha siasa atang'olewa katika nafasi yake.Pia kasema hatua hiyo itamsababishia anguko kubwa la kisiasa kiongozi huyo.Pia kasema rais Kikwete kwa mwaka huu atafanya jambo kubwa ambalo litamjengea heshima kubwa kitaifa na kimataifa.Kaongezd mwaka 2014 sio mzuri kwa viongozi wa kidini.my take:mgogoro wa CDM na ZITTO ndo umepelekea utabiri huu au kuna kiongozi mwingine mkubwa wa chama cha siasa?
 
Teh teh teh!mkuu hamkupata muda wa kumuuliza maswali?
 
Huyu si mtabiri kabisa anasoma alama za nyakati halafu anajifanya katabiri. Nani hajui kwamba Kikwete anapaswa kuteua mawaziri kujaza nafasi zilizoachwa wazi na hao waliolazimika kujiuzulu na mmoja kufariki dunia? Zitto inafahamika kabisa kwamba anguko liko mlangoni kwake anasubiriwa kufungua mlango limuangukie. Atabiri nani mgombea urais kupitia CCM?
 
Hapo kwenye mwaka 2014 sio mzuri kwa viongozi wa dini tunatengua unabii wake kwa damu ya YESU. Mungu ndiye mwenye jibu la mwanadamu. Wakati mwanadamu anakuwazia mabaya Mungu anakuwazia mema. Kama unaamini sema inshaalah au AMINA.
 
Mrithi wa aliyekuwa mtabiri na mganga wa kienyeji marehemu Shekhe Yahaya Hussein, Hassan Yahaya ametabiri mambo mbalimbali yatakayotokea mwaka 2014,kubwa amesema ametabiri kiongozi mkubwa wa chama cha siasa atang'olewa katika nafasi yake.Pia kasema hatua hiyo itamsababishia anguko kubwa la kisiasa kiongozi huyo.Pia kasema rais Kikwete kwa mwaka huu atafanya jambo kubwa ambalo litamjengea heshima kubwa kitaifa na kimataifa.Kaongezd mwaka 2014 sio mzuri kwa viongozi wa kidini.my take:mgogoro wa CDM na ZITTO ndo umepelekea utabiri huu au kuna kiongozi mwingine mkubwa wa chama cha siasa?
Believe this and you will believe that you can be killed by your own trousers!
 
[h=1]WAGANGA NA WANAJIMU MARUFUKU KUJITANGAZA[/h] VYOMBO vya habari vya utangazaji vimepigwa marufuku kurusha matangazo yanayohamasisha biashara ya waganga wa kienyeji na wanajimu ambao ni maarufu kama watabiri wa nyota.

Hatua hiyo imo kwenye rasimu ya kanuni za Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta ya mwaka 2010 (EPOCA) wakati zikijadiliwa Dar es Salaam jana na wadau mbalimbali ili kuziboresha.

Kwenye kanuni hizo katika kifungu kinachoelezea
mambo ya kuepuka katika vipindi vya redio na televisheni mojawapo ni la kuhakikisha vipindi vinavyohamasisha waganga wa kienyeji na wanajimu havipewi nafasi.

Licha ya baadhi ya wadau kuhoji kwa kina suala hilo, Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasialiano (TCRA) ilitoa msisitizo kuwa matangazo ya aina hiyo kwenye vyombo vya utangazaji vinavyopewa leseni na mamlaka hiyo ni marufuku.

Akifafanua kifungu hicho, Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Habib Gunze, alisema ni hatari kwa Taifa, iwapo vyombo vya utangazaji vitahamasisha tiba zinazotolewa na waganga wa kienyeji na masuala ya utabiri wa nyota.

"Kwa nini utangaze biashara ya waganga wa kienyeji, mbona hatujawahi kuona hospitali kama Muhimbili zinajitangaza, kama wanatoa tiba za kweli, hizo tiba zao ndizo zitakazowatangaza na si kutumia vyombo vya habari," alisema Gunze wakati akijibu swali la mmoja wa wadau waliotaka ufafanuzi katika eneo hilo.

Gunze alifafanua kuwa vyombo vya habari hasa vya utangazaji, vina jukumu la kulinda wananchi "leo hii mtu anajitangaza mimi ni Daktari bingwa wa kutibu magojwa sugu kama … niko Mwanza hoteli chumba namba fulani, mtu akienda na asipone au akipata madhara itakuwa mbaya kwa vyombo vya utangazaji? Alihoji Gunze.

Hoja hiyo iligusa wajumbe wengi na mdau kutoka Radio Iman ya Morogoro, alihoji kuwa vituo vyao vimekuwa vinatumia baadhi ya watabiri na wataalamu wengine wa mambo ya tiba naye akataka ufafanuzi kuhusu suala hilo.

Mkurugenzi wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Joyce Mhaville, naye alishauri kuwa suala hilo liangaliwe vizuri na akashauri kuwa vipindi ambavyo vinatakiwa kupigwa marufuku, viwe ni vile ambavyo vinawataja waganga hao kuwa mabingwa wa kutibu magonjwa fulani wakati si kweli.

"Sisi Watanzania tuna utamaduni wetu, miaka yote magonjwa mengine kwa hapa nchini yamekuwa yanatibiwa na dawa za miti shamba, kwa hiyo nashauri tuwe makini na suala hili," alisema Mhaville.

Akifafanua suala hilo, Gunze alisisitiza kuwa vipindi na matangazo ya waganga wa kienyeji na watabiri hayataruhusiwa kwenye vyombo vya utangazaji.

"Tuna mifano vyombo vya habari vimehamasisha sana suala la Samunge (kikombe cha Babu Loliondo) na matokeo yake tunajua kuna watu wamepata matatizo."

Ila alisema wanachoweza kuruhusu ni kama kuna mtaalamu wa miti shamba ambaye anaweza kuzungumza kwenye vipindi, kuwa magonjwa kama saratani licha ya kutibiwa hospitalini, pia inaweza kutibiwa na miti shamba ambayo ataitaja majina.

Pia alisema miti shamba hiyo iwe imethibitishwa na taasisi za kitaalamu kama Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na nyinginezo zinazohusika na utafiti wa dawa za asili.

"Tusipofanya hivyo, huyu mtu tunayemtangazia akienda huko kwa mganga bingwa na sipo, ni tatizo … kutangaza biashara ya waganga wa kienyeji hairuhusiwi."

Baadhi ya matangazo maarufu ya uganga yanayorushwa kupitia televisheni nchini ni pamoja na la dawa ya vidonda vya tumbo, maarufu Fiterawa, na yanayoendeshwa na Dk . Issack Ndondi.

Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta ya Mwaka 2010 (EPOCA) ilipitishwa na Bunge Januari mwaka jana na kufuta sheria mbili: Sheria ya Utangazaji namba 6 ya Mwaka 1993 na Sheria ya Mawasiliano Tanzania namba 18 ya mwaka 1993.

Kwenye kanuni hizo pia vyombo vya utangazaji wakati wa uchaguzi vinalazimishwa kutoa haki sawa kwa vyama vyote vya siasa na wagombea wao wa udiwani, ubunge na urais. Vyombo hivyo pia vinakatazwa kutoa waandishi wao wa habari kugharimiwa na wanasiasa kwenye kampeni.

Gunze katika eneo hilo, alisema sheria inawataka ambao wanaanzisha vyombo vya utangazaji kuhakikisha wana uwezo kifedha kugharimia wanahabari wao wanaokwenda nje ya kituo cha kazi.

"Sasa wewe umeanzisha televisheni au redio huna hata fedha za kuwagharimia wafanyakazi wako wanapokwenda nje ya kituo cha kazi … sheria inakataza hali hiyo."

Pia katika kanuni hizo, umiliki wa vyombo vya habari utaruhusu raia kumiliki asilimia 51 na raia wa kigeni kumiliki asilimia 49 kwa ambao watapenda kuingia ubia. Gunze alisema ni hatari kwa Taifa kuruhusu wageni kumiliki vyombo vya habari vya utangazaji kwa aslimia 100.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkhoma, alisema katika mfumo wa utangazaji wa dijitali, mamlaka yake inaangalia uwezekano wa vyombo vyote vya utangazaji kutumia king'amuzi kimoja kurusha matangazo yao kuliko ilivyo sasa kuwa na ving'amuzi vingi.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi, akifungua mkutano huo wa wadau, alivitaka vituo vya utangazaji kuhakikisha vinafuata maadili na akatoa mfano kuwa kuna malalamiko kwamba baadhi ya televisheni zinarusha matangazo mchana yakikiuka haki za watoto.

Pia alivitaka vituo hivyo kuwa vibunifu na kuhakikisha kuwa vipindi vyao vingi vinakuwa katika lugha ya Kiswahili, ambayo ndiyo lugha ya Taifa.
 
Well Well said.... Remo' hebu waelimishe majahili !

Mkuu najiuliza sana, kwani huyu bwana na mwanae waitwe mashekhe????
...
Sababu ni kuwa Quran imeweka wazi, kupiga ramli ni haramu!
Sikumbuki ni aya gani! But kuna aya inasema:
'hakuna aijuae kesho'
sasa kama hawa mabwana wanapingana na Quran huo ushekhe wameupatia wapi?
 
Kwa heshima zote kwako Masha' Ukitazama historiya ya madajali ( swindler/impostor ) wengi wao hutumia mgongo wa dini na wingi wa upofu wa waumini ( innocents/illiteracy) ili wajinasibishe kama wasomi au wataalamu juu ya ilmu ya Kitabu. Ofcoz Mkuu kuwa sheikhe mwenye Elimu ni lazima uhitimu masomo ya FEEQh (fikih), SHERIA, TAWHID na LUGHA hapo unatunukiwa usheikhe...na huwa inaResponsibilities nyingi kiutendaji.
Sasa wakuu hawa huwekaga masilahi yao mbele na kujipa Umaarufu bila kujali dhimaa za UPOTOSHAJI,UBABAISHAJI,PROPPAGANDA,DHAMBI ilimradi anawaliwaza wafuasi (Mass) !! very sad and Shame to the faith of Islam.
Binafsi ninawaombea Msamaha na Istigh-faar kwa Moula-karim.AMIN
Oh God forgive them.
 
Mrithi wa aliyekuwa mtabiri
na mganga wa kienyeji marehemu Shekhe Yahaya Hussein, Hassan Yahaya
ametabiri mambo mbalimbali yatakayotokea mwaka 2014,kubwa amesema
ametabiri kiongozi mkubwa wa chama cha siasa atang'olewa katika nafasi
yake.Pia kasema hatua hiyo itamsababishia anguko kubwa la kisiasa
kiongozi huyo.Pia kasema rais Kikwete kwa mwaka huu atafanya jambo kubwa
ambalo litamjengea heshima kubwa kitaifa na kimataifa.Kaongezd mwaka
2014 sio mzuri kwa viongozi wa kidini.my take:mgogoro wa CDM na ZITTO
ndo umepelekea utabiri huu au kuna kiongozi mwingine mkubwa wa chama cha
siasa?

zzk tayari ameshaangushwa na jk tayari amethubutu kuleta katiba mpya
 
Huyu si mtabiri kabisa anasoma alama za nyakati halafu anajifanya katabiri. Nani hajui kwamba Kikwete anapaswa kuteua mawaziri kujaza nafasi zilizoachwa wazi na hao waliolazimika kujiuzulu na mmoja kufariki dunia? Zitto inafahamika kabisa kwamba anguko liko mlangoni kwake anasubiriwa kufungua mlango limuangukie. Atabiri nani mgombea urais kupitia CCM?

Ha ha ha anatafuta pa kutokea huyu.. Na kwa jinsi hao waliokuwa wanashirikiana na baba yake walivyo wajinga utasikia anakaribishwa mpaka ikulu huyo..
 
Mrithi wa aliyekuwa mtabiri na mganga wa kienyeji marehemu Shekhe Yahaya Hussein, Hassan Yahaya ametabiri mambo mbalimbali yatakayotokea mwaka 2014,kubwa amesema ametabiri kiongozi mkubwa wa chama cha siasa atang'olewa katika nafasi yake.Pia kasema hatua hiyo itamsababishia anguko kubwa la kisiasa kiongozi huyo.Pia kasema rais Kikwete kwa mwaka huu atafanya jambo kubwa ambalo litamjengea heshima kubwa kitaifa na kimataifa.Kaongezd mwaka 2014 sio mzuri kwa viongozi wa kidini.my take:mgogoro wa CDM na ZITTO ndo umepelekea utabiri huu au kuna kiongozi mwingine mkubwa wa chama cha siasa?

Naye kaanza kutumiwa kama baba yake. Hamna lolote.
 
Mim pia ni mtabiri
"tazama mwezi huu hautaisha jk atasafiri kwenda nje ya nchi mara 3"
 
Kwa heshima zote kwako Masha' Ukitazama historiya ya madajali ( swindler/impostor ) wengi wao hutumia mgongo wa dini na wingi wa upofu wa waumini ( innocents/illiteracy) ili wajinasibishe kama wasomi au wataalamu juu ya ilmu ya Kitabu. Ofcoz Mkuu kuwa sheikhe mwenye Elimu ni lazima uhitimu masomo ya FEEQh (fikih), SHERIA, TAWHID na LUGHA hapo unatunukiwa usheikhe...na huwa inaResponsibilities nyingi kiutendaji.
Sasa wakuu hawa huwekaga masilahi yao mbele na kujipa Umaarufu bila kujali dhimaa za UPOTOSHAJI,UBABAISHAJI,PROPPAGANDA,DHAMBI ilimradi anawaliwaza wafuasi (Mass) !! very sad and Shame to the faith of Islam.
Binafsi ninawaombea Msamaha na Istigh-faar kwa Moula-karim.AMIN
Oh God forgive them.

Well said Mkuu! Naweza kusema waislamu tuliowengi Tz, hatujui dini (waislamu jina) ndio sababu washirikina kama Shehe Yahaya hawapati upinzani!
...
Sijui nani tumchune ngozi!
 
asante kwa ufafanuzi mzuri
 
Well said Mkuu! Naweza kusema waislamu tuliowengi Tz, hatujui dini (waislamu jina) ndio sababu washirikina kama Shehe Yahaya hawapati upinzani!
...
Sijui nani tumchune ngozi!
Ngduguyangu FYI, hizi ni hulka za binaadamu wewe chunguza utaona hata wanaSiasa wao na watoto wao hujirithisha kinamna !! ata kama elimu ndogo... Utakuta kuna mgongo umesha inama kama DARAJA (bridge) hutimika kwa umaarufu wa fulani " sasa Binaadamu akipata wafuasi huanza na zake hapo sasa" Umashuhuri unajipamba vilivyo.
 
Back
Top Bottom