UTABIRI: Vipers vs Simba & Real Bamako vs Yanga

CARDLESS

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
7,786
15,732
Wadau wa michezo, weekend hii tutashuhudia game za kibabe katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika sambamba na ile ya Kombe la Shirikisho.

Pamoja na kuwa game nyingi ila hapa mimi nitajikita katika kutabiri game mbili tu, hasa zinazotuhusu sisi Watanzania. Utabiri huu utazingatia zaidi hali ya vikosi, mbinu, mwendelezo wao nk.

Mechi hizi ni muhimu sana kwa klabu zetu za Tanzania (Simba & Yanga).

Mjini Entebbe kutakuwa na game ya kukata na shoka kati ya Vipers vs Simba, game hii itatoa taswira halisi juu ya vibonde hao wa kundi hili la C kwenye Klabu Bingwa. Ndio ni vibonde kwa maana wote wanapumulia mashine.

Mechi ni ngumu kwa pande zote mbili na hii inachagizwa na mechi ya Raja vs Horoya, na hapa naweka rekodi sawa, Raja kila anapokutana na Horoya basi hali yake huwa mbaya, na always kila mmoja hushinda awapo kwao. Hivyo kundi linaonekana wazi hadi kufikia game za 4 kila mmoja basi Raja atakuwa na point 9, na Horoya point 7.

Tuje kwenye mechi yetu hii sasa, hii mechi kila mmoja anaona ndio pa kupatia point, yaani Simba anaona yeye atapata point kwa kibonde Vipers lakini pia Vipers wanaona watajizolea point kwa kibonde Simba.

Hii mechi kama Simba itaanza na wachezaji hawa (Sakho Chama, Saido, Baleke, Phiri, Bocco) kwenye safu yake ya juu, basi bila shaka yoyote Simba anaenda kupasuka hii game.

Kwanini? Simba itabakiwa na wachezaji 7 ambao ndio wafanyaji kazi pindi ambapo watakapokuwa hawana mpira, hiyo cream yote ya mbele hakuna anayeweza kushuka kusaidia timu, na pia umri sambamba na majeraha ya baadhi yao kuwafanya kutomudu matumizi makubwa ya nguvu.

Simba ifanye nini ili kukabiliana na hili?

1. Kapombe acheze namba 7 (winga) ya kulia, huku beki namba 2 akiachwa bwamdogo Mwenda. hii itasaidia sana timu kuzuia na kushambulia kwa wakati na kwa umoja mkubwa sana.

2. Chama acheze nyuma ya mshambuliaji yaani acheze namba 10, huku Saido akianzia Benchi na nafasi yake ikichukuliwa na Kapombe.

3. Kushoto asimame Kibu D, yes Kibu D, hapendwi ila binafsi kama mtu wa mpira namkubali kwa maana anakuoffer vitu vingu ukilinganisha na Sakho. hapa upande huu utakuwa Safe kwa maana una Shabalala na Kibu D na itakuwa ngumu kwa Vipers kutumia staili yao ya kaunta.

4. Viungo. Kipande hiki Simba kama wanataka kuwin game kwa urahisi wanapaswa kuwatumia Sawadogo + Kanoute yes hiyo combo ni rahisi kukupa matokeo kwa sababu imechanya nguvu na utulivu. Pamoja na upole wa Sawadogo ila ni mtu ambaye hapotezi mipira hovyo ukilinganisha na Mzamiru.

5. Juu pale asimame Kyombo.

Sina shaka na beki za kati za Simba.

Kama Simba watatumia mbinu ya kuwachosha Vipers kupitia pembeni kama nilivyshauri nawaona wazi wakichomoza na ushindi si chini ya Magoli 3.

Utabiri, Kutegemeana na Upangaji wa kikosi, kama Simba itaamua kuanza na mmoja kati ya Chama, na Saido basi nawapa ushindi wa 2-1 tofauti na hapo nawapa Vipers ushindi wa 1-0 au 2-1.

Upande wa Bamako kule Mali.

Hawa jamaa Real Bamako wanasifika kwa kupiga pasi nyingi, ni timu yenye uwezo mkubwa wa kumiliki Mpira, vimo vya wachezaji wao, lkn pia katika game zao 10 wako nafasi ya 2 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Yanga inatakiwa kuwaje?
Shida kubwa ya Yanga ni Eneo la Washambuliaji wa pembeni, eneo hili limekuwa na watu ambao kama uyoga yaani hawaeleweki muda upi watakupa kitu sahihi. Lakini pia Nadi ana shida ya kujaribu sana eneo la mabeki, unaweza kuta game hii Kibwana na ile hakuanza, yaani ni ngumu kujua ataanza nani.

Yanga anahitaji alama 3 hizi kwani itamfungulia njia kwa namna kundi lao lilivyo ushindi wowote wa Yanga basi ataongoza kundi lake, ni kwa sababu Mazembe na Monastir lazima Mazembe ashinde au iwe SARE hakuna namna Monastir atashinda hiyo mechi.

Yanga wapaswa kuanza na kikosi kama ifuatavyo (nitaweka maeneo muhimu tu).

1. Mbele, mechi hii ni ngumu na inahitaji ulazima wa kushinda hivyo Nabi anatakiw kuanza na Musonda, asimame kushoto, Kisinda asimame Kulia, juu amuweke Aziz KI (10) na Namba 9 asimame Mayele. hii ni kutokana na balansi ya hizo Njemba za Bamako. watu kama Moloko wanafaa kuongia Game inaelekea mwisho.

2. Viungo, Aucho namba 8 Na Bangala na 6.

3. Eneo la mabeki ni muhimu sana, na kwa nguvu wanayotumia hawa Bamako basi Djuma, Job, Mwamnyeto na Faridi (asimame namba 3) tunaweza wamudu na hatimaye kuondoka na alama.

Utabiri kwa game hii, kama plani ya Nabi itaelekea na nilivyowaza basi Yanga anaenda kushinda 2-1.

Tofauti na hapo Bamako wanaenda kuchukua alama zote 3.

Utabiri wa Jumla:
Vipers 1-2 Simba
Bamako 1-2 Yanga
 
It's either Nakivubo Kampala or Nambole in Mukono the outskirt of Kampala, not Entebbe labda kama vipers wana uwanja wao
 
Natoa shilingi mkuu.

Simba anampasua Vipers 2 bila majibu
Na Yanga anakufa 3 kwa moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom