UTABIRI: 2020 kama Rais Magufuli atashinda uchaguzi, Tanzania itaingia katika rekodi ambayo haijawahi kutokea

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,004
2,000
Itakuwaje siku siasa zikiruhusiwa na aliyezizuia? Je viongozi wa upinzani watakamatwa kwa uchochezi kwa kuwa watakayoyanena yatakuwa yanakosoa utawala uliopo? Je, wananchi watawaunga mkono kwasababu ya maisha magumu wanayopitia katika awamu hii? Au watawasusa kwa kuwa wanaishi maisha ya raha kuliko awamu zote zilizopita?

Miaka mitano (2015-2020) ikipita tukiendelea kuona na kuishi maisha hayahaya kama tunavyoyaona, je miaka mingine mitano ya mwisho (2020-2025) itakuwaje? Je, atafuata mkondo uleule wa Mseveni, Kagame, Nkurunzinza au Mugabe?

Je, watumishi, wakulima, wafanyabiashara, wanafunzi wa elimu ya juu na wananchi kwa ujumla, kwa maisha mnayoishi sasa hivi, itakuwaje baada ya 2020? Yataendelea kuwa hayahaya? Yatakuwa bora zaidi? Au yatakuwa magumu zaidi?

Tumuombe Mungu ili Wakurugenzi, Polisi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi watende haki mwaka huo maana yajayo YANAFIKIRISHA! yatabadili taswira ya Tanzania kitaifa na kimataifa.

Tunakuomba
Mungu Baba muweza wa yote, Mwaka huo utuepushe na mapungufu kama yale ya uchaguzi wa marudio wa Ukonga, Kinondoni, Siha na Kakonko.

Tunakuomba pia utuepushe na yale ya Uchaguzi mkuu wa 2015 wa Raisi, Wabunge na Madiwani. Yasitokee kama yale yaliyotokea Tabora, Nyamagana, Mtama na sehemu nyingine katika uchaguzi mkuu wa 2015, yasijirudie tena 2020.

Tunakuomba utujalie baraka zako kwasababu kuna mgombea hatakubali kirahisi iwapo matokeo halali yatabadilishwa/yatapindishwa. Ataungwa mkono na jumuia za kimataifa hivyo kuiweka nchi ya Tanzania katika historia mpya.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,771
2,000
Kwa taarifa yako vyombo vya kimamlaka vyote viongozi wake ni wateule wa rais kutokana na katiba mbovu. Hivyo wote penda wasipende wameshapewa maelekezo ya kumtangaza yeye na chama chake kuwa washindi. Lengo ni kumtangaza yeye kuwa mshindi kwa 90%+, na wagombea wa ccm kwa 95%, lengo ni ili kupata bunge litalomuongezea muda wa kukaa madarakani zaidi ya 10yrs.
 
anjnr

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
519
250

Endapo mwenyezi Mungu ataruhusu aishi hadi muda huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Andresen

Member
Feb 21, 2019
43
125
Kwa taarifa yako vyombo vya kimamlaka vyote viongozi wake ni wateule wa rais kutokana na katiba mbovu. Hivyo wote penda wasipende wameshapewa maelekezo ya kumtangaza yeye na chama chake kuwa washindi. Lengo ni kumtangaza yeye kuwa mshindi kwa 90%+, na wagombea wa ccm kwa 95%, lengo ni ili kupata bunge litalomuongezea muda wa kukaa madarakani zaidi ya 10yrs.
No
Nakuhakikishia kuwa 2020 ngosha hapiti ndani ya CCM, trust me my brother.
Mimi ni miungoni mwa nitakao Chukua form ya Urais kupitia chama changu cha CCM na wengi wataamua kiniunga mimi mkono na kuachana na jiwe maana wataona hatari iliyopo mbele Yao endapo jiwe atapewa awamu nyingine.

Kama huamini basi trust me, muda utaongea
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,026
2,000
Hilo liko wazi na halihitaji ubashiri wowote. Utashindwaje kushinda wakati mamlaka husika zote ziko chini yako?! Tume isiyo huru, Manjagu, wajeda, maDED, Msajili, n.k.
Katiba mbovu ya Nyerere kopi and paste toka kwa rafiki yake Mao wa China ya kuabudu MTU kuliko utaifa itambeba,atachaguliwa na katiba sio kwa ridhaa ya wengi.wengi watapotea,watauwawa,maisha yatakuwa magumu zaidi ya hapa,atakaa madarakani hadi Mungu akipenda.wabunge wote watakuwa wanamuwakilisha yye sio wananchi,probably 87% wakawa kabila moja
 
Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
6,398
2,000
Kwa taarifa yako vyombo vya kimamlaka vyote viongozi wake ni wateule wa rais kutokana na katiba mbovu. Hivyo wote penda wasipende wameshapewa maelekezo ya kumtangaza yeye na chama chake kuwa washindi. Lengo ni kumtangaza yeye kuwa mshindi kwa 90%+, na wagombea wa ccm kwa 95%, lengo ni ili kupata bunge litalomuongezea muda wa kukaa madarakani zaidi ya 10yrs.
Thubutu atapitia wapi huyo jiwe tukio tayari atumalize abaki yeye na Bashite tu .Ikibidi tushirikiane na mabeberu mpaka asepe .
 
2013

JF-Expert Member
Jan 1, 2013
11,331
2,000
Trust None,Mkuu Umetabiri kimakosa sana.

1. Watanzania wengi wakiumizwa na
Kupigika. Ndio watazidi kua watiifu na waaminifu kwa utawala huu.

Maisha Magumu Ni Moja ya Mambo huwafanya wananchi kudumaa kifikra na kimsimamo.

"MwanaNchi ni kama Mwanamke wa Kijijini. Jinsi anavyopigwa na Mumewe zaidi. Ndivyo anavyolinda ndoa yake asiachwe".

Kiongozi anayeweza kuondolewa Ni yule anaye wa empower watu wake waweze kufanya maamuzi wenyewe bila Kutegemea Serikali.

Lakini huwezi kuta haya kwenye nchi za kidikteta(Rogue States) kama North Korea, nk.

2. Watanzania wachague chama mbadala wa CCM, wanahitaji kuwekewa mezani Mbadala huo, ili Wakiutazama wasipate mashaka. Jambo lililo dhahiri zaidi Ni kwamba Ifikapo 2020 hata huo Upinzani hautakua na Pumzi ya kusimama Dhidi ya CCM ya JPM.
Kumbukeni misemo Tata iliyovuma 2015. Kama...
"Kuna Maisha baada ya Uchaguzi"

Yanayo wakumba wapinzani Leo ndio Maisha baada ya Uchaguzi wa mwaka Uleeee!!

#Save the date
 
blackcornshman

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
3,855
2,000
No
Nakuhakikishia kuwa 2020 ngosha hapiti ndani ya CCM, trust me my brother.
Mimi ni miungoni mwa nitakao Chukua form ya Urais kupitia chama changu cha CCM na wengi wataamua kiniunga mimi mkono na kuachana na jiwe maana wataona hatari iliyopo mbele Yao endapo jiwe atapewa awamu nyingine.

Kama huamini basi trust me, muda utaongea
Hahahaa 2020 siyo mbali inshallah.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom