Usiwakopeshe watu hawa

Usiwakopeshe watu hawa

Kuna askari mmoja jamaa yangu alikuja kunikopa mwanzo nilim test kumkopa elfu 30 hakuludisha so na mimi sikumkumbusha next time akapata tatizo la milioni na nilikua nnauwezo wa kumpa ila nikaona ndio itakua mwisho wa urafiki wetu nikampotezea.
Ungemwambia arudishe Ile 30 Kwanza!
 
Kwakweli ktk kukopesha naishiaga kutapeliwa au kushindwa kufuatilia deni.
Kuna jamaa mmoja kila nilipomuomba anikopeshe kiasi flan yy alinipa kiasi kidogo huku akinambia nisirejeshe.
Alifanya hivyo mara kadhaa..
Nikajifunza kwake.
Mtu akija kwangu kukopa laki 2..
Nampatia 50000 akatumie bila kunirejeshea.
Akija kukopa 50000 nampa 10000/15 kulingana na tatzo akatumie.
Aisee tangu apo naona sipati headache ya mikopo na kudai watu.
 
Kwenye kijiwe kimoja kuliibuka mjadala kuhusu uaminifu wa mkopwaji,kuna mzee mmoja alisema kwa kusisitiza kuwa "vijana wangu mkopeshe mtu yeyote lakini si kiongozi wako yeyote wa kiroho (mchungaji wako n.k, kiongozi wako yeyote wa kisiasa (mwenyekiti,katibu n.k),Hakimu mliyezoeana,Askari mliyezoeana".Kama ni kumpa mpe tu then usahau lakini usithubutu kumkopesha na utarajie kuwa atakurejeshea.

Je, ni kweli hao watu waliotajwa hawakopesheki? Na ni nini hasa kinachopelekea wasiwe wepesi kurejesha mkopo waliochukua kwa marafiki/jamaa zao?.

Mtu aliye karibu na viongozi wa dini na kuwafanya kuwa Mungu wake huyo ni mwehu na atengwe kama ukoma, mara nyingi watu kama hawa ni mambumbumbu na wanafki waliopitiliza tena hawafai ndani ya jamii.
 
Kwenye kijiwe kimoja kuliibuka mjadala kuhusu uaminifu wa mkopwaji,kuna mzee mmoja alisema kwa kusisitiza kuwa "vijana wangu mkopeshe mtu yeyote lakini si kiongozi wako yeyote wa kiroho (mchungaji wako n.k, kiongozi wako yeyote wa kisiasa (mwenyekiti,katibu n.k),Hakimu mliyezoeana,Askari mliyezoeana".Kama ni kumpa mpe tu then usahau lakini usithubutu kumkopesha na utarajie kuwa atakurejeshea.

Je, ni kweli hao watu waliotajwa hawakopesheki? Na ni nini hasa kinachopelekea wasiwe wepesi kurejesha mkopo waliochukua kwa marafiki/jamaa zao?.
Umesahau mchepuko
 
Kingine ni biashara za ahadi ya malipo ya tarehe flani (Promissory Notes). Kwa wabongo ni sumu usijaribu huwa hawajali muda!

Hii kitu imenisababishia headaches mpaka sasa hata kusafiri nashindwa. Kuna mtu nimemuuzia mali kalipia Advance ila kumalizia mkia ndio imekuwa shughuli.

Tunasumbuana mpaka nafikiria nikamfungulie kesi polisi. Anakera kinoma yani. Biashara ya 19/5 akaahidi kumalizia 2/6 ila hajafanya hivyo mpaka sasa ni story nyingi tu mara msiba, mara vile mwisho ananiambia nimepambana nimeshindwa labda mpaka mwisho wa mwezi. Ina maana nipoteze mwezi wote wa 6 bure tu!

Mwengine ni ex classmate nae wa Tarehe 9/4 akaahidi by tarehe 30/4 anamaliza. Imefika siku ya kulipa hela hana, akanipiga sound mpaka 15/5 hela yenyewe akatoa nusu. Tumesumbuana tarehe 23/5 akatoa tena nusu ya iliobaki. Toka na hapo hela hajamalizia tena kila nikimcheki anapambana mambo magumu.
 
Andikishaneni akizingua sheria ipo wabongo mnawaza ngono tu!

Sasa wee unataka tuwaze nini mkuu ebu tuambie.

Maana ata huyo mfalme sulemani aloyekuwa tajiri akaangalia na akona kuwa vyote hivi ni ubatili.
 
Back
Top Bottom