KUTATABHETAKULE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 5,456
- 5,462
Kwa maana hiyo hujaelewa?????mkuu umenifanya nicheke sana. unataka kusema polisi hawajitambui???
Mkuu,
Pengine wewe ungekabidhiwa PAGALA sasa hivi ili uishi ndani yake, nini ungewaza cha kwanza, kukarabati pagala hilo au KULIVUNJA na kuanza ujenzi wa nyumba mpya utakayoishi ikiwa uwezo unao wa kufanya hivyo?
Ukiamua kukarabati, ipo siku itakuangukia kwakuwa kuna maeneo hutoweza kukarabati na yanaendelea kuoza au kila mara utagharamika mara dufu kwenye ukarabati, gharama ambayo ungeweza kuanza moja tu.
Ukiamua kuvunja, wakati unapoanza kuvunja hakuna atakayejua unataka kujenga nyumba ya namna gani, utakapoanza kuweka boma, pole pole watasema, "nyumba kubwa sana ile halafu ina complications", ukishapaka rangi wataisifia na kusema, "jamaa kajipinda haswaaa, ile sasa ndio nyumba". Ila sidhani kama itakuchukua siku moja kufikia kusikia maneno hayo.
Tuwe na subira.
hapo kuna hatari ya kuambiwa ni lugha ya uchochezi
I can be a President of united republic of Tanzania!What can you be?
[emoji16] Mleta uzi unaongea ukweli kama utani vile, lakini tunapaswa kua na subra maana kulikua na matundu mengi sana ngoja wamalizie kuyaziba wenyewe tutafurahi[emoji12]
Natabiri rais wangu John Pombe Magufuli atapata mtikisiko mkubwa ndani ya utawala wake.
Mh Magufuli katika uongozi wake umekuwa wakukimbia tatizo badala ya kulitatua.
1. Hajajenga mazingira mazuri kibiashara: kodi TRA- imekuwa sio rafiki.
biashara zime dorora.wafanya biashara wakiongea/
mh Magufuli:"mlikuwa wapiga dili"wafanya biashara wamekaa kimyaa (bomu linachemka)
2. Walimu: Hakuna uamisho, hakuna niongeza, hakuna kupanda daraja, walimu waliomaliza hakuna ajira.
Mh magufuli: "subirini tumalizane na wafanya kazi hewa"walimu wamekaa kimyaa (bomu linachemka)
3. Wanainchi wanalalamika njaa
Magufuli:"serekali haina shamba"
wanainchi wamekaa kimya ( bomu linachemka)
4. Ajira kwa ujumla. vijana wakapata moyo na milion 50 kila kijiji. milion 50 hakuna vijana wa watoto masikini wametulia mtaani kuzurura nakushabikia mpira na ishu ya madawa ya kulevya.
Magufuli; " vijana jiajirini hapa kazi tu"
Vijana wamekaa kimya(bomu linachemka)
5. Watumishi wa umma: Hofu imewatanda wanafanya kazi kwa hofu bila kuwa na utaratibu maalumu, matamko yanafanya watumishi kushindwa kufanya kazi kwa utaratibu.
Magufuli: " narudisha nidhamu"
Wamekaa kimyaa sio kwamba wanafurahia ni shida tu" bomu linachemka"
6. Bank na wateja wao: ongezeko la vat '
Wamekaa kimyaa: "bomu linachemka"
7. Timua timua ya wanafunzi chuo. TCU waliwapokea leo hawana vigezo,
mikopo shida.
Wamekaa kimya: "bomu linachemka"
8. Machinga
Magufuli: " mtu asiwaguse"
mikoa mingi wamepewa taarifa hawatakiwi barabarani bila kupangiwa sehemu rafiki, mfano mzuri yaliotokea Mwanza.
Machinga wako kimyaa " bomu linachemka"
Sijagusia:
Polisi.
Wanasiasa( wapinzani)
Utalii.
Viwanda.
NSSF
Wakulima
Makusanyo ya mapato.
Bunge
Makundi ndani ya chama chako.
Tahadhari mh Magufuli kukimbia tazizo sio njia ya kutatua tatizo. unatengeneza mabomu mengi sana.
Wanakuvumilia na siku zote uvumiliza una mwisho wake
Usipochukua hatua natabiri mtikisiko mkubwa ndani ya utawala wako.
Muda huu ni wa kuwa kazini, maneno ya nini?
Mkuu Kumbuka wale wanapata Maagizo kutoka juu sasa tusiwalaumuWasiojitambua hapa ni POLISI tu!
Acha kupotosha watu na kuingiza mijadala ya kiuchochezi na kampeni ndani yake wakati sio mda wake
prophetHuu ni utabiri au ni uchambuzi yakinifu?