Uswazi na misosi!

Uswazi na misosi!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,914
Hebu leo tucheke kidogo kwa kukumbushana pilika za enzi hizo utotoni hasa kwenye msosi

Kuna mambo ambayo ukiyakumbuka yalivyokuwa enzi hizo za utoto basi unaweza kucheka hadi mbavu zikauma hili ninalokwenda kulizungumzia hapa ni kwa wale tuliokulia uswazi na ambao bado tunaishi Uswazi maana wale watoto wa kishua hii hawakuijua kabisa hivyo wanaweza kuona kama ni hadithi tu

Moja kati ya jambo ambalo nikilikumbuka ni pale kwenye msosi unapokuwa umetengwa mezani,kwa zile familia zetu ambazo ailikuwa na uwezo wa chini kidogo kulipokuwa kunapikwa nyama basi siku hiyo kwenye msosi mezani zinaweza kupigwa ngumi kwa kugombea finyango za nyama,kwa kuepusha hilo wazazi walikuwa wanahesabu finyango kwa idadi yetu wote na kabla ya kuanza kula mlikuwa mnaambiwa "mtakula kila mmoja finyango mbilimbili" na baada ya hayo kila mmona alikuwa anatoa finyango zake na kuziweka kwenye bakuli kubwa au sinia ambalo ugali umewekwa na kuanza kuchovya mchuzi na mchika kama utakuwepo

Lakini kuna kitu amcacho nadhani kimetuathiri kutokana na hii kitu ya utotoni,huku ukubwani nimeona watu wengi sana wakiwa wanakula hasa kwetu ambao tunakula kwa mama ntilie,utaona kuwa mtu kama ameagiza wali na nyama au ugali na samaki basi nyama au samaki huachwa na kuja kuliwa mwishoni,sijui hii ni kwasababu gani

Lakini kwa uchunguzi wangu mdogo nimegundua kuwa ile dhana ya utotoni ya kuthamini sana vitoeo kama vile nyama husababisha kuona kama ni vya thamani sana na hupelekea watu kuacha na kuvila mwishoni ili auone utam wake .....lol

Nimeshaona wengi sana kwenye hili lakini kila nikiona huishiakucheka na kukumbuka mbali sana zile enzi za vurugu kwenye msosi

Vipi,wewe ukiwa kwenye msosi unaousisha kitoweo kama kuku,au nyama ya ng'ombe unaacha vile vi finyango hadi mwishoni au unakula bila kuzingatia kuwa kuna finyango?

Hebu tukumbuke kidogo na tufurahi na kucheka hizi enzi zetu za uswazi!!!!!!
 
Ha ha haa! Utafanya nikaangue kicheko kwa restaurant!
 
Ha ha haa! Utafanya nikaangue kicheko kwa restaurant!

Hahahahahaaaaaa!!!!!!!!!!

Mkuu angalia wasikuone kama vile una tatizo.............lol!!!!!!!!!
 
1465124_471983246245328_2005175894_n.jpg
 
Moja kati ya jambo ambalo nikilikumbuka ni pale kwenye msosi unapokuwa umetengwa mezani,kwa zile familia zetu ambazo ailikuwa na uwezo wa chini kidogo kulipokuwa kunapikwa nyama basi siku hiyo kwenye msosi mezani zinaweza kupigwa ngumi kwa kugombea finyango za nyama,kwa kuepusha hilo wazazi walikuwa wanahesabu finyango kwa idadi yetu wote na kabla ya kuanza kula mlikuwa mnaambiwa "mtakula kila mmoja finyango mbilimbili" na baada ya hayo kila mmona alikuwa anatoa finyango zake na kuziweka kwenye bakuli kubwa au sinia ambalo ugali umewekwa na kuanza kuchovya mchuzi na mchika kama utakuwepo
!

602801_435228543254132_1544932322_n.jpg
 
Mimi nilikulia familia bora pindi mshua alikuwa na pei kinyama ila sasa am back in thug life vokume 1.
 
Mi nilikuwa mtaalamu wa kwenda kula ubwabwa kwenye Maulid za watu mtaani.

Mida kama ya saa tano tano hivi unaanza kusikilizia harufu ya pilau.

Ile sinia linapelekwa na wewe huyo tayari ushasogea.

Halafu sasa kabla hata halijawekwa chini watu washaanza kudaka matonge ya nyama.

Mpaka linafika chini nyama zishaisha kilichobaki vifupa tu.

Mwananyamala Visiwani kuna vituko sana aisee.
 
Halafu kulikuwa na madogo wenye tabia mbaya...

Anaficha finyango zake na wengine wote mkimaliza yeye ndoa naanza kula kwa madaha kama paka aliyeshiba panya... Anawakera kiasi kwamba kama hana ubavu mnamvamia na kumpora....
 
hahahahhaha baba paroko nahisi unanisema mimi yaani mpaka leo nimeshazoea kuacha nyama ya mwisho hata ziwe finyango nyingi kiasi gani kwenye plate yangu lazima kipande kimoja nikile mwishooooo afu kaka zangu walikuwa wanachukia ile tabia tunakula pamoja then chakula kikianza kuisha wanaambiwa muachieni mtoto hapo mimi bichwaa hiloooo
 
kweli Eiyer, sisi tuliokulia uswazi huu mchezo umetuathiri sana, lakini haya mazingira unaweza kuyabadilisha kwa familia yako isiwe kama wewe ambae unafanya hadi sasa ukubwani! wazazi walifanya hivi votoweo kuwa ghali na vya thamani sana, japo hii inaendelea hadi sasa... lakini inaweza kubadilika na vikawa vya kawaida sana...
Nashukuru nimefanikiwa hilo....
 
Last edited by a moderator:
Nani humu keshahudhuria sherehe za kumtoa mwali?

Mie nshahudhuria ngoma za kumtoa mwali wa Kimakonde na Kizaramo.

Wacha kabisa bana....
 
Mi nilikuwa mtaalamu wa kwenda kula ubwabwa kwenye Maulid za watu mtaani.

Mida kama ya saa tano tano hivi unaanza kusikilizia harufu ya pilau.

Ile sinia linapelekwa na wewe huyo tayari ushasogea.

Halafu sasa kabla hata halijawekwa chini watu washaanza kudaka matonge ya nyama.

Mpaka linafika chini nyama zishaisha kilichobaki vifupa tu.

Mwananyamala Visiwani kuna vituko sana aisee.
Nyani umenikumbusha mbali hapo.... juzi kati nipo kwamtogole kule jirani na nilikwenda kuna harusi, nikamwambia jamaa yangu leo lazima nijikumbushie cha uswahilini.....! nikapiga goti nakula!
 
Last edited by a moderator:
Nyani umenikumbusha mbali hapo.... juzi kati nipo kwamtogole kule jirani na nilikwenda kuna harusi, nikamwambia jamaa yangu leo lazima nijikumbushie cha uswahilini.....! nikapiga goti nakula!

Hahaaaa sinia moja mikono ishirini!

Watu wanafinyanga matonge, wanalamba mikono, wanarudi tena kufinyanga.

Ni uchafu lakini kuna raha yake. Leo hii siwezi hata kula ugali na watu halafu wote tuwe tunachovya kwenye bakuli moja.
 
Back
Top Bottom