Usivunje mtungi ili kumuua Panya!

Usivunje mtungi ili kumuua Panya!

Lipanya lenyewe limekuwa kubwa haliwezi hata kupenya kwenye mdomo wa mtungi, sijui hata wakiinamisha kama litaweza kutoka, ni lina vitoto vingi balaa,
panya kashakuwa na kambi vitioto navyo vimezaliana mtungi hautoshi kuwabeba kiasi kwamba siku wakiinamisha mtungi utapasuka hapo hapo, na panya watatokomea na mtungi watakosa, UKAWA WILL TAKE CHARGE WASIPOTEZE VYOTE WAO WALEE PANYA WAO.
 
Na kwa vile panya hawajui cha mpango wa uzazi,CCM wajiandae kuliwa.

Tatizo hawataki kusikia yaani sijui tuwafanyeje.Inabidi UKAWA waandae INDOCID tu ya kuwamaliza maana ili vihenge vipone tunahitaji INDOCID na unga kidogo tu kama kilo hivi................
 
Ah,wadhani hivyo?Kumbuka Mwenyenyumba kesha ozesha watoto wake kwa huyo panya,unadhani watoto watamkimbia baba yao?Hata kidaogo.Na kumbuka Babu ya watoto naye hawezi kuwakimbia wajuuze maana ni damu yake pia....................

Watu wa dunia wanasema ili tukujue TABIA yako utwambie RAFIKIYO,then tutakujua vyema au wasemaje bro?

Ngoja niendelee kufikiria ulichoandika ntakuja i will be back midamida
 
Ngoja niendelee kufikiria ulichoandika ntakuja i will be back midamida

Ninamaana hivi Watoto wa mwenye nyumba wameshazalishwa na PANYA,na WAJUKUU weshatokea,je wadhani BABU atawakaa WAJUKUU ZAKE?Je na watoto waliozaliwa watamkimbia BABA yao PANYA?

Nikazidi kukwambia hivi ili tujue tabia yako tutakuuliza rafiki zako..............
 
kwa mantiki hiyo Charles Makongoro Nyerere ndiye anayestahili kuwa mgombea wa urais kupitia CCM kwa sababu ndio mtu pekee anayeweza kukirejeshea chama umoja mshikamano na nidhamu. Na isitoshe sio mnafiki na hana kisasi na mtu isipokuwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za chama.

maamuzi magumu, ni udikteka, na safari ya matumaini ni ishara ya kutokuwa na uhakika.

Wakati wapinga ufisadi wanamuona MN ndiye atakayeunganisha ukoo wa panya MAFISADI wanamuona kama atawawekea usiku. Hii vita sio ndogo
 
Sasa nape anaanza kukua...ujana na hamaki za ujana kuona mambo yanafanyika haraka na majibu yake kupatikana haraka sasa yanaanza kupotea ndani ya kijana nape..huo ndio uzuri wa kufanya kazi na watu wazima waliopitia UPS and DOWN kwenye mambo mengi.Kwa busara za wazee wenye kufikiria mbali Nape sasa anaanza kuvuna maarifa ya ziada kuwa PATIENCE kwenye maswala nyeti utoa majibu mujarabu na kukupa maarifa ya ziada ya kupambana na matatizo mengine yajayo kwa uangalifu.

Ukiwa kijana unapokutana na matatizo unakuwa na muhemuko wa kulitatua kwa haraka haraka kwa kutumia njia ambazo wewe kama kijana unao kuwa zina majibu toshelezi ya utatuzi wa tatizo lina kukabili.Kumbe kwa tatizo kama hilo lako kuna watu wazima walishakumbana nalo na njia unayotka kupitia nawo kwa dhama zao walishapitia likawa gharimu na wakajifunza kwa makosa yao wenyewe.Sasa kupitia kuwa nao karibu Nape kama kijana anapata fursa ya kujifunza kupitia uzoefu waliovuna watu wazima katika kukabiliana na mambo mazito ndani ya chama chao.

Kwa haraka za ujana ndizo zilizo msababisha Zito na wenzie kuchemka ndani ya CDM na hivyo kuibua songombingo nzito iliyozaa jina USALITI ..lakini kama wangekuwa wasikivu na kupata busara za wazee watu wazima uenda wangepata majibu ya maswali yao na mahitaji yao kwa kuvuta subira.Waswahili walisema subira yavuta heri..ni kweli ..mambi ya UFISADI wa baadhi ya CCMM kuna kipindi yalipatwa kujadilika kwa kasi ndini ya CCM kwa jina la KUJIVUA GAMBA.Lakini kutokanna na kuwa unaposema Ufisadi unaamnisha ni maslahi HARAMU ya watu ndani ya TAIFA.Linapokuja kuwa ni maslahi ya watu hakika kuwaondolea watu hao maslahi hayo HARAMU ni VITA ya kutoa uhai wa baadhi ya watu...Kwa kuwa WANAONYANGANYA maslahi hayo AKILI zao na MAWAZO yao uwa ni kuwa MASLAHI yale NI YAO na ni HAKI yao chini ya kivuli cha UMOJA wao.

Kuwatoa kwenye FIKRA hizo na kuwarudisha kwenye uhalisia ugeuka kuwa na ugomvi tena mkubwa na ufikia kutishia USALAMA WA TAIFA kwa kuwa waliofika uko uwa washijijengea UFALME [Empire] kubwa kwenye jamii,tunawaona kama Wazito, wakubwa, matajiri, wanene, vibopa, na majina kedekede yakiwazunguka kudhihirisha neema hiyo ya wizi wa mali ya umma na kujimilkisha binafsi.

Sasa anachokisema Nape ni zoezi zima la wazrendo wa Taifa [Mtungi] kuahakikisha kile kilichoingia kwenye mtungi na kuharibu maji yaliyomo mtungini kinatoka bila kuingiza chochote kile kinachoweza kuhalibu au kubomoa Mtungi.Kwa kuwa bidii yoyote ya kutaka kutoa kilichomo mtungini kitapelekea kuchagwiza na mtafaruku utakao kuwa unatokea ndani ya Mtungi na kuwatia hofu wanaotia bidii ya kutoa Panya aliyedumbukia Mtungini.

Sasa taaraaaatibu unanyanyua mtungi nakuelekeza pole pole mdomo wa mtungi chini uku wengine wakiwa na fimbo, na silaha yoyote liwe fagio, gongo, nk mara tu akidondoka chini ya mdomo wa Mtungi Panya anakula kipondo cha kufa na akibahatika kupona basi ndani ya nyumba na Mtungini hatokanyaga maisha yake yote.Safiii sana Nape sasa unaanza kukua na kuongeza ufahamu wa kubeba mambo mzito kifuani huku yakishughurikiwa katika namna ambazo ni very confusing kama akili haijajiandaa kupokea unaweza kukimbia na kuacha kazi.Hongera kwa dongo zuriii lenye ujuzi mwingi sana kwa wenye ufahamu unaongeza ufahamu kuwa kumbe hatua zinasogea na majibu yanakaribia MWISHO
 
ImageUploadedByJamiiForums1433281310.782409.jpg

Kupitia ukurasa wake wa twitter amemuambia makongoro hivyo. Anataka kutuaminisha kuwa makongoro ndo ameshachaguliwa au?
 
Hahhaaha aisee wasie mpenda nape wale malimao
Nape kwenye ubora wake
 
Lowasa akishinda nape atakuwa mkimbizi
 
chukua za nape changanya na zako then sepa
 
Sifa za uongozi mbovu hizo iwapo mawasiliano ya muhiumu yanafanyika kutumia twitter
 
View attachment 256569

Kupitia ukurasa wake wa twitter amemuambia makongoro hivyo. Anataka kutuaminisha kuwa makongoro ndo ameshachaguliwa au?

nadhani Makongoro hawezi kupita ndani ya chama.
Nadhani ni kati ya Mwigulu au Muhongo, hawa ndio watamprotect JK akitoka madarakani.
 
Dawa ya lowasa iko tayari sauti ya simba inaunguruma kazi ishaanza taratibu japo itakuwa kubwa sana kuanzia leo pale dodoma baada ya kuchukua fomu.

makongoro kwenye ubora wake bana twende makongoro tukanyooshe mafisadi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom