GHIBUU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 4,432
- 3,006
Ndugu Wa Tanzania
Tumepokea malalamiko ya watu wa rika mbali mbali toka mwaka jana juu ya mashirika ya ndege hapo Dar es salaam wanavyo wasumbua watanzania wanao taka kusafiri kwenda nchi za nje kwa sababu mbali mbali.
Vijana wanatafuta fursa mbali mbali za halal kabisa za kwenda nje ,kimatembezi wengine kikazi, wanapatiwa visa halali kabisa kutoka balozi za nchi.
Wanapo fika Airport kupatiwa boarding pass hapo ndio shughuli mpya, huwasumbua na kuwakatalia kuwapa ticket kwa kisingizio eti hawatarudi Tanzania, hivi wakirudi au wasirudi wewe kama shirika la ndege ni kazi yako ? Ni maamuzi ya mtu mwenyewe.
Mtu anapo fika nchi kama za ulaya ,America na Canada kuna fursa mbali mbali, kama ni mgeni halali kabisa, fursa za kuishi huko zipo kisheria, Sasa shirika unamnyima Mtanzania boarding pass kwani wewe ni nani ?
Na mbaya zaidi mashirika hupiga simu kwenye balozi wakati mwengine na kuziharibu visa zao wasafiri.
Tunaomba serikali , Uhamiaji na sector nyengine kutupia jicho haya mashirika na wasafiri kwa usumbufu wanao pata hapo Airport.
Rais Samia pamoja na mabalozi wetu wamekuwa wakitu hangaikia ndani na nje ya nchi ili tuweze kupata Ajira, na kukuza uchumi wetu
Ahsante
Diaspora