Utabiri kwa uongozi wa Rais Magufuli

Utabiri kwa uongozi wa Rais Magufuli

utaburi mzuri huu na ni bora kuliko kuota ndoto
 
Natabiri rais wangu John Pombe Magufuli atapata mtikisiko mkubwa ndani ya utawala wake.

Mh Magufuli katika uongozi wake umekuwa wakukimbia tatizo badala ya kulitatua.

1. Hajajenga mazingira mazuri kibiashara: kodi TRA- imekuwa sio rafiki.
biashara zime dorora.wafanya biashara wakiongea/

mh Magufuli:"mlikuwa wapiga dili"wafanya biashara wamekaa kimyaa (bomu linachemka)

2. Walimu: Hakuna uamisho, hakuna niongeza, hakuna kupanda daraja, walimu waliomaliza hakuna ajira.

Mh magufuli: "subirini tumalizane na wafanya kazi hewa"walimu wamekaa kimyaa (bomu linachemka)

3. Wanainchi wanalalamika njaa

Magufuli:"serekali haina shamba"

wanainchi wamekaa kimya ( bomu linachemka)

4. Ajira kwa ujumla. vijana wakapata moyo na milion 50 kila kijiji. milion 50 hakuna vijana wa watoto masikini wametulia mtaani kuzurura nakushabikia mpira na ishu ya madawa ya kulevya.

Magufuli; " vijana jiajirini hapa kazi tu"

Vijana wamekaa kimya(bomu linachemka)

5. Watumishi wa umma: Hofu imewatanda wanafanya kazi kwa hofu bila kuwa na utaratibu maalumu, matamko yanafanya watumishi kushindwa kufanya kazi kwa utaratibu.

Magufuli: " narudisha nidhamu"

Wamekaa kimyaa sio kwamba wanafurahia ni shida tu" bomu linachemka"

6. Bank na wateja wao: ongezeko la vat '

Wamekaa kimyaa: "bomu linachemka"

7. Timua timua ya wanafunzi chuo. TCU waliwapokea leo hawana vigezo,
mikopo shida.

Wamekaa kimya: "bomu linachemka"

8. Machinga

Magufuli: " mtu asiwaguse"

mikoa mingi wamepewa taarifa hawatakiwi barabarani bila kupangiwa sehemu rafiki, mfano mzuri yaliotokea Mwanza.

Machinga wako kimyaa " bomu linachemka"

Sijagusia:

Polisi.
Wanasiasa( wapinzani)
Utalii.
Viwanda.
NSSF
Wakulima
Makusanyo ya mapato.
Bunge
Makundi ndani ya chama chako.

Tahadhari mh Magufuli kukimbia tazizo sio njia ya kutatua tatizo. unatengeneza mabomu mengi sana.

Wanakuvumilia na siku zote uvumiliza una mwisho wake

Usipochukua hatua natabiri mtikisiko mkubwa ndani ya utawala wako.
Kwa kifupi mabomu yana chemka!!!
 
Sisi wenye jicho la pili(ukiondoa macho ya kawaida)tunaona mambo mengi sana tena sanaaa lkn kutakua na mabadiliko na yataletwa na Mungu mwenyewe.Mungu anawaona maskini wa nchi hii wanaoteseka na atawasaidia!
 
[emoji16] Mleta uzi unaongea ukweli kama utani vile, lakini tunapaswa kua na subra maana kulikua na matundu mengi sana ngoja wamalizie kuyaziba wenyewe tutafurahi[emoji12]
MTU anaelekea Hatarini hatakiwi kutiwa moyo Bali asaidiwe kutambua hali ya hatari inayoweza kutokea wakati wowote punde. msaidie mkulu maana nchi hii ni yetu sote
 
hata msemeje magufuli hatawaachia muuze madawa ya kulevya tena. Imekula kwenu na hizi dili zenu fake. Wakati Wa jk watu walikuwa wanaumia zaidi Ila kikudi kidogo ndo kinaenjoy mjini wacha magufuli awanyooshe wotetule tule kwa jasho siyo nyie mnakula kilaini tu

Hilo ndio tatizo.

Mwanzo mtu aliyekuwa anapinga serikali alikuwa ni fisadi, sasa hivi anakuwa ni muuza madawa.

Hebu kaa chini angalia mfumuko wa bei wa vyakula vya kila siku kama Sembe, Maharage na Mchele. Fananisha bei ya mwanzoni mwa mwaka jana na Leo.

Inawezekana bado unakula kwa mama, lakini muulize mama tofauti ya bei ndio utajua kwa nini watu wanalalamika.
 
Hilo ndio tatizo.

Mwanzo mtu aliyekuwa anapinga serikali alikuwa ni fisadi, sasa hivi anakuwa ni muuza madawa.

Hebu kaa chini angalia mfumuko wa bei wa vyakula vya kila siku kama Sembe, Maharage na Mchele. Fananisha bei ya mwanzoni mwa mwaka jana na Leo.

Inawezekana bado unakula kwa mama, lakini muulize mama tofauti ya bei ndio utajua kwa nini watu wanalalamika.
Tatizo mliamimishwa na wapinzani kuwa siasa ndo chakula nchi nzima ikageuka siasa watu hawalimi tena kwa hiyo matatizo tuliyategemea kwa SBB ya ujinga wenu.

Watu wakilima na kufanya kazi kama magufuli anqvyotaka bei mwakani zitapungua sana. Bei za vitu hazipunguzwi kwa maneno kama ambavyo mnataka kuwaaminisha watuanyumbu nyie
 
Maneno kuntuuu baba umesahau moja tu hapo makato ya bodi ya mikopo kutoka asilimia 8% kwenda 15% wakati kunawatumishi wana1/3 ya mshahara ilonalo bomu wataishi kama mashetani
 
Alafu enhee!! Huo msamiati ni kichekesho, kuna mwaka fulani tulikuwa tunaelekea uchaguzi mkuu, kuna mama mmoja alikuwa jukwaani akisema nchi fulani imepinduliwa sio raisi kuichukuwa kwa makaratasi, nani anachochea.
 
Kuna mambo ya kusahihisa kidogo kwa sababu hivi sasa ichi inaendeshwa kama nchi ya kijamaa kumbe ni "free market". Sekta binafsi ina utaratibu wa ku control production na ufanisi. angalia mfano wa shule binafsi. Mwenye kiwanda hamsubiri waziri wa kazi kuhimiza kazi! serikali inamkamua kodi na yeye anakamua nguvu kazi.
Hivi kwa mfano, kuna sababu gani kuwaamuru watu wa Dar wasinywe pombe mchana wakati wakazi wengi wako sekta binafsi na sidhani kama waajiri kule wanataka walevi!
Katika soko huria kanuni ni "Survival of the Fittest" mzembe atajifia mwenyewe
Kwa hivi leo hii jukumu la kila mwajiri ni kusimamia eneo lake kikamilifu.
Kazi ya serikali ni kujenga nidhamu ya watumisshi wake kwani wao ndio hutoa huduma kwa sekta binafsi. katika hili serikali inatimiza wajibu wake.
Pili kazi ya serkali ni kuweka sera rafiki ili sekta binafsi iweze kutoa mchango wake halisi.
Kosa linalojitokeza sasa ni kujaribu kutekeleza sera za kijamaa huku mfumo uliopo ni wa kibepari. Ziko amri nyingi ambazo zilitumika enzi za kujenga ujamaa mfano hili la usafi Jumamosi katika jiji kubwa la kibiashara kama Dar.
Kuanzia saa moja hadi saa nne hakuna biashara, hakuna faida lakini kodi iko pale pale! kwani hakuna njia nyingine?
Basi tuseme moja tu kwamba tumeamua kurudi kwenye ujamaa ieleweke kwa sababu tunaegemea mno kwenye state cntrol for everything na hii inaleta shida.
 
Kama umetaja mapungufu yake, basi na utaje na mazuri yake.

Ndio kwanza ana mwaka mmoja na miezi, mpeni muda.
 
Kauli ya kikwete.. Tumeleta chuma sasa, kina nguvu kweli kweli,,,pale nilipokwenda pole pole chuma kitakwenda kwa kasi zaidi na tayari kimeanza kutema checheeeee!!!!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Anko Magu bhanaaaaaa sio wa mchezo mchezo yani yeye ana deal na wapiga dili
 
Back
Top Bottom