Usiwakopeshe watu hawa

Usiwakopeshe watu hawa

Joined
Jul 28, 2019
Posts
6
Reaction score
2
Kwenye kijiwe kimoja kuliibuka mjadala kuhusu uaminifu wa mkopwaji,kuna mzee mmoja alisema kwa kusisitiza kuwa "vijana wangu mkopeshe mtu yeyote lakini si kiongozi wako yeyote wa kiroho (mchungaji wako n.k, kiongozi wako yeyote wa kisiasa (mwenyekiti,katibu n.k),Hakimu mliyezoeana,Askari mliyezoeana".Kama ni kumpa mpe tu then usahau lakini usithubutu kumkopesha na utarajie kuwa atakurejeshea.

Je, ni kweli hao watu waliotajwa hawakopesheki? Na ni nini hasa kinachopelekea wasiwe wepesi kurejesha mkopo waliochukua kwa marafiki/jamaa zao?.
 
Kuna askari mmoja jamaa yangu alikuja kunikopa mwanzo nilim test kumkopa elfu 30 hakuludisha so na mimi sikumkumbusha next time akapata tatizo la milioni na nilikua nnauwezo wa kumpa ila nikaona ndio itakua mwisho wa urafiki wetu nikampotezea.
 
IMEANDIKWA : ".... naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo"

MATHAYO 5:42b



JESUS IS LORD!
 
Kuna rafiki alinikopesha laki 6. Sijamlipa hadi leo mwaka wa 4. Sina amani kabisa moyoni maana sikukusudia ila mambo yalikwenda kombo.

Mungu nisaidie nimlipe pesa yake.
Kabisaaa, bora ulipe mzeee...
Mimi kwa kweli sina amani kabisa nikivusha deni..
Ila kuna wanyabe sijui wameumbwajeee...
Yaani yeye Hayupo tayari kurudisha deni na hawazi....

Na hamnaga kesi ngumu kama za madai...
 
kama ulidhani umemuelewa sana mzee wako,kopesha yeyote ukiwa na uhakika 100 pesa itarudi😁😁😁😁.

ndio maana wengine ukija kutukopa,hatukupi uliyoomba tunakupa 50% ili ukiamua kusepa nayo ikusaidie uendako.
 
Kabisaaa, bora ulipe mzeee...
Mimi kwa kweli sina amani kabisa nikivusha deni..
Ila kuna wanyabe sijui wameumbwajeee...
Yaani yeye Hayupo tayari kurudisha deni na hawazi....

Na hamnaga kesi ngumu kama za madai...
Ni kweli. Nilishaongea nae tukakubaliana kumlipa kidogo kidogo.

Sijui wanaodhulumu huwa na roho ganif
 
Kuna rafiki alinikopesha laki 6. Sijamlipa hadi leo mwaka wa 4. Sina amani kabisa moyoni maana sikukusudia ila mambo yalikwenda kombo.

Mungu nisaidie nimlipe pesa yake.
Miaka 4 hujapunguza deni hata kidogo? Hata kama mambo yamekwenda kombo unatakiwa uonyeshe nia ya kulipa kwa kuanza kupunguza kidogokidogo.
 
Back
Top Bottom