usoni amejaa sononi mashaka na woga

usoni amejaa sononi mashaka na woga

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,085
Ukimwangalia kwa haraka utafikiri ni mtu mzima lakini ni mtoto mdogo tu ,ndoto zake za maisha mema ya mafanikio na furaha yamekatishwa na mwanaume aliyejazwa tamaa ya ngono mharibifu na bazazi aso haya.

Ana mtoto mgongoni nguo zake na za mwanao zote chafu ana beseni la matunda au ungo wa ubuyu karanga au korosho mtaji wake haufiki elfu kumi anapita huku na kule na mwanae mgongoni akitafuta riziki yake na mwanae inahuzunisha mno.

Hayuko peke yake wako wengi wa aina hiyo wengine wakijiuza usiku na wateja wao wakuu wakiwa na haohao mabazazi wenye watoto kama hao wanakesha usiku kucha wakijiuza na kufanyiwa vitendo viovu mno vya udhalilishaji mkubwa.

Wanakamatwa ma sungusungu wanadaiwa pesa hawana wanapelekwa selo maskini ya Mungu mbona wateja wao hawakamatwi ?hawapigwi picha ?majina yao hayaandikwi na kutangazwa kwenye vyombo vya habari ? Mfumo dume huo!

Wanaume tufikirie mara mbili tunapotongoza watoto wadogo tunawaharibia future zao tunazima ndoto zao tunawaondolea furaha zao tunawaumiza mno tunawatesa.

Tunawapachika mimba kisha tunawatelekeza ,wazazi wanawatelekeza ndugu wanawatenga jamii inawacheka! tunajiundia laaana mbaya
Muda huu au kesho ukikutana naye kumbuka haya mwangalie kwa makini usoni utaona uso wake umejaa sononi na maumivu mengi rohoni

TUWAHURUMIE...!!!
 
UKIELEWEKA kwa msomaji kutumia akili na nguvu kubwa ni HATUA moja katika KUPOTEZA wasomaji wako
 
Life's not fair and survival will always be for the fittest,cha msingi jitahidi utoke huko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom