excel
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 22,463
- 17,958
Habari wana JF??
Nilikuwa nasikia story tu kuwa watu huanzia kwenye mitandao (jinsia tofauti) na hatimae kukutana uso kwa uso, kwa mara ya kwanza jana nimefanikiwa kukutana na member wa JF MMU tena ni gwiji (maarufu) humu.
Tulianza kwa kujibizana mara hivi mara vile kwa inbox then namba za simu hatimae naandika hapa huku yeye akiwa pembeni hapa anacheekaaa na kuomba nisimtaje jina lake la kwenye ulingo wetu wa MMU!!! Akiandika humu unaweza kudhani ni wa kimjini mjini sana lakini kumbe wapi, mtoto ni mzuri huyooo, halafu ni mpole na mtulivu sana kuongea kwenyewe ni mpaka umchokoze!!!
Kikubwa ninachotaka kusema hapa ni kwamba JF ikitumiwa vizuri inaleta marafiki, inakutanisha ndugu, unafanya biashara na hata yale mahusiano yanayozungumzwa sana kwenye ukumbi wa MMU!!
Bila Kusahau: Nimegundua pia kuwa watu humu JF wanapretend tabia na maisha, wanavaa uhusika si wakwao kabisa!! Mfano, kuna watu wanashawishi anasa na kujifanya wao maisha yao ni anasa tupu!!! Iga ufeee, watu wana maisha yao bana
Eeh!! Mwisho kabisa ni kwamba JF kuna wasichana wazuri asikwambie mtu!!
Nawasilisha
mkuu wanawake ama wadada wengi walio jf wanajitambua!
kuna mmoja nilikutana nae kwenye gari akiwa anatokea mnazi mmoja hivi anaelekea mitaa fulani ya mabibo hostel (tulipanda gari moja japo hakujua na mie ni mwana j,), for sure alikuwa ni mtu mwelewa sana pale alipomuokoa mzee fulani hivi asiibiwe pesa yake kama shs laki moja hivi!
mzee huyo alikuwa ameziweka zile pesa kwenye mfuko wa nyuma, basi zile pesa zooote zilikuwa zinaonekana!!! kiasi kwamba zilikuwa ni za ku-chop tu kwa vidole viwili!
she really impressed me though i didnt want to introduce myself so much to her!